Fahamu kwa kina kuhusu suala la nyongeza ya mshahara

Monica Mgeni

Member
Joined
Oct 7, 2021
Posts
82
Reaction score
134
Mwalimu Ester Shayo
Moshi
22.07.2022

Nimepita katika mitandaoni nimeona maoni mbalimbali ya watumishi wa umma mbalimbali kuhusu ongezeko la mishahara yao katika mwaka wa fedha wa 2022/ 2023, baada ya Serikali kutangaza kuwa mishahara itaongezeka kwa 23.3%

Nimegundua kuwa baadhi ya wananchi wakiwemo watumishi wa umma hawakujua kuwa ongezeko la 23% lilikuwa kwa ajili ya kuwainua watumishi wa umma wenye mishahara ya kima cha chini.

Sasa nawafumbua macho ili kuondoa upotoshaji uliopo kutokana na uelewa mdogo uliopo juu ya suala hilo.

Ukweli ni kwamba katika mshahara uliongia siku ya leo watumishi wenye mishahara ya kima cha chini wameona kuwa kuna ongezeko kubwa katika mishahara yao, Ila watumishi wenye mishahara mikubwa wameona kuwa ongezeko ni dogo.

Hivyo basi hii inamaanisha kuwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais SAMIA SULUHU HASSAN imetekeleza ahadi ya kuboresha maslahi ya watumishi wa Umma wenye kipato cha chini kwa maslahi mapana ya Taifa na jamii kwa ujumla.

Nina imani kuwa kwa dhamira kuu ya Rais SAMIA SULUHU HASSAN huu ni mwanzo tu ila yajayo yanafurahisha kwa kuwa amedhamiria kuboresha zaidi maslahi ya watumishi wa umma. Tuendelee kumuunga mkono na kupiga kazi kwa bidii kulijenga Taifa letu.
 
Niko na mwalimu eusebio hapa anasema sawa mama "nimekuelewa naenda kununua lita 3:za mafuta" msalimie IGP na mamilioni ya mahela ya kupandishwa cheo : mlw eusebio!!
 
Jf imevamiwa jaman
 
Utapata shida ya bure, vijana wengi siku hizi uwezo wao wa kuelewa mwenendo wa serikali ni mdogo sana, hawawezi kutumia akili kuelewa miongozo wao wanakwenda wazimawazima.
 
Nakuja kumhamisha mwanangu kwenye hiyo shule unayofundisha! Kwa ku argue huku, lazima somo lako unafelisha tu NB (kwa akili hizi ccm itatawala milele)
 
Konyoooooo sana wewe
 
Mara nyingi waliopata division 3 na 4 ndo hukimbilia kuwa Walimu. Naona tatizo lilipo sasa.
 
 
Certified imbecile
 
Hili taifa bhana unaweza kukuta huyu Ni kipenyo ....
 
Ahsante msemaji wa wizara ya fedha, uliyejitunuku welewa kupita wenzako... Umesahau kuandika namba ya simu ili utakapoitwa kule mjengo mweupe iwe rahisi... Endelea kupita mtandaoni Kuna mengi yanahitaji ufafanuzi wako....!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…