Fahamu madhara ya kunywa pombe bila kula

Fahamu madhara ya kunywa pombe bila kula

Nimekusamehe, ntachukulia kama sijawahi soma hii thread yako, usirudie tena.
 
😀😀 Alaa kumbe ndo tatizo linapoanzia
kuna vidada vinavaaga viatu vya manyoya na dera halafu mkononi kashika simu yenye kava la mdori,mgongoni kabeba kibegi kiduchu kama kinataka kudondoka hivi!.. cheza mbali ndugu
 
Kama wewe ni mnywaji wa pombe zinazotengenezwa kwa ngano au pombe kali inakuhusu hii.

Wataalamu wa afya wameeleza uwepo wa athari hasi, kwa wale wenye tabia za kunywa pombe kabla ya kula chakula kwani huchangia mnywaji kula chakula kidogo kuliko mahitaji ya mwili au kuharibu kuta za utumbo.

Mtaalamu wa Lishe na Meneja Mradi wa Afya ya Mama na Mtoto kutoka Shirika la World Vision, Dk Daudi Gambo amesema athari inategemea ni pombe ipi amekunywa, kwani kuna tofauti kati ya pombe kali na zile zilizotengenezwa kwa ngano.

“Pombe zenye ngano kama bia aina zote, yule mtu anakuwa amechukua kaloris nyingi kutoka kwenye kabohaidreti, kwa maana hiyo anaweza kujikuta ameshiba na ile hamu ya kula chakula ikapungua kwa sababu nguvu tayari anazo, hivyo atapunguza nafasi ya yeye kula kitu kingine,” anasema.

Dk Gambo anasema mnywaji atakuwa amechukua kaloris, hivyo vitamin, protini, madini vyote hivyo amevikosa na wengi akishiba anaweza asile, hivyo hajapata virutubisho vyote vinavyopatikana kwenye makundi sita ya vyakula.

Anasema anayekunywa bia anakuwa amechukua sehemu moja na ameacha virutubisho kutoka makundi mengine na akishakunywa hamu ya chakula inapungua au inaisha kabisa.

Akizungumzia pombe kali, Dk Gambo anasema zinaathiri vimeng’enya chakula ‘enzymes’ na ikiathiri utengenezaji wa vimeng’enya chakula inaua wale wadudu waliopo kwenye utumbo.
Hayabanaa
 

Attachments

  • Screenshot_20240517-065902_Gallery.jpg
    Screenshot_20240517-065902_Gallery.jpg
    210.9 KB · Views: 3
Back
Top Bottom