Nawashauri wale mnaotaka kuanzisha VICOBA, muachane na mpango huo na badala yake muanzishe vikundi vya kijamii vinavyofanya kazi kwa urahisi zaidi. Anzisha kikundi cha HISA ambacho muda wake wa kufanya kazi unaeleweka na mambo yakienda kombo mtu unachomoa kilicho chako unaendelea na mambo mengine. Ila kiukweli vikundi vya HISA vinazalisha sana hela kwa sababu mtu analazimika kuwekeza kila wiki na kama program itaenda hadi miezi 12 kuna uwezekano mtu akawekeza Tshs. 1,000,000/= na mwisho wa mwaka akapata zaidi ya 2,000,000/=.
Hii program nimeanza nayo kuifundisha wakati ikiitwa SILK; baadaye ndo ikapanuka na sasa naona inawasaidia wengi. Mwenye maswali kuhusu kikundi cha HISA anaweza kuniuliza lakini VICOBA ni mpango wa mtu mmoja ambapo mwisho wa siku anapata faida kubwa. HISA hakuna anayemnyonya mwenzake hata siku moja.
Kila la kheri.