Fahamu mambo mbalimbali kuhusu Kilimo cha Korosho

Lumumba
Shukran sana mkuu, nilibahatika kupata shamba Masasi na kwa sasa lipo kwenye maandalizi nitaomba ushauri wako kipindi cha kupanda mbegu mwezi November,
 
Nina shamba langu la hekari 50. Lipo Rufiji. Nataka kulima Korosho. Naomba nisaidiwe namna ya kupata mbegu bora na jinsi nitakavyozipata. Nimebahatika katika mtandao kupata mwongozo toka Bodi ya Korosho. Taarifa nilizoziona ndani yake ni pamoja na kwamba mbegu bora zinapatikana Naliendele.

Pamoja na ombi la awali, pia naomba kwa yeyote mwenye mawasiliano na watendaji wa kituo cha utafiti Naliendele anipatie contacts ama kama mtu anayemfahamu mkulima wa Korosho anayetayarisha mbegu bora, anisaidie mawasiliano mawasiliano ya mhusika nawasiliane kwa ajili ya kupata mbegu hizo.

Ni imani yangu wadau wapenda maendeleo mtanipatia msaada huo. Asanteni. Nasubiri kwa hamu kubwa kuwezeshwa niingie kazini.
 
Nakushuru sana kwa namba ya simu uliyotoa, lakini kila ninapopiga iko busy. Nimetuma ujumbe nao bado haujajibiwa.

Members, bado ninauhitaji sana wa mbegu hizo na abc za upandaji au ulimaji wa Korosho kama nilivyoeleza awali. Bado tumaini langu la kusaidiwa katika jukwaa hili ni kubwa.

Asante.
 
Wasiliana nasi sasa kwa mahitaji ya miche bora ya korosho kwa shilingi 1000 tu.

WhatsApp/call/text
0766006128
0655715184
0683433440
Ofisi zipo kilombero &kibaha (opening soon).
Vile vile tuna miche mbali mbali ya mbao kwa shilingi 400 tu
 
Wasiliana nasi sasa kwa mahitaji ya miche bora ya korosho kwa shilingi 1000 tu.

WhatsApp/call/text
0766006128
0655715184
0683433440
Ofisi zipo kilombero &kibaha (opening soon).
Vile vile tuna miche mbali mbali ya mbao kwa shilingi 400 tu

Habari
Kiongozi hv kwenye shamba la heka moja inaingia miche mingapi ya korosho?
 
Mbegu za mikorosho zinatolewa bure haziuzwi, kama uko Rufiji nenda ofisi za wizara ya kilimo watakuelekeza mahali vitalu vya miche vilipo hapo Rufiji.
 
Mwaka huu Miche ya mikorosho haitolewi bure. Kama una shida ya Miche Na utaalamu wa jinsi ya kuhudumia Shamba LA mikorosho contact 0784474935
 

Kagalala - Uliweza kupata mrejesho juu ya hili suala - kama wataalamu wa bodi ya korosho wanaridhia kupanda miche 120 kwa ekari (kwa upana wa mita 5-6 x 6-7)? Nauliza kujua kama ukiomba miche yao (ile wanayogawa bure) kama watakubali kukupa miche zaidi ya kipimo chao cha 25 kwa ekari.
 

Kwanza hakuna miche ya bure this year hiyo ilikuwa ni programme ya 2017/2018. Sina hakika na idadi ya miche unayoweza pewa kwa ekari ila wanasisitiza miche 28 tu kwa ekari!
 
Hapa

Sie wa mbali hautushauri kulima huko korosho? Najiona nimekuwa so interested lkn mamangu kanikatisha tamaa kuwa inahitaji close supervision, na wakati wa mavuno korosho hudondoka hivyo ni rahisi kuibiwa. Nimekatishwa tamaa lkn bado roho haitaki kuacha Jambo hili, nawe umesisitiza hapa.
 

Ni kweli! Ushauri wa mama yetu upo sahihi kabisa! Uwekezaji wowote unahitaji usimamizi (supervision) ya hali ya juu! Kumbuka kuwekeza ni jambo moja na kusimamia uwekezaji wako ili kufikia malengo uliyojiwekea ni jambo jingine!

Kuhusu kuibiwa wakati wa mavuno hiyo ni kweli ila inategemea na nguvu kazi uliyojiwekea katika hicho kipindi cha miezi miwili ya mavuno ili kuhakikisha hakuna upotevu mkubwa kwa njia hiyo!

Bado nakusisitiza amka na ifuate NDOTO yako!
All the best!
 
Very very educative thread! Tunahitaji mijadala ya namna hii siyo mijadala ya porojo porojo tu ambazo hazitusaidii chochote! big up wadau wote wa hii thread!
 
Habari Lumumba
Binafsi nimeanza kupanda korosho lakini mbegu zilizotumika sio miche bali ni korosho zenyewe, je kuna athari yoyote mkuu?
Shamba langu lipo wilaya ya Masasi , mbuyuni kitongoji cha Mitonji

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante kwa taarifa Je, mkuu msimu wa kupanda ni miezi ipi ambayo kuna mvua. Nahitaji kujua

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…