Mwamuzi wa Tanzania
JF-Expert Member
- Apr 7, 2020
- 15,486
- 45,256
Habari!
Hii mada nimeileta kutokana na uzi aliouandika bwana mmoja hapa jf akilalamika jinsi simu za ndugu na marafiki zinavyomiminika kuomba msaada pindi tu anapopata fedha.
Kuna watu mpaka kanisani wanashuhudia jinsi Mungu alivyowavusha walipopata tatizo, wakisema kuwa tatizo lilipokuja ashukuriwe Mungu tayari alikuwa ameshalipwa aidha mshahara, mafao yake ya kustaafu n.k.
Nikiwa katika huduma za kiroho nimekutana na case nyingi tu watu wakilalamika kuwa wakipata kiasi fulani tu tatizo huja na huanza upya. Yaani watu wamewekewa kikomo cha umiliki wa pesa.
Kwa hakika Mungu hawezi kuruhusu upoteze fedha kirahisi hivyo.
Iko hivi, watu wanaopata pesa kichawi wanawawekea watu kitu kama chip, yaani vipepo vya kichawi vinakusanya fedha kiasi fulani na kukubakishia kiasi fulani bila wewe kushtuka.
Sasa ili usishtuke unapewa vijitatizo vya hapa na pale ili uone pesa yako imeenda sawia tu kumbe watu wameshachota.
Ukifungwa na roho hizi za kichawi utajikuta unashindwa kumiliki hata kiwanja wakati wewe ni meneja wa taasisi huku unaowaongoza wanalipwa chini yako wanafanya maendeleo.
Kuna mbaba namfahamu anafanya kazi ulaya sasa yeye alikuwa kila mwezi anawatumia pesa karibu ndugu zake wote. Alipofunguliwa kwa maombi akawa huru sasa anafanya maendeleo.
Pesa tuwasaidie watu ila tuwe makini, muda mwingine unajua unamtumia mtu pesa kumbe jini ndilo unalitumia. Bila haya mtu huyohuyo two weeks later anaomba pesa unaanza kushangaa si nilitumia majuzi.