Fahamu mambo mbalimbali kuhusu Kilimo cha Korosho

Nimevutiwa sana na kilimo cha korosho je mashamba ya kukodisha yanapatikana na gharama za kukodisha ziko vipi.
 
Asante sana.
 
Swali langu. Jee? Kwa Heka moja inatakiwa kitaalamu upande miche mingap? Na je, ukishapanda mikorosho ni ikawa mikubwa unaweza ukapanda mahindi yakakubali au mboga mboga. Au unaweza ukaotesha nyasi za mifugo ikakubali

HABARI,
"Come27,
Safi kwa swali zuri kwa kitaalamu idadi ya miti ya korosho kwa heka hakuna idadi kamili inategemea na mpango wako wa matumizi ya aridhi kama unataka kuchanganya mazao kama swali lako unaweza kupanda miti 50-80 kwa heka kama ni mpang wa korosho pekeyake mpaka miti 100-120 unaweza kama ukitumia mbegu za kisasa na unapopanda miti 120 baada ya miaka 10-15 unaweza kuanza kupunguza miti ikianza kubanana ila unakuwa tayari umesha anza kuvuna kwa muda.

Pia unaweza kabisa kupanda mahindi,mogamboga na nyasi za mifugo pia hakuna shida,KARIBU


LUMUMBA
 
Nimependa hapo uliposema

Duniani hakuna kuchelewa hadi unaingia kaburini..nami naongezea "utakachokifanya hapa duniani siyo lazima ukifaidi wanaweza kufaidi Hata wanao"


HABARI,
"Marire,
Asante hata wewe umeongea vema leo hii nchi nyingi zilizoendelea kama marekani wanatumia matunda ya waliotangulia ndio maana hata wao wanapambana kuweka sawa maisha ya wamarekani wa miaka 200 ijayo.

LUMUMBA
 


HABARI,
"daudthefarmer,
Kweli kabisa asante sana nashukuru,

LUMUMBA
 
Dodoma napo zinakubali saana hasa kongwa sehemu moja inatwa mkoka mashamba yapo kibao bei chee na yana rutuba balaa, wakenya ndio wanamwagika kuja kujichukulia mashamba kwa migongo ya wenyeji wakat sisi tumelala jaman. Mfano hizi picha hapa chini ni korosho za Dodoma ila sisi Watanzania jamani tuna shida saana.

 

Attachments

  • IMG_20171118_145306#1.jpg
    199.4 KB · Views: 103
hata hiyo ya kisasa huja kukua huwa kama ya kizamani, njoo shambani kwangu uione, usione inazaa ikiwa na tawi moja ukadhani inaishia hapo.
Unalima sehemu gani mkuu? Nataka Mimi nije wakati wa musimu kwa ajili ya manunuz na kwa wakulima wengine VP nitaweza kununua sh ngp per kg?
 
Unalima sehemu gani mkuu? Nataka Mimi nije wakati wa musimu kwa ajili ya manunuz na kwa wakulima wengine VP nitaweza kununua sh ngp per kg?
Njoo Liwale pia. Korosho zinapatikana kwa wingi sana.
 
Mkuu Lumumba,

Nashukuru kwa uhamasishaji wako mzuri. Nania ya kuwekeza kwenye korosho kuanzia eka 30 mpaka 100 kwa lengo la kupanda kila mwaka sio chini ya eka 20 kama Mungu akinipa nguvu.

Naomba kujua mambo yafuatayo mkuu;

1. Wapi panafaa kwa uwekezaji huu kati ya Lindi na Mtwara (hapa tukiangalia upatikanaji wa ardhi ya kutosha kuweza kupanuka kwa urahisi, bei ya ardhi kwa eka ya mkoa husika, miundombinu n,k).
2. Gharama za kupanda zikoje mathalani kwa eka moja hii itanisaidia kutengeneza bajeti.
3. Changamoto kubwa ya zao hili ni zipi?
4. wastani wa mavuno kwa mti mmoja ni kilo ngapi?

Natanguliza shukrani zangu za dhati. Naamini majibu yako yatasaidia na wengine pia na hatimaye kuhamasika kuwekeza kwenye zao hili ambalo lina fursa lukuki.

Asante
 
Kaka lumumba samahani mikorosho 17 waweza pata gunia ngp

HABARI,
"rommy shabby,
Karibu sana mdau bila samahani,Kipimo kizuri cha mavuno ya korosho ni kilo si gunia kwani bei yake huanzia kilo tofauti na mahindi kwa gunia. Mikorosho 17 kwa ule wenye umri wa miaka 5-10 unaweza kupata kilo 10-20 au zaidi inategemea na matunzo na kwa kilo ya sasa 3000-4000.

LUMUMBA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…