Fahamu madhara ya kunywa pombe bila kula

Fahamu madhara ya kunywa pombe bila kula

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Kama wewe ni mnywaji wa pombe zinazotengenezwa kwa ngano au pombe kali inakuhusu hii.

Wataalamu wa afya wameeleza uwepo wa athari hasi, kwa wale wenye tabia za kunywa pombe kabla ya kula chakula kwani huchangia mnywaji kula chakula kidogo kuliko mahitaji ya mwili au kuharibu kuta za utumbo.

Mtaalamu wa Lishe na Meneja Mradi wa Afya ya Mama na Mtoto kutoka Shirika la World Vision, Dk Daudi Gambo amesema athari inategemea ni pombe ipi amekunywa, kwani kuna tofauti kati ya pombe kali na zile zilizotengenezwa kwa ngano.

“Pombe zenye ngano kama bia aina zote, yule mtu anakuwa amechukua kaloris nyingi kutoka kwenye kabohaidreti, kwa maana hiyo anaweza kujikuta ameshiba na ile hamu ya kula chakula ikapungua kwa sababu nguvu tayari anazo, hivyo atapunguza nafasi ya yeye kula kitu kingine,” anasema.

Dk Gambo anasema mnywaji atakuwa amechukua kaloris, hivyo vitamin, protini, madini vyote hivyo amevikosa na wengi akishiba anaweza asile, hivyo hajapata virutubisho vyote vinavyopatikana kwenye makundi sita ya vyakula.

Anasema anayekunywa bia anakuwa amechukua sehemu moja na ameacha virutubisho kutoka makundi mengine na akishakunywa hamu ya chakula inapungua au inaisha kabisa.

Akizungumzia pombe kali, Dk Gambo anasema zinaathiri vimeng’enya chakula ‘enzymes’ na ikiathiri utengenezaji wa vimeng’enya chakula inaua wale wadudu waliopo kwenye utumbo.
 
Wamefanya tafiti au na wao wame google kama sisi, kiufupi sioni jipya hapo
 
Kwakifupi wanashauri ule chakula kwanza chenye virutubisho vyote ndio upige mtungi, kidogo wameshauri kitu cha maana
Binafsi siwezi kunywa kwanza kabla sijala hilo haliwezekani kabisa 😊🤒😎
 
kuna utata hapa! sasa kama bia inaongeza nguvu kama vile amekula chakula cha carbohydrates,sasa mbona tukinywa tunaanguka au nguvu hupungua miguuni nakuhamia mdomoni..?
 
Beer inakuwaga tamu sana kama hujala.
Beer mbili tu unakaa sawa, halafu ndipo unaanza ku deal na soup au nyama choma.
 
Back
Top Bottom