Fahamu maajabu ya Vinasaba vinne vya msingi

Fahamu maajabu ya Vinasaba vinne vya msingi

Ni kawaida sana kusikia mama akisifiwa kwa kuzaa photocopy ya mume wake, bila kujua kwamba ile process ya ‘photocopying’ haikufanyika tumboni kwa mama, bali ilianza kwenye ‘Gonads /(Korodani)’ za baba mtu na kwenda kukamilika tumboni kwa mama.

Kidijitali taarifa za kielektroniki zinatunzwa na kusafirishwa katika ‘Digits’, yaani tarakimu ‘1’ na tarakimu ‘0’, na hizi ndio taarifa za chini kabisa za msingi za kidijitali. Muunganiko wa hizo tarakimu (bits) zikawa 8, ndio tunaita ‘byte’; mfano [10110001] ni ‘byte’ moja (1B) ya taarifa. Muunganiko wa hizi ‘bytes’ zikawa elfu moja , ndio tunaita ‘Kilobyte’ moja (1Kb). Muunganika wa hizo ‘Kilobyte’ zikawa elfu moja, ndio tunaita ‘Megabyte’ moja ya ‘data’/(taarifa) yaani (1Mb).

Kwahiyo ukiambiwa umepata 100Mb maana yake ndio hiyo. Hizi data zinatafsirika na kusafirishika vipi? Mfano ukitumia whatsapp kutuma neno ‘Mama’, hilo neno lina herufi 4, katika lugha za kidijitali (mfano Android platform) kuna makubaliano au standard (lugha ni makubaliano yaletayo maelewano) ; mfano; kwamba herufi ‘m’ iwakilishwe na byte 3 zenye mpangilio fulani wa zile bits (1’s and 0’s), (Switch on/Switch off) na hivyo yule mpokeaji wa meseji simu yake inatafsiri huo mpangilio wa ‘bits’ katika kila ‘byte’ na kupata jibu kwamba mtumaji anamaanisha herufi ‘m’, na herufi ‘m’ hutokea kwenye screen, halikadhalika kwa herufi zote la neno mama. Hadi hapa naweza kusema kwamba mtumaji wa meseji yenye neno ‘mama’ ndio baba ambae amezituma mbegu zake kwenda tumboni kwa mama, na yule mama ndio mpokeaji wa meseji na akaitafsiri kuleta matokea tarajiwa. Nimetolea hii computer analogy ili niweze kueleweka kwenye hatu inayofuata ya vinasaba vya msingi.

Vinasaba vya msingi kwa viumbe vyote hai duniani ni vinne (analogous to digits/bits); ambavyo ni ADENINE, THYMINE, GUANINE, CYTOCINE. Na huu ndio msingi haswa wa kipimo cha DNA. (Deoxyrybonucleic acid) testing.

*Na reserve comment ya kwanza ili niweze kufafanua jinsi hivyo vinasaba vinavyofanya maajabu yenyewe sasa.Kuanzia kwenye ‘Meiosis’ kabisa.., pia tutajaribu kufanya mjadala katika msingi wa kudodosa kuona inawezekana vipi mtoto anafanana hadi kutembea na baba yake?

View attachment 1684441
Umejitahidi sana kufafanua kuhusu binary. Hongera sana
 
 
Kwa hiyo unawashauri binadamu wachaguane wazuri ili wazae watoto wazuri...
Mtoto anaweza kurithi vinasaba vya babu, bibi, mjomba , Shangazi nk. , ndio maana unakuta jitu liko hovyo ila watoto ni wazuri balaa...,

 
 
 
Mkuu kwanza hongera kwa huo ujuzi ulionao maana ni wachache sana hufahamu mambo hayo. Mimi naomba kufahamu kuhusu ugonjwa wa ukoma(leprosy) kwani nimekua nikibashana na watu sana kuhusu huu ugonjwa. Huu ugonjwa ni ugonjwa wa kurithi (genetic inherited) ama ni familial disease?
 
Wengine hufanana na bibi zao au babu zao, tutadodosa hili pia, hasa hasa tukijikita kwenye ‘Recessive’ na ‘Dorminant’ genetic traits tukizingatia matokeo yake katika ‘Homogenous’ na ‘Heterogenous’ combinations...
Unakopi kutokea mtandao gani?
 
Mkuu kwanza hongera kwa huo ujuzi ulionao maana ni wachache sana hufahamu mambo hayo. Mimi naomba kufahamu kuhusu ugonjwa wa ukoma(leprosy) kwani nimekua nikibashana na watu sana kuhusu huu ugonjwa. Huu ugonjwa ni ugonjwa wa kurithi (genetic inherited) ama ni familial disease?
Kwa haraka haraka, Ugonjwa unaoambukizwa baada ya mtu kuwa keshazaliwa huwa sio wa kurithi
 
Back
Top Bottom