Mwalimu wa tuisheni
JF-Expert Member
- Oct 19, 2019
- 6,602
- 10,801
Wanacheza magemu ya gta 🤣 😂Mie siamini hii story..
Maana wabongo kwa kujipakulia minyama hatujambo.
Unataka kutuaminisha aliruka na fighter akawa anakimbiza ndege za adui akaipiga ya kwanza halafu akaipiga nyingine, hapo hapo akaingia UG akapiga benki, akapiga na radar...
Sidhani kama ni rahisi hivyo..
Ukipita forums za hao mapilot wa hizo mig21 wanasema ni ndege ngumu kuzi operate na ilihitaji uwezo haswa.Wanacheza magemu ya gta 🤣 😂
Wewe kinda sana endelea kubisha. Hiyo siyo cinema ambayo matukio yanapangwa na kuwa rehersed bali ni spontaneous activity at speed of light.Hii story haina muunganiko, just a cheap propaganda na uongo mwingi.
Ni kama story kutoka kwenye filamu, haya ndio yale mliambiwa Amin anakula watu mkatengenezewa na filamu za uongo na kweli.
Huwezi shambulia ndege vita ikaanguka halafu eti rubani akajua wewe adui ni mwenzake ukamfuata nyuma na kumshambulia, unataka kutuaminisha hio mig ya UG haikuwa na uwezo kufanya mawasiliano na hio ya Tz?
Mig21 ni interceptor, hapo hapo unatuambia ikaenda UG ikapiga ground targets...
Interceptors sio ndege nzuri kupiga targets za ardhini na si rahisi kama unavyosema hapa, mig21 ni nzuri kupiga ndege za adui kama bomber, reconnaissance aircraft n.k...
Soma hapa nimekuletea material halafu urudiUkipita forums za hao mapilot wa hizo mig21 wanasema ni ndege ngumu kuzi operate na ilihitaji uwezo haswa.
Wanasema zilkuwa ni ndege hatari hata kwa usalama wao... Lakini huyu jamaa hapa anakusimulia Gen Mboma aliruka akapiga ndege ya UG , akapiga maneuver chap akakaa nyuma ya ndege ya adui akawa anamfuata nyuma akamshambulia na yeye, akaingia UG akapiga bank ya Libya baadae akapiga kona akashambulia radar....
Duh!!! Hii chai hainyweki.. sio rahisi kufanya yote hayo kwa ndege kama mig21 za 1950s...
Sisi hata ile vita kilichotusaidia makundi ya watu wa UG ambao hawakumtaka Amin, na jeshi la Obote, tulikuwa hoi tu... Hata UG ilikuwa vizuri kijeshi kutuzidi.
Hata mi nimeona uongo ongo no mwingi.Uongo ni mwingi sana,
No mwaka flan sio mbali nikiwa sehem nlkuta wanazo zngne kutoka chna vna rangi ya pinki resemble na mig...nazan by now total fleet kuazia 100...( Minimum estimation)...Chache sana ni za kichina halafu old model na zina umri mrefu.
Idadi yake zikiwa nyingi sana ni 15..
Tumuulize tuu kama JWTZ ni mgambo je, jeshi la wananchi la nchi yake linaitwaje!?Wanaohakikisha usalama wako huko vichakani unakoishi! Mkishavuta mibange yenu mnandika chochote!
Sema nini mkuu tukiishi kwa kujilangansha hivo itafika mahali tutaacha kuona thamani hata ya juhud za wazazi wetu katika maisha yetu.Hakuna la maana
Hapo USA kuna vitoto vidogo tu vimepiganisha vita Iraq, Afghanistan na kwingineko na havina mbwembwe
hizi sasa ndio habari zake nzuri nilikuwa nazijuaNina wasiwasi na namba 5. Ila kuna haya mawili hujayataja:
1. Yeye ndiye aliyezishambulia ndege za Uganda aina ya MIG 21 zilipokuja Mwanza na kudondosha mabomu Kisiwa cha Saanane Mwanza ndani ya Ziwa Victoria. Ya kwanza aliipiga akiwa angani na kisha akaendelea sambamba kwenda Entebbe akifuatana na ile nyingine
2. Aiipiga ndege nyingine ya pili uwanja wa Entebbe baada ya kutua kwa pamoja
3. Alishambulia radar ya Entebbe Airport hivyo kuwapunguzia uwezo wa jeshi la anga
4. Kisha akapiga benki ya Libya iliyokuwako Kampala kabla ya kurudi Mwanza Airport
Kinda anakuzidi maarifa sana.Hizo sifa unazombambikia Gen hazina muunganiko mzuri unaoeleweka na kushawishi.Wewe kinda sana endelea kubisha. Hiyo siyo cinema ambayo matukio yanapangwa na kuwa rehersed bali ni spontaneous activity at speed of light.
Gen Robert Mboma mwenyewe yupo Mbezi Beach nenda kumhoji
Hii Historia Imenikumbudha Mambo Mengi ya Utotoni Mboma Alikuwa jirani yetu hapo Isamilo mimi nikiwa mtoto Mdogo nikiwa naishi Isamilo nakumbuka nilikuwa naenda kuvhexa kea mboma nakumbuka Alikuwa na Watoto Mkubwa Alikuwa Anaitwa Sophia Mboma na Wa Pili Issa Mboma popote Mlipo nawakumbuka tulicheza wote.Leo nimeona niwaletee machache kuhusu Jenerali Robert Mboma, aliyepata kuwa Mkuu wa Majeshi wa Tanzania miaka ya nyuma huku akiwa na rekodi mbalimbali. Twende kazi…
1. Jenerali Robert Mboma alijiunga na Jeshi la Wananchi na kulitumikia katika nafasi mbalimbali mpaka pale alipostafu mwaka 2001 kwa utumishi uliotukuka.
2. Ni miongoni mwa vijana wasomi wa mwanzoni kabisa baada ya kuanzishwa kwa JWTZ mwaka 1964. Kumbuka miaka hiyo wasomi walikuwa wachache sana.
3. Jenerali Mboma ni miongoni mwa Marubani mahiri kuwahi kutokea katika historia ya JWTZ kitaalam alikuwa mbobezi haswa wa Ndege Vita. Ukienda Ngerengere jina lake linatajwa sana na hutumika sana kama mfano kwa Marubani wapya wa JWTZ.
4. Ni wakati wa Vita ya Kagera, Jenerali Mboma alijijengea jina kubwa sana kwa uhodari na umahiri wake wa kurusha Ndege Vita. Yeye na wenzake walileta taharuki kubwa sana kwa Waganda pamoja na Vikosi vya Nduli Idd Amin kuanzia Mbarara, Jinja, Masaka, Entebbe mpaka Kampala. Waganda walikuwa wanaogopa sana Ndege Vita za Tanzania kutokana na namna walivyokuwa wanafanya mashambulizi hasa yale ya kushtukiza huku wakishindwa kuwanasa.
5. Wakati wa Vita ya Kagera, kwa kushirikiana na Idara ya Intelijensia Jeshini, alihusika katika Utekaji wa Ndege ya Kivita iliyokuwa imebeba Silaha kutoka Libya kwa Gaddafi kwenda kwa Idd Amin. Ndege hiyo ilitekwa na kubadilishwa uelekeo badala ya kutua Entebee ikaenda kutua Mwanza/KIA. Hii ilikuwa ni kete muhimu sana kwa JWTZ katika vita hiyo.
6. Baada ya Vita kuisha na Tanzania kushinda, Wanajeshi wetu walipokelewa uwanja wa Uhuru na siku hiyo Jenerali Mboma alipoteza rafiki yake ambaye alikuwa ni rubani mwenzake. Ndege Vita ya JWTZ ilipoteza mwelekeo wakati wa sherehe pale Uwanja wa Uhuru, rubani akaenda kuidondosha pembeni mwa uwanja huo ili asije akaua wananchi. Rubani wa ndege ile alifariki palepale na mnara wa tukio hilo upo karibu na uwanja wa mpira wa Benjamin Mkapa upande wa Mgulani JKT.
7. Baada ya Vita, Rais Nyerere aliamua kuanzisha Kamandi ya Anga ndani ya JWTZ. Robert Mboma akiwa Brigedia Jenerali kwa wakati huo akawa ni Mkuu wa Kwanza wa Kamandi ya Wana anga ya JWTZ katika historia. Aliteuliwa kushika mdaraka hayo mwaka 1982.
Baadhi ya wanajeshi wa Kamandi ya wanaanga kama Vile Komando Tamimu walishiriki katika Jaribio la Mapinduzi la mwaka 1982 lakini chini ya Uongozi wa Mboma na idara ya Usalama wa Taifa na Kamandi nyingine za JWTZ walifanikiwa kuzima Jaribio hilo.
8. Kutokana na uweledi wake wa kutukuka, aliiongoza Kamandi hiyo kuanzia February 1982 mpaka March 1994 alipopanda cheo na kuwa CDF. Alikuwa Mkuu wa Kamandi ya Anga kwa Miaka 12 rekodi ambayo inasimama mpaka leo na mpaka sasa hakuna aliyevunja rekodi hiyo!
9. March 28 mwaka 1994, Rais wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi alimteua Meja Jenerali Mboma kuwa Mkuu wa Majeshi akichukua nafasi ya Jenerali Mwita Kiaro aliyekuwa amestafu.
10. Jenerali Robert Mboma ni Mkuu wa Majeshi wa tano katika historia ya Jeshi la Wananchi Tanzania. Akishika wadhifa huo kuanzia March 1994 mpaka alipostafu utumishi wake Jeshini mwaka 2001 chini ya Rais Benjamin Mkapa. Hivyo kufanya Mboma kuwa CDF wa pili kutumikia Marais wawili tofauti. Jenerali Mboma anabakia CDF pekee wa JWTZ kutokea kamandi ya Anga.
Bonus:
Baada ya kustaafu utumishi wake Jeshini, aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini kama vile Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini chini ya Rais Kikwete.
Vilevile aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Shirika la Umeme nchini Tanesco mwaka 2012.
View attachment 3143488
Mkikaa na huyo mmalila mwambie kwao alipotoka katika kata ya santilya ,kijiji cha santilya hakuna maji wala umeme na ni sehemu vijana wanakataa shule mbaya zaidi kwa takwimu za mwaka jana ni kijiji cha pili kwa upande wa mkoa wa mbeya kuwa na maamumbukizi ya virusi vya UKIMWI .Leo nimeona niwaletee machache kuhusu Jenerali Robert Mboma, aliyepata kuwa Mkuu wa Majeshi wa Tanzania miaka ya nyuma huku akiwa na rekodi mbalimbali. Twende kazi…
1. Jenerali Robert Mboma alijiunga na Jeshi la Wananchi na kulitumikia katika nafasi mbalimbali mpaka pale alipostafu mwaka 2001 kwa utumishi uliotukuka.
2. Ni miongoni mwa vijana wasomi wa mwanzoni kabisa baada ya kuanzishwa kwa JWTZ mwaka 1964. Kumbuka miaka hiyo wasomi walikuwa wachache sana.
3. Jenerali Mboma ni miongoni mwa Marubani mahiri kuwahi kutokea katika historia ya JWTZ kitaalam alikuwa mbobezi haswa wa Ndege Vita. Ukienda Ngerengere jina lake linatajwa sana na hutumika sana kama mfano kwa Marubani wapya wa JWTZ.
4. Ni wakati wa Vita ya Kagera, Jenerali Mboma alijijengea jina kubwa sana kwa uhodari na umahiri wake wa kurusha Ndege Vita. Yeye na wenzake walileta taharuki kubwa sana kwa Waganda pamoja na Vikosi vya Nduli Idd Amin kuanzia Mbarara, Jinja, Masaka, Entebbe mpaka Kampala. Waganda walikuwa wanaogopa sana Ndege Vita za Tanzania kutokana na namna walivyokuwa wanafanya mashambulizi hasa yale ya kushtukiza huku wakishindwa kuwanasa.
5. Wakati wa Vita ya Kagera, kwa kushirikiana na Idara ya Intelijensia Jeshini, alihusika katika Utekaji wa Ndege ya Kivita iliyokuwa imebeba Silaha kutoka Libya kwa Gaddafi kwenda kwa Idd Amin. Ndege hiyo ilitekwa na kubadilishwa uelekeo badala ya kutua Entebee ikaenda kutua Mwanza/KIA. Hii ilikuwa ni kete muhimu sana kwa JWTZ katika vita hiyo.
6. Baada ya Vita kuisha na Tanzania kushinda, Wanajeshi wetu walipokelewa uwanja wa Uhuru na siku hiyo Jenerali Mboma alipoteza rafiki yake ambaye alikuwa ni rubani mwenzake. Ndege Vita ya JWTZ ilipoteza mwelekeo wakati wa sherehe pale Uwanja wa Uhuru, rubani akaenda kuidondosha pembeni mwa uwanja huo ili asije akaua wananchi. Rubani wa ndege ile alifariki palepale na mnara wa tukio hilo upo karibu na uwanja wa mpira wa Benjamin Mkapa upande wa Mgulani JKT.
7. Baada ya Vita, Rais Nyerere aliamua kuanzisha Kamandi ya Anga ndani ya JWTZ. Robert Mboma akiwa Brigedia Jenerali kwa wakati huo akawa ni Mkuu wa Kwanza wa Kamandi ya Wana anga ya JWTZ katika historia. Aliteuliwa kushika mdaraka hayo mwaka 1982.
Baadhi ya wanajeshi wa Kamandi ya wanaanga kama Vile Komando Tamimu walishiriki katika Jaribio la Mapinduzi la mwaka 1982 lakini chini ya Uongozi wa Mboma na idara ya Usalama wa Taifa na Kamandi nyingine za JWTZ walifanikiwa kuzima Jaribio hilo.
8. Kutokana na uweledi wake wa kutukuka, aliiongoza Kamandi hiyo kuanzia February 1982 mpaka March 1994 alipopanda cheo na kuwa CDF. Alikuwa Mkuu wa Kamandi ya Anga kwa Miaka 12 rekodi ambayo inasimama mpaka leo na mpaka sasa hakuna aliyevunja rekodi hiyo!
9. March 28 mwaka 1994, Rais wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi alimteua Meja Jenerali Mboma kuwa Mkuu wa Majeshi akichukua nafasi ya Jenerali Mwita Kiaro aliyekuwa amestafu.
10. Jenerali Robert Mboma ni Mkuu wa Majeshi wa tano katika historia ya Jeshi la Wananchi Tanzania. Akishika wadhifa huo kuanzia March 1994 mpaka alipostafu utumishi wake Jeshini mwaka 2001 chini ya Rais Benjamin Mkapa. Hivyo kufanya Mboma kuwa CDF wa pili kutumikia Marais wawili tofauti. Jenerali Mboma anabakia CDF pekee wa JWTZ kutokea kamandi ya Anga.
Bonus:
Baada ya kustaafu utumishi wake Jeshini, aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini kama vile Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini chini ya Rais Kikwete.
Vilevile aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Shirika la Umeme nchini Tanesco mwaka 2012.
View attachment 3143488
Nina wasiwasi na namba 5. Ila kuna haya mawili hujayataja:
1. Yeye ndiye aliyezishambulia ndege za Uganda aina ya MIG 21 zilipokuja Mwanza na kudondosha mabomu Kisiwa cha Saanane Mwanza ndani ya Ziwa Victoria. Ya kwanza aliipiga akiwa angani na kisha akaendelea sambamba kwenda Entebbe akifuatana na ile nyingine
2. Aiipiga ndege nyingine ya pili uwanja wa Entebbe baada ya kutua kwa pamoja
3. Alishambulia radar ya Entebbe Airport hivyo kuwapunguzia uwezo wa jeshi la anga
4. Kisha akapiga benki ya Libya iliyokuwako Kampala kabla ya kurudi Mwanza Airporte
Dadeki walah ilkua mashineNina wasiwasi na namba 5. Ila kuna haya mawili hujayataja:
1. Yeye ndiye aliyezishambulia ndege za Uganda aina ya MIG 21 zilipokuja Mwanza na kudondosha mabomu Kisiwa cha Saanane Mwanza ndani ya Ziwa Victoria. Ya kwanza aliipiga akiwa angani na kisha akaendelea sambamba kwenda Entebbe akifuatana na ile nyingine
2. Aiipiga ndege nyingine ya pili uwanja wa Entebbe baada ya kutua kwa pamoja
3. Alishambulia radar ya Entebbe Airport hivyo kuwapunguzia uwezo wa jeshi la anga
4. Kisha akapiga benki ya Libya iliyokuwako Kampala kabla ya kurudi Mwanza Airport
Wanajeshi wanakuaga humble sana. Shida kwa ndugu zetu polisi.Niliwahi kuhudhuria hafla fulani nyumbani kwa Mboma miaka ya themnini huko Oysterbay akiwa Brigadier ila wakati huo sikujua kama ni Brigadier ila nilipofika ndipo nikakutana na walinzi wanajeshi. Sasa wakati hafla inaanza rasmini akatutambulisha marafiki zake wakiwa ni makanali na maluteni kanali kadhaa pamoja na meja mmoja. Nilpokunywa bia kadhaa za bure nikapata ushujaa kumwuliza kuwa vipi mbona anajuana na maafisa wa juu wa jeshi na mji wake pia unalindwa na wanajeshi, kulikoni. Akanijibu kwa uungana tu kuwa hao wote ni wafanyakzi wenzake Jeshini na yeye mwenyewe pia ni mwanajeshi nakamanda wao. Nikatosheka na jibu kabisa.