jackderick
Member
- Dec 31, 2012
- 29
- 9
Habari wadau,
Najua wengi wenu mko poa. Naomba tupeane maujuzi jinsi ya kusajili kikundi kidogo cha vijana mama 15. Hivi ni mchakato gani tufate na ni ofisi gani inafanya hii kazi?
Kwenu wadau
Kama huko zenji kuna ofc ya maendeleo ya jamii nendeni mkawaone watawasaidia. Ila kama mnaogopa riba nawashauri msiendeKwanza Samahanini sana wakuu, Ni mara yangu ya kwanza kupost kitu naombeni ushauri kwa yeyote anayefahamu vizuri michakato ya kusajili vikoba, Ni ofsi gani ya serikali inayohusika na usajili wa vikundi vay vicoba? ninawadau wenzangu tunataka kuunganisha nguvu ili tuweze kujikwamua kiuchumi but tunahitaji tusifanye mambo kinyemela sasa kwa niaba ya wenzangu naomba mwenye kujua michakato ya mambo haya aweze kutusaidia, Tupo zanzibar na pia kama kwa huku zanzibar kama kuna mtaalamu wa mambo ya vicoba tungependa kukutana naye ili aweze kutupa darasa.
nawasilisha samahanini sana wakuu.
Asante kwa ufafanuzi.
Ukweli ni kuwa sijawi kufikiria kuwa VICOBA vina-operate mjini. Maana hata neno Village linamaanisha kijiji. Nilifikiria vipo vijijini kutokana na Mabenki mengi yanayo-operate mjini kushindwa kuwafikia wanavijiji na hivyo kuvifanya VICOBA kuwa mbadala. Thanks, nimejifunza kitu.
VICOBA vina- operate hata mjini ndugu, hii nikutokana na commercial bank, kuwa na riba kubwa, dhamana/collateral kwa ajili ya kupata mkopo. Sio wote waliopo mjini wanaweza pata dhamana inayowezesha kupata mikopo benki, hii ni miongoni mwa sababu za kuanzishwa kwa Vicoba.
Kuna MTU anajiita yemco instagramuni huko mcheki,Nimeanza kufuatilia Mada kuhusu vicoba hivi karibuni. Nimebaini mijadala kuhusu mada hii kuhusu uanzishaji na uendeshaji wa vicoba imeishia 2017. Naweza kupata mdau wa kunisaidia kupata literature kuhusu kuanzisha na kuendesha kikundi cha vicoba? Nikipata contact ya mtaalam anayeweza kunisaidia itakuwa bora zaidi. Mimi naishi Dar, Wilaya ya Kinondoni.
Nawashauri wale mnaotaka kuanzisha VICOBA, muachane na mpango huo na badala yake muanzishe vikundi vya kijamii vinavyofanya kazi kwa urahisi zaidi. Anzisha kikundi cha HISA ambacho muda wake wa kufanya kazi unaeleweka na mambo yakienda kombo mtu unachomoa kilicho chako unaendelea na mambo mengine. Ila kiukweli vikundi vya HISA vinazalisha sana hela kwa sababu mtu analazimika kuwekeza kila wiki na kama program itaenda hadi miezi 12 kuna uwezekano mtu akawekeza Tshs. 1,000,000/= na mwisho wa mwaka akapata zaidi ya 2,000,000/=.
Hii program nimeanza nayo kuifundisha wakati ikiitwa SILK; baadaye ndo ikapanuka na sasa naona inawasaidia wengi. Mwenye maswali kuhusu kikundi cha HISA anaweza kuniuliza lakini VICOBA ni mpango wa mtu mmoja ambapo mwisho wa siku anapata faida kubwa. HISA hakuna anayemnyonya mwenzake hata siku moja.
Kila la kheri.