Fahamu Mambo 10 kuhusu Jenerali Robert Mboma, CDF pekee kutokea Kamandi ya Anga

🙏🏾🙏🏾
 
Ile kashfa yao na akina Iddi Simba mbona umeamua kuiacha? Na wasifu wa kuwa mwanaCCM kiasi cha kutaka kugombea ubunge kwenye kura za maoni huko Mbeya vijijini mbona hujaandika?
 
Baadhi ya wanajeshi wa Kamandi ya wanaanga kama Vile Komando Tamimu walishiriki katika Jaribio la Mapinduzi la mwaka 1982 lakini chini ya Uongozi wa Mboma na idara ya Usalama wa Taifa na Kamandi nyingine za JWTZ walifanikiwa kuzima Jaribio hilo.
Hivi ni Mboma au Augustine Mahiga ndie aliewezesha kumalizwa kwa Komandoo 'Mohamed Tamimu' aliekwiva kwa mafunzo ya kijeshi kutoka Cuba?
 
Hahaha hapa imebidi nicheke kidogo uongo ukinigeshwa sana
 
Mie siamini hii story..
Maana wabongo kwa kujipakulia minyama hatujambo.

Unataka kutuaminisha aliruka na fighter akawa anakimbiza ndege za adui akaipiga ya kwanza halafu akaipiga nyingine, hapo hapo akaingia UG akapiga benki, akapiga na radar...

Sidhani kama ni rahisi hivyo..
 
Hakuna la maana
Hapo USA kuna vitoto vidogo tu vimepiganisha vita Iraq, Afghanistan na kwingineko na havina mbwembwe
 
Uongo ukichangamka ndio yanakua yaleyale ya Mayunga na Milinga simulizi za uongo uongo mara kageuka Kobe Oya Tusepe
 
Uongo ukichangamka ndio yanakua yaleyale ya Mayunga na Milinga simulizi za uongo uongo mara kageuka Kobe Oya Tusepe
Atuelezee jeshi la anga la UG walikuwa wanatumia ndege za aina gani, halafu ilikuwaje ndege vita ya UG ikapige kisiwa kisicho na impact yeyote kwa jeshi.

Hizo ndege kipindi zinaingia Mwanza, hio Mig ya Tanzania ilikuwa ikipiga doria? Au iliruka kutokea airport...?

Ina maana jeshi la UG waliacha targets zoote wakaenda kupiga kisiwa kina mijusi na kenge?

Hata airport ya Mwanza hawakuiona?

Hii ni chai.
 
Mkuu asante kwa historia iliyotukuka ya huyo Mjeshi.
 
Umezaliwa mwaka 2000 ni hiari yako kuamini au kukataa.

Muulize baba yako mzazi akuambie kazi ya Gen Robert Mboma ilikuwa vipi.

Sisi wote tulikuwa tuna ndege za aina moja (MIG 21). Kwa hiyo baada ya zile ndege 2 kushambulia kisiwa cha Saanane, ndipo Mboma akaipiga moja. Wakati ile iliyobaki inarudi yule pilot alijuwa ni mwezie, hakujuwa kuwa ni ndege ya Tz. Hata kwenye radar walijuwa ni ndege yako mpaka pale iliposhambuliwa.

Kasome The Art of War- by Sun Tzu, waeweza kunielewa
 
Hii story haina muunganiko, just a cheap propaganda na uongo mwingi.

Ni kama story kutoka kwenye filamu, haya ndio yale mliambiwa Amin anakula watu mkatengenezewa na filamu za uongo na kweli.

Huwezi shambulia ndege vita ikaanguka halafu eti rubani akajua wewe adui ni mwenzake ukamfuata nyuma na kumshambulia, unataka kutuaminisha hio mig ya UG haikuwa na uwezo kufanya mawasiliano na hio ya Tz?

Mig21 ni interceptor, hapo hapo unatuambia ikaenda UG ikapiga ground targets...

Interceptors sio ndege nzuri kupiga targets za ardhini na si rahisi kama unavyosema hapa, mig21 ni nzuri kupiga ndege za adui kama bomber, reconnaissance aircraft n.k...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…