Fahamu kuhusu muigizaji N!xau maarufu kama Bushman

Fahamu kuhusu muigizaji N!xau maarufu kama Bushman

Movie zake nzuri sana nazipenda mpaka kesho.
 
Code:
HISTORIA: MFAHAMU "BUSHMAN" MCHEZA FILAMU MAARUFU ZAIDI KUWAHI KUTOKEA BARANI AFRIKA.
Jina lake halisi anaitwa Nixau. Inakadiriwa alizaliwa kati ya mwaka 1943 au 1944, kwani yeye binafsi hakuwa akijua umri wake. Alikuwa ni mzaliwa wa nchini Namibia kijiji cha Tsumkwe katika Jangwa la Kalahari.
Hakuwahi kujifunza sanaa ya uigizaji hapo kabla, kwa sababu huyu alikuwa ni mtu pori halisi [yaani kama vile anavyoishi kwenye movie zake basi huo ndio uhalisia wa maisha yake aliyokuwa akiishi hapo kabla] hivyo katika maisha ya porini na Jangwani hakukuwa na sanaa ya maigizo.
Ila wazungu walimtafuta mtu ambaye alikuwa ni Bush man halisi ili wamuweke kwenye movie zao ndipo wakakutana na huyu bwana.
Hivyo alianza maisha yake mapya ya uchezaji filamu mwaka 1980 -1994. Zifuatazo ni filamu maarufu zaidi alizopata kucheza na zikaja kuwa kubwa zaidi ulimwenguni kote hata kufanikiwa kujishindia TUZO mbalimbali:
1. The Gods Must Be Crazy II,
2. Crazy Safari,
3. Crazy Hong Kong, na
4. The Gods Must Be Funny in China".
Katika movie yake ya kwanza ambayo ni "The Gods Must Be Crazy "alilipwa dollars 300 tu za Kimarekani, ambazo kiuhalisia ni kiasi kidogo mno cha pesa, lakini hela hizo zote alizichana sababu hakuwa akijua matumizi ya hela kwa sababu hapo awali hakuwa kutumia hela.
Ila baadae baadae alifundishwa umuhimu wa kutumia hela, hivyo katika filamu zilizofuata akaanza kudai malipo tena makubwa kweli kweli.
Pia kabla ya kucheza filamu yake ya kwanza alikuwa bado hajawahi kuwaona Wazungu machoni pake, tena hakuwa amewahi kufika mjini.
Baada ya kumaliza maisha yake ya uigizaji huko Ughaibuni ndipo aliporudi nchini kwao Namibia, ndipo alipoanza maisha mapya alijenga nyumba nzuri ya kifahari kisha akaanza kujihusisha kwa shughuli za kilimo na ufugaji, ambapo katika mifugo aliyokuwa akifuga haikuzidi idadi ya 20, na hiyo ni kwa sababu hakuwa akiweza kuhesabu zaidi ya 20.
Lakini bado hakuacha tamaduni yao ya Uwindaji hivyo aliendelea kuwa hivyo licha ya utajiri aliokuwa nao.
Nchini kwao Namibia anaheshimika mno kuwa ndiye Msanii mkubwa na mtu maarufu zaidi kuwahi kutokea nchini mwao.
Hapo kabla hakuwa na dini hivyo mwaka 2000 ndipo alipoamua kubatizwa na kuwa Msabato. Hatimaye tarehe 1 July 2003, alifariki baada ya kuugua kifua kikuu
kilichokomaa ugonjwa alioupata kutokana na baridi ya uwindaji wa ndege usiku.
Anakadiriwa kufa akiwa na miaka 59 baada ya kufariki alizikwa kwenye makaburi ya asili huko Tsumkwe mnamo 12 July 2003 pembeni mwa kaburi la mke wake wa pili, aliacha watoto 6.
Comment R. I. P kumtakia pumziko jema Mr. Bushman.
The Diplomats.....
 
Ivi ile ya wale watt wake wanapotea anakutan nao mwishon inaitwaje?
 
View attachment 616101

N!xau [HASHTAG]#Toma[/HASHTAG] ni mzaliwa wa Namibia katika kabila la San ambao wengi ni Bushman. Alikuwa hajui miaka yake. Kabla ya kuanza kuigiza, alikuwa hajui chochote kuhusu maisha ya kisasa “ Modern Civilization “. Alikuwa ashawahi kuona wazungu wa tatu tu kabla ya kuigiza na alikuwa hajui thamani ya fedha. Mshahara wake wa kwanza kupitia filamu ya “ The Gods Must Be Crazy” 300$ ulipeperushwa na upepo.

Alikuwa ametoka kwenye utamaduni ambao haukujua thamani ya fedha wala kuelewa matumizi yake. Ila baadae aliweza kutumia hela yake kujenga nyumba ya matofali yenye maji na umeme.

Filamu zake ziliingiza mapato mengi sana kwenye box office. Baada ya kustaafu uigizaji, alirudi namibia na akawa mkulima wa Maindi na maharage, alikuwa mfugaji wa ng’ombe ila hawakuzidi 20. Gazeti la “ the independent “ linaeleza kuwa alifanya hivyo kwa sababu alikuwa hajui kuhesabu zaidi ya 20.

Alifariki Julai 5 mwaka 2003. Julai mosi alienda kuwinda na hakurudi, familia yake iliupata mwili wake siku nne baadae. Ameacha mke mmoja na watoto 6.


John snow [emoji300]️.
Kipindi Usher Raymond ana tofaut na 50 cent, jamaa wa G-unit walikuwa wakimkejeli ya kuwa huyu jamaa ni uncle wake
 
Back
Top Bottom