complex31
JF-Expert Member
- Jun 15, 2016
- 421
- 1,289
Kumekua na ushindani mkubwa sana miaka ya hivi karibuni kwa wamiliki wa bus kati ya kampuni ya Scania kutoka Sweden na kampuni za Kichina.
Scania
Hizi ni gari ambazo ni himilivu sana kwenye mazingira ya barabara zetu nyingi. Bus za Scania zimezihirisha uwezo wake wa kufanya safari kila siku kwa kipindi cha mwaka mzima bila kupumzishwa.
Mfumo wa Engine za hizi bus nyingi zinatumia engine model ya 94. Upande wa body zinatengenezwa na kampuni kama Marcopolo kutoka Brazil, Gemilang kutoka Malaysia na Body by Dar coach kutoka hapa kwetu nyumbani Tanzania. Hizi body za hizi bus ndio zinapelekea bei zake kua ghali sana watu wengi washindwe kuhimili.
Body za Marcopolo Model ya G7 1050 ambazo kwa bongo wanamiliku Dar Express na shule ya Kaizerege gharama yake ni 850mil na ushee
Hizi body zinauzwa ghali kutokana na bidhaa zinazotengenezea “fibre glass” hivo hua ngumu kuchaa au kuharibika kutokana na mazingira iwe joto au baridi.
Model nyingine za hizi body za Marcopolo ni kama G6 ambazo kwa bongo ziko nyingi mfano Kilimanjaro Express, Irizar Centrury alikua nazo pia Dar express
Aina nyingine ya body ni Gemilang hizi pia ni himivu sana, mfano kwa mabus ya Sauli, Dar express hizi mpya, Rungwe express n.k
Gharama za hizi body pamoja na Chasis ya Scania inakadiriwa kua kwenye 500mil na ushee.
Pia kuna Body by Dar Coach Model ya Crystal na Tanzanite zinazotengenezwa hapa bongo.
Mwisho kwa upande wa Scania kuna body za kuunda hapa hapa nyumbani amabzo nyingi ndio zilikua kiinua mgongo kwa wamiliki wa mabus wa miaka ya 2000 kama Buffalo Coach, Kapricon, Ngorika na mengine.
Bus za “Kichina” kutoka China ambazo zenyewe kwanzia Engine, Gearbox mpaka body huundwa na kampuni za huko huko kwao kama Cummins, Dongfeng n.k
Yutong
Hizi ndio zilikua bus za kwanza kuletwa bongo kutoka China na kampuni kama Ibra Line na Abood.
Kuna model kama F9, F12, F12+ n.k kwa upande wa hizi ni himilivu kiasi kwenye barabara za Tanzania ukilinganisha na model nyingine ya hizi bus.
Zimetoka soko kubwa la usafiri kutokana na bei pia Mnunuzi anaweza kuchagua awekewe Seat ngapi, za ukubwa gani pamoja na viburudisho vingine ikiwa ni tofauti na hizi Za Marcopolo.
Upande wa biashara huweza kurudisha faida katika kipindi kifupi lakini gari hizi ni ngumu sana kuikuta barabarani baada ya miaka 2 hadi 3 hivo baadhi ya kampuni hua engine ikianza kusumbua hutoa na kuweka ya Scania mfano Kilimanjaro Express BVA na ADJ.
Zhongtong na Golden Dragon hizi mara nyingi baada ya mwaka mmoja na nusu engine huanza kusumbua, kuharibika katikati ya safari ni kwaida. Lakini hurudisha mtaji na kukupa faida kwa kipindi kifupi.
Higer, Sunlong, AsiaStar
Hizi ni bus ambazo zinawahi kuchoka na kusumbua engine kwa kipindi kifupi kama itakua inaenda route ya mbali mfano Dar Mwanza.
Ni bus ambazo ni himilivu sana kwa route fupi kama Dar Dodoma na huweza kukupa faida kwa kipindi kifupi.
Hivo kwa anaetaka kufanya bishara hii ya magari ya kubeba abiria na kutaka faida kwa kipindi kifupi ushauri wangu ni kununua bus zinazotengenzwa China na kuitaftia route isiozidi 600km.
Kwa wenye uwezo na kutaka faida kubwa kwenge long run, unashauriwa kununua Scania G6 au G7 au Gemilang utaweza kuipa route ya 1800km kwa siku na zaidi ikaenda na kurudi mwaka mzima bila matatizo makubwa makubwa ya engine.