Teko Modise
JF-Expert Member
- May 20, 2017
- 2,331
- 7,733
Leo nimeona niwaletee machache kuhusu Jenerali Robert Mboma, aliyepata kuwa Mkuu wa Majeshi wa Tanzania miaka ya nyuma huku akiwa na rekodi mbalimbali. Twende kazi…
1. Jenerali Robert Mboma alijiunga na Jeshi la Wananchi na kulitumikia katika nafasi mbalimbali mpaka pale alipostafu mwaka 2001 kwa utumishi uliotukuka.
2. Ni miongoni mwa vijana wasomi wa mwanzoni kabisa baada ya kuanzishwa kwa JWTZ mwaka 1964. Kumbuka miaka hiyo wasomi walikuwa wachache sana.
3. Jenerali Mboma ni miongoni mwa Marubani mahiri kuwahi kutokea katika historia ya JWTZ kitaalam alikuwa mbobezi haswa wa Ndege Vita. Ukienda Ngerengere jina lake linatajwa sana na hutumika sana kama mfano kwa Marubani wapya wa JWTZ.
4. Ni wakati wa Vita ya Kagera, Jenerali Mboma alijijengea jina kubwa sana kwa uhodari na umahiri wake wa kurusha Ndege Vita. Yeye na wenzake walileta taharuki kubwa sana kwa Waganda pamoja na Vikosi vya Nduli Idd Amin kuanzia Mbarara, Jinja, Masaka, Entebbe mpaka Kampala. Waganda walikuwa wanaogopa sana Ndege Vita za Tanzania kutokana na namna walivyokuwa wanafanya mashambulizi hasa yale ya kushtukiza huku wakishindwa kuwanasa.
5. Wakati wa Vita ya Kagera, kwa kushirikiana na Idara ya Intelijensia Jeshini, alihusika katika Utekaji wa Ndege ya Kivita iliyokuwa imebeba Silaha kutoka Libya kwa Gaddafi kwenda kwa Idd Amin. Ndege hiyo ilitekwa na kubadilishwa uelekeo badala ya kutua Entebee ikaenda kutua Mwanza/KIA. Hii ilikuwa ni kete muhimu sana kwa JWTZ katika vita hiyo.
6. Baada ya Vita kuisha na Tanzania kushinda, Wanajeshi wetu walipokelewa uwanja wa Uhuru na siku hiyo Jenerali Mboma alipoteza rafiki yake ambaye alikuwa ni rubani mwenzake. Ndege Vita ya JWTZ ilipoteza mwelekeo wakati wa sherehe pale Uwanja wa Uhuru, rubani akaenda kuidondosha pembeni mwa uwanja huo ili asije akaua wananchi. Rubani wa ndege ile alifariki palepale na mnara wa tukio hilo upo karibu na uwanja wa mpira wa Benjamin Mkapa upande wa Mgulani JKT.
7. Baada ya Vita, Rais Nyerere aliamua kuanzisha Kamandi ya Anga ndani ya JWTZ. Robert Mboma akiwa Brigedia Jenerali kwa wakati huo akawa ni Mkuu wa Kwanza wa Kamandi ya Wana anga ya JWTZ katika historia. Aliteuliwa kushika mdaraka hayo mwaka 1982.
Baadhi ya wanajeshi wa Kamandi ya wanaanga kama Vile Komando Tamimu walishiriki katika Jaribio la Mapinduzi la mwaka 1982 lakini chini ya Uongozi wa Mboma na idara ya Usalama wa Taifa na Kamandi nyingine za JWTZ walifanikiwa kuzima Jaribio hilo.
8. Kutokana na uweledi wake wa kutukuka, aliiongoza Kamandi hiyo kuanzia February 1982 mpaka March 1994 alipopanda cheo na kuwa CDF. Alikuwa Mkuu wa Kamandi ya Anga kwa Miaka 12 rekodi ambayo inasimama mpaka leo na mpaka sasa hakuna aliyevunja rekodi hiyo!
9. March 28 mwaka 1994, Rais wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi alimteua Meja Jenerali Mboma kuwa Mkuu wa Majeshi akichukua nafasi ya Jenerali Mwita Kiaro aliyekuwa amestafu.
10. Jenerali Robert Mboma ni Mkuu wa Majeshi wa tano katika historia ya Jeshi la Wananchi Tanzania. Akishika wadhifa huo kuanzia March 1994 mpaka alipostafu utumishi wake Jeshini mwaka 2001 chini ya Rais Benjamin Mkapa. Hivyo kufanya Mboma kuwa CDF wa pili kutumikia Marais wawili tofauti. Jenerali Mboma anabakia CDF pekee wa JWTZ kutokea kamandi ya Anga.
Bonus:
Baada ya kustaafu utumishi wake Jeshini, aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini kama vile Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini chini ya Rais Kikwete.
Vilevile aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Shirika la Umeme nchini Tanesco mwaka 2012.