Fahamu mambo mbalimbali kuhusu Kilimo cha Korosho

Good
 
Mkuu nimeona ukihasisha ulimaji wa korosho kwa kutumia mikorosho iliyopandishwa. Maswali yangu inapatikanaje? Inapandishwa kwa miti gani?

Maana nijuavyo upandishaji wa mti juu ya mti mwingine (grafting)hutegemea uwepo wa miti mingine sasa shamba ukilima utapata wapi miti ya kupandishia?

Asante.
 

HABARI,
M2pc,
Safi kwa swali zuri,kwanza Kuna post moja nimeweka utaona video zinazoonyesha jinsi ya ubebeshaji Na mahali pa kupata miti ya kupandishia ni rahisi sana kama ukiwa tayari unayo miche ukaenda kwenye mti wowote mkubwa ila ni vema kujua uzaaji wake hapo unaweza kukata vipande vya nchani na ukaenda kubebesha kwenye kitalu chako.Vipande vilivyo katwa unaweza kuvishafirisha kwa masaa 24 mpaka mahali kilipo kitalu chako ila ni vema ukavifunga kwenye mfuko wenye unyevu ile visipoteze maji.

Miti mikubwa iko mingi sana mikoa Mtwara, Pwani, Lindi n.k

LUMUMBA
 
Lumumba ungeweka na garama kwa heka mpka kuvuna ungekuwa poa.

HABARI,
"chuma cha Mjerumani,

Niwie radhi ndugu kwa kuchelewa kujibu,Kwa gharama ya heka moja kama mche wa mkorosho ulioboreshwa wa sh,1000 kwa miche 100 ya heka moja utapata laki moja.Gharama ya uandaaji shamba kama mashimo na kusafisha kama shamba ni jipya hiyo inategemeana na eneo na hapo mbolea kama utapata ya samandi hapo itakuwa nzuri zaidi ila tuwekane wazi mbolea isiwe kikwazo mikorosho mingi imepandwa bila mbole na ikazaa vizuri hiyo isiwe kikwazo ndugu zangu.

Hapo nina uhakika kwa heka moja mpaka laki2.5-3 unaweza kuanza kilimo.

LUMUMBA
 
Bro upo vzr sn
 
Hongera mkuu kwa kutupa hii elimu. Naomba kuuliza ikiwa mikorosho inaweza kustawi vyema handeni mkoani tanga, ninalo shamba la hekari tano nafikiria kubadili aina ya mazao ya kilimo.
 
Nimefurahishwa na uzi huu. Bahati mbaya nimeingia wakati umeshaenda sana lakini natumaini mchango wangu unaweza kusaidia. Mimi ni mmoja wapo wa watu waliohamua kuingia kwenye hiki kilimo cha Korosho. Ni mmoja wapo wa walipata ardhi Manispaa ya Lindi na kupambana na kusafisha misitu. Mpka sasa hivi bado tuko site tunapambana maana kazi ya kusafisha misitu si kazi lelemama.

Huko tunaambiwa na wataalamu kuwa tupande kwa upana wa 12m x 12m, hivyo tunaweka miche 25 kwa ekari. Miche wanatoa bure.

Naweza kukubaliana na Lumumba nadhani ni kweli tunapoteza ardhi kwa kupanda miche 25 kwa ekari lkn ni ngumu kutofuata masharti ya wataalamu na Board ya Korosho wanaotoa miche.

Nadhani wazo la kupanda mingi alafu ukapunguza ikianza kushikana ni wazo zuri kabisa. Ntajaribu kuwauliza wataalamu na kuleta mrejesho.
 
Hbr yako kaka vp ardhi bado yapatikana huko, mie nimekuja tandahimba jana kucheki mashamba huku so bado nina zunguka kusurvey ila nimeshuudia mwenywe jinsi kilimo kilivyotoa watu katika maisha watoto wadogo tu walifanikiwa kuwekeza wanamiliki majumba mazuri magari ya biashara na kutembelea, kilimo kinalipa korosho inalipa tuacheni kelele tufanye kazi shambani tutapata mali. mie nipo tandahimba Kijiji cha kitama ya mwanzo ila home huko dar es Salam
 
Mkuu Ardhi ilikuwa inatolewa na Halmashauri ya Lindi. Sijuhi kwa sasa hivi kama bado wanatoa maana mvua ndo zinaishia labda mpk mwakani tena.
 
Hongera Sana kwa kuthubutu Ideally, karibu Tandahimba Wataalam tupo makin tutakusaidia kwa ukaribu ukiwa tayari. Ni taaluma yangu na ni ajira yangu. Nitafute tuijwnge Tanzania.
 
Hongera Sana kwa kuthubutu Ideally, karibu Tandahimba Wataalam tupo makin tutakusaidia kwa ukaribu ukiwa tayari. Ni taaluma yangu na ni ajira yangu. Nitafute tuijwnge Tanzania.
Asante sn kaka kwa kwel nimeipenda sn tandahimba jana nilikua mivanga huku kitama ya mwanzo nilikua naenda kucheki shamba kwa ajili ya kupanda korosho, nashukuru nimepata shamba ila ni la kujiandaa sn maana ni msitu flani hv ata hvy nilipata lingine lina miti 19 ya korosho. Wamakonde wakalimu mno wamenipokea vzr sn nashukuru ntakutafuta kaka. nimeona mwenywe jinsi korosho ilivyo Tajikistan watu ndani ya miaka 2 tu si mchezo yaani
 
Mkuu Ardhi ilikuwa inatolewa na Halmashauri ya Lindi. Sijuhi kwa sasa hivi kama bado wanatoa maana mvua ndo zinaishia labda mpk mwakani tena.
Njoo Lindi Kijiji cha rikwaya wameanza kuuza me nimechoka heka 50 nimeshapanda
 
Please naomba angalia sera ya kilimo kwanza na kipaumbele chake for the next five years. Na kama tuna road map yoyote.
 
Kwa heka yenye miti 25-30 unapata kg ngapi ?
Usipige mahesabu hayo piga hivi mwaka jana kilo ilifika 3900 na korosho wauza kwa kilo, gunia moja ni sawa na kilo mia sasa itategemea kwenye hiyo miti 25 au 30 utapata kilo ngapi, mfano miti yote ya korosho hiyo 30 au 35 umepata kilo elfu tano mia tano.

1kilo=3900tsh
5500kilo=×?
21,450000tsh hiyo kwa bei ya mwaka jana so mwaka huu hatujui if itapanda au laa kama itapanda itazidi kua neema kwa wakulima wa korosho. Na huo ni mfano tu kama utapata hizo kilo au kwa magunia itakua hv
1gunia=390000tsh
20gunia=?
7, 80000tsh
Ni hivyo tu nadhani kaka lumumba akija atatoa ufafanunuzi vzr. Shukran sana
 
Wakuu mkorosho una chukua muda gani hadi kuanza kutoa mazao(korosho)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…