Fahamu kuhusu Scania Buses VS Yutong, Kinglong, Zhongtong, Higer, Golden Dragon, Sunlong Buses

Mkuu sababu za engine kusumbua kwa hii nchi yetu sio ubovu wa chombo, most of the times ni uzembe wa kibinadam

Wote tunajua uimara wa engine za benz lakin kampun ya Sauli washaua engine ya lile benz DPC, utasema benz mbovu? Gari inaenda mwezi mzima dar mbeya bila kucheckiwa

Mfano wa gari za kichina zilizodum zaid ya miaka 5 ni higer za upendo (Iringa-dar) yutong f10 za super feo (vipisi vile) New force za Moro-dar.......

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Gari ya kichina hata uitunze vipi, ukinipa mishe mishe tu lazima isumbue, ukiona mtu amesurvive kwa muda mrefu na Gari ya kichina basi ujue anafanya kazi nyepesi nyepesi, kama vile abood

Sijui unazumgungumzia higer ipi ya upendo, nafa hamu zile za mwanzo zilipaki muda sana, kwanza katika magari mabovu ya mchina hiyo higer nadhan inashika namba Moja, nimeshuhudia nyingi tu zikikata chassis, imagine basi, la kubeba watu 55 linakata chassis!!!

Superfeo unazosema vipisi, hazinaga route ndefu ndo mana zimedumu kuna mtu alinunua hizo you tong ndogo wakati zinaingia, akawa anapeleka mwanza to mbeya, haikukaa hata miezi Sita ikafa

Tukija kwenye Mercedes benz, hizo Zina Jina tu, ingia . Truck net forum hata siku Moja uone kama benz inasemwa vizuri, kitu pekee benz inatamba ni fuel consumption, pamoja na drive train imara, lakini kwenye swala la kudumu inaachwa mbali sana na Swedish,

Sent from my BKK-AL10 using Tapatalk
 
Higer za upendo bado zipo barabaran, ndo gari pekee anazotumia Iringa-dar,

Yutong za super feo zimepiga root ngumu tu, sidhan kama km 400 za songea-iringa au songea-mbeya ni route nyepes, bado nasimamia kwny suala la matunzo. Hata sauli pamoja na kuwa na 95 scania kama atakua anatembeza gari kila siku bila kupumzisha haziwez kutoboa miaka miwili bila kuweka engine mpya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Songe-iringa ruti ngumu sana milima kama yote songea-njombe
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Si vema kutoa ushuhuda kwa mambo ya watu ila Superfeo amepaki hizo youtong nyingi tu kwa route hiyo hiyo fupi.

Scania inahitaji maintanace na services tu, Swala la kupumzika sio ishu kubwa, hata ninesahau ni mara ngapi tume wahi kusafiri kwa masaa 36 bila kuzima (scania truck) kwa Gari ambayo ilikuja nchi likiwa mtumba wa mwaka 2003 uliotembea 1.6 million km, na hadi Leo hii ni miaka Sita toka liingie bongo na lipo barabarani. Kusema 95 itakufa Kwa kutopumzika ni ndoto za mchana

Sent from my BKK-AL10 using Tapatalk
 
Ile kauli mbiu ya Scania, when I grow up I want to be a scania.

Hivi hua naona mabasi ya Volvo,Actros na mengine huko ulaya kwenye tv ila mbona bongo siyaoni?

Volvo ziko bongo kama Majinjah anayo, Actros ni kwa magari ya mazigo zipo pia tatizo ni kwenye bei ya kununulia ni ghali sana hivo wenye uwezo ni wachache pia maintenance cost zake ni kubwa
 
Ile volvo ya majinjah iko njema sana ila ni ya kizamani mno uzuri mashine iko mang'anyu.
Volvo ziko bongo kama Majinjah anayo, Actros ni kwa magari ya mazigo zipo pia tatizo ni kwenye bei ya kununulia ni ghali sana hivo wenye uwezo ni wachache pia maintenance cost zake ni kubwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Volvo ziko bongo kama Majinjah anayo, Actros ni kwa magari ya mazigo zipo pia tatizo ni kwenye bei ya kununulia ni ghali sana hivo wenye uwezo ni wachache pia maintenance cost zake ni kubwa
Mercedes benz bei ghali kuliko scania ikiwa used. Sababu ni kuwa ili Mercedes ikubali kufanya second life Africa ni lazima ununue ikiwa premium toka huko ulaya, yani liwe jipya jipya, hapa unazungumzia km 400,000 to 700000 max, na Hilo ulaya mb ikifika hizo km Wanaiweka sokoni

Sababu ya mlundikano wa scania Tanzania ni kuwa Kutokana na uwezo wake wa kushikilia maisha, huwa zinatumika kwa miaka mingi Sana huko ulaya, si ajabu kukuta scania imetumiaka Km hata milioni na nusu huko, na hapa ikaja kufanya kazi vizuri


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo bei ya mabasi ya scania kununuliwa kwa 500-800ML na kampuni ya Dar Express mimi nakataa kabisa. Sio kweli. Hapo umetia chumvi nyingi sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…