Fahamu mambo mbalimbali kuhusu Kilimo cha Korosho

HABARI,
"mnyikungu,
Sawa hongera sana Tena kwa Iringa mna fulsa nyingine ambayo maeneo mengi hakuna fulsa ya kilimo cha parachichi kwenye wilaya ya kilolo na mkoa wa Njombe nakutakia kila jema Comrade.

LUMUMBA
Nashukuru mkuu, hiyo plan ya palachichi nataka nianze mwaka huu nina eneo wilaya ya mufindi nimeambiwa inafaa. Kwahiyo haya maarifa uliyomwaga hapa nitayatumia pia kwa parachichi. Asante sana
 
Nashukuru mkuu, hiyo plan ya palachichi nataka nianze mwaka huu nina eneo wilaya ya mufindi nimeambiwa inafaa...kwahiyo haya maarifa uliyomwaga hapa nitayatumia pia kwa parachichi...asante sana

HABARI,
"mnyikungu,
Safi sana omba niulize heka moja wanauzae.

LUMUMBA
 

Asante mkuu, nina swali la ziada kutoka kwenye hizo video nimezifuatilia kwa umakini sana na nimeelewa kifanyikacho physically ila chemically kuna vitu huenda sijaelewa vizuri au sababu zake au mibadala yake, ni kuhusu hiyo plastic film anayozungushia nimeangalia video nyingi sana wengine wanatumia kitu kama gundi ya sellotape ambayo ina dark color wengine wanatumia hizo plastic film ambazo ni transparents halafu wana cover kikonyo kizima kilichobebeshwa kuprevent kisikauke kimsingi nataka kujua mazingira sahihi na vifaa vya kazi haswa kwa sie ambao tunatarajia kufanya kienyeji enyeji ili kupata matokeo sawa na anaebebesha kisasa na kuweza kupunguza gharama ikiwezekana.
 
Niko na takriba

Ni ekari 20 za miparachichi ambazo nimeanza kupanda kuanzia mwaka jana na mwaka huu shughuli zinaendelea,tamaa ya moyo wangu ni kuwa pia na shamba la mikorosho ktk maeneo Morogoro au Iringa.

Lkn ipo hofu kidogo juu ya haya mazao ambayo soko lake asilimia mia ni la nje,je kinini kimesibu zao la mbaazi ufuta ,choroko.nk kuporomoka bei kwa kiwango hicho?na je changamoto hii haiwezi kutokea kwa korosho?

Natanguliza shukurani comredi!
 
Nina heka 20 lindi nimeanza kulisafisha ikiwezekana msimu ujao nianze kupanda korosho inabidi nije PM kuchukua namba yako comrade Lumumba waweza kuwa msaada kwenye hatua zangu za awali za hili zao.
 

HABARI,
"jombezi,

Hongera Sana kuthubutu heka 20 za Parachichi ni uwekezaji mkubwa sana, kwa zao la korosho nashauri kama ukipata kwa morogoro Itakuwa vema sina taarifa za utafiti wa kina kama umefanyika Iringa na pia wakulima mkiwa wachache hakuna mnunuzi atakaye kuja kununua kiasi kidogo ni lazima kuwa wengi. Hilo la korosho nakushauri ungeliacha kwa sasa wewe wekeza zaidi kwenye parachichi ukikaa sawa na kuanza kurudisha pesa sasa unaweza kuangalia uwezekano hata wa kwenda mkoa wa pwani ukapata heka 200 uhakika upo kama unapesa ukaanzisha korosho.

Kwenye swala la mbaazi, ufuta, choroko, dengu shida ya hii ni kwamba soko kubwa lilikuwa India na wengi wanaopeleka kule ni wahindi wa hapa tanzania na walikuwa wanafaidika sana kwa kuwalalia wakulima tofauti na soko la korosho vietnam.Na pia ni kweli mnunuzi mkubwa alikuwa ni Manji sasa toka naye apate matatizo ya kesi sasa hakuna mnunuzi mwingine, ila kama tungekuwa na watanzania wenzetu wenye uwezo wakatafuta masoko nje na kununua mazao yetu na kuyapeleka huko ingekuwa Tiba kubwa kwa tatizo hili. Mfano mdogo ni zao la muhogo mikoa mingi zao la muhogo linastawi na kuna mbegu nzuri ziko kutoka kwenye vituo vya utafiti na china wanahitaji sana muhogo kwa matumizi mengi ila hakuna mtu wa kupeleka kule ila soko lipo. Hapa comrade kunatatizo kubwa sana.

Kwa korosho tatizo hili ni gumu kwakuwa soko kubwa lakorosho lipo marekani hata Vietnam wakinunua wao wanapeleka marekani na ulaya pia muda wa sisi kuvuna korosho nchi nyingi msimu unakuwa umekwisha hivyo mahitaji yake yanakuwa juu sana kama ilivyo parachichi inaweza kutokea ila pana ugumu sana hilo lisitukatishe tamaa Tupande.

LUMUMBA
 
Asante sana comredi,umenitia nguvu za kusonga mbele, barikiwa sana kwa ufafanuzi mzuri, wewe mi mtu mhimu sana kwangu nitazidi kukusumbua usipojali
 
Asante sana. Kuna mtu kanishawishi niingie kwenye hiki kilimo kulikuwq na fursa ya kununua mashamba mkoa wa Lindi kwa sh 50,000 kwa heka nimeshalipia eka 20, wiki ijayo nataka niende huko nikaone eneo na nianze matayarisho.

Tuendelee kujuzana kuhusu hili suala.
 
Asante sana comredi, umenitia nguvu za kusonga mbele, barikiwa sana kwa ufafanuzi mzuri, wewe mi mtu mhimu sana kwangu nitazidi kukusumbua usipojali

HABARI,
"jombezi,
Asante nawe pia. Amen ubarikiwe nawe pia usijali Karibu sana kama unaswali lolote muda wowote nitakujibu kwa kiwango cha juu cha uelewa wangu.

LUMUMBA
 
Brother Lumumba Ubarikiwe kwa maarifa unayo tupa hapa nimejifunza mengi mimi mwaka huu ndiyo ninataka nianze kupanda korosho maeneo ya kisarawe ila sina uzoefu wowote. Kuna mbegu ametuambia ni ya miaka mitatu naomba kujua kama unauelewa nayo nijue faida zake na asara zake ili nijipange mapema pia naomba kujua uzaaji wa hizi korosho pia nitashukuru sana.
 

HABARI,
"baba2,
Asante ubarikiwe nawe pia Samahani nilichelewa kujibu swali lako majukumu yalibana kidogo, Hongera kwa kuweka mkazo kwenye kilimo ndiyo Ninauelewa na hizo mbegu kwa uelewa wangu ni kweli kuna mbegu ziko za miaka mitatu hizo ni zile zilizofanyiwa utafiti na kuboreshwa Hasa kutoka kituo cha naliendele na hasa ubora wake unakuja kwanza zinaanza kutoa mazao ndani ya miaka mitatu ila muda unavyozidi kwenda ndio mavuno yanaongezeka na pia mbegu hizo zinahimili sana magojwa mavuno yake ni mengi ukifananisha na zile za kienyeji unaweza kukuta hizi za kisasa mti wa miaka 10 ukavuna kilo 30 kila mtu wakati zile za kienyeji zitachelewa kutoa mazao na mti wa miaka 10 ukavuna kilo 10. Pia hizi unaweza kupanda maramoja na nusu idadi kwenye heka moja tofauti na ile za kienyeji hizo ni faida mama zinazohitajika, kwenye hasara naomba nisitumie hilo neno huwa hakuna hasara ila kuna faida hasi ila ni za lazima kufata kwa kila mkulima mbegu hizi huwa zinahitai mbolea ya kupandia inashauriwa ili kuipa nguvu mimi naweza kusema hilo ndio kubwa.

LUMUMBA
 
Kaka Lumumba Nashukuru sana hapa umechochea kitu ndani yangu nitakuacha kwa sasa ila nitakuwa nakuatafuta Mara kwa Mara ili kile Mungu alicho weka ndani yako tukifaidi wote kaka.
 
Kaka Lumumba Nashukuru sana hapa umechochea kitu ndani yangu nitakuacha kwa sasa ila nitakuwa nakuatafuta Mara kwa Mara ili kile Mungu alicho weka ndani yako tukifaidi wote kaka
HABARI,
"baba2,
Asante nimefarijika sana kama nimeweza kutoa kitu na kikawa msaada kwa wengine wewe nitafute majukumu hayaishi mimi nimejitolea muda wowote wakati wowote uliza swali nitalitengea muda wa kulijibu wala usihofu hakuna kuniacha ukikaa kimya na mimi kuna mambo yatapotea kichwani uliza hata mje 100 nitajibu kila swali kwa muda wake kama litakuwa nje ya upeo wangu kuna wengine watajibu hakuna muda wa kupoteza tena.

Natamani kuona Tanzania ambayo hakuna kipande cha aridhi kikiota nyasi na vichaka mbadala iwe ni mazao ya biashara ya kutuletea fedha za kigeni na kupaisha uchumi wetu kuna nchi jirani tu hawana aridhi wanahangaika sisi tunayo tunaichezea alafu tunalia umasikini hata mbele za mungu ni dhambi kwasababu kila kaya ikiwa hata na mikorosho 100 hao sio masikini tena hii kitu inanipa shida sana"baba2,

LUMUMBA
 
Nawatafuta wakulima wa korosho Mtwara
 
Mkuu Lumumba asante sana kwa taarifa kwa kweli nimekuwa nafuatilia sana mada zako especially kwenye zao la korosho na nimekuwa interested sana najaribu kukusanya data maana nataka nifanye uwekezaji mkubwa sana kwenye hilo zao kwa kuanzia kama heka 100 swali langu je kwa tanga kama nitapata eneo na nikafanikiwa kulima wanunuzi wanakuja maeneo hayo au ndio mpaka tusafirishe kupeleka kusini au pwani na calcurated risk ya hili zao ni zipi.
 
Ubarikiwe sana mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…