Fahamu matokeo ya meditation

Fahamu matokeo ya meditation

Meditation bora mtu akuelekeze ufanye mwenyewe na upate experiences zako mwenyewe. Kwa kusoma kitabu am afraid unaweza kuwa unafanya Meditation huku unatafuta experiences za aliyeandika kitabu, and this won't be a Meditation at all. Kama ni breath Meditation mtu akufundisha inavyofanyika then nawe unatoka na your own experiences.
 
🧘🧘🧘TOFAUTI YA MEDITATION NA KUNDALIN🧘🧘🧘
1736626072741.jpg

✍️Kutafakari ni mchakato wa kutupeleka kuelekea amani ya mwisho. Kadiri tunavyotafakari ndivyo tunavyomkaribia nguvu ya kiungu zaidi

✍️ Kundalini pia huamshwa kupitia kutafakari tu . Hii ina maana kwamba Kundalini ni nguvu iliyopatikana katika mchakato huu, kama matokeo ambayo tunasonga kwa kasi kuelekea Samadhi.

📖 Hapa tunaweza kusema kwamba Kundalini inafanya kazi kama injini inayokua haraka kwetu, lakini kuamka kwa Kundalini haimaanishi kuwa tumepata ukamilifu.

📖 Wakati Kundalini inapoamshwa, tunapata nguvu za kimungu, lakini kwa nguvu hizo hatuwezi kumfikia Mungu(ukamilifu), kwa hivyo watafutaji wa kiwango cha juu hawaachi kutafakari hata baada ya Kundalini Shakti kuamshwa, ili kufikia Mungu yaani kufikia ukamilifu Samadhi inahitajika

✍️ Samadhi ni hali kamili ya kutafakari na ni hapa ndipo tunamfikia Mungu.(ukamilifu)siyo kiumbe chenye ndevu nyingi na malaika huko mbinguni.

✍️ Kwa nini kila mtu anataka kufungua nguvu ya Kundalini moja kwa moja??

📖 Kabla ya kuamsha Kundalini, kwanza lazima aura ya nje iwe imetiwa nguvu, kisha aura ya ndani inatiwa nguvu, kisha chakras hutiwa nguvu, basi chakras zote zinatiwa nguvu, kisha chakra kuamka, kisha chakras zote huunganishwa na kisha Kundalini huinuka. , Kwa jinsi ilivyo rahisi kuandika, ni vigumu kuelewa na hata vigumu zaidi kufanya.


🧘Asili kwanza
 
Asante sana mkuu.
Mm natak kufahamu kuhusu womb healing
 
Meditation bora mtu akuelekeze ufanye mwenyewe na upate experiences zako mwenyewe. Kwa kusoma kitabu am afraid unaweza kuwa unafanya Meditation huku unatafuta experiences za aliyeandika kitabu, and this won't be a Meditation at all. Kama ni breath Meditation mtu akufundisha inavyofanyika then nawe unatoka na your own experiences. You will get your own story to tell. Thanks
Thank you so much!! Umenena vizuri sana.👍
 
Endelea mkuu Dogoli kinyamkela

  • Huwa unafanya meditation kila siku?
  • Una shuhuda gani za namna meditation imeweza kukusaidia hadi sasa?

Mimi hii issue ya meditation bado nina uelewa nayo mdogo sana, kiasi bado cha kushindwa kuamini. Naiona kama ni some kind of imagination tu, unapokuwa umefunga macho.

Labda pengine inawezekana ni vile hadi sasa in reality sijakutana na mtu ana kwa ana anayepractice hii, zaidi ya kuona tu kwenye Tv.
 
Unaposema meditation ya kutafuta roho yangu, hapo swali linabaki mimi ni nani. Maana kilichotafutwa na roho yangu na sio mimi. Je mimi ni roho?
Ndo unatakiwa ujitafute ujijue kama wewe n nani nanulikuja apa duniani kwa mission
  • Huwa unafanya meditation kila siku?
  • Una shuhuda gani za namna meditation imeweza kukusaidia hadi sasa?
Nina miaka 10 sasa Niko naishi nayo.
Pia faida zipo nying kama ninazo fafanua kwenye Uzi zangu,moja wapo umenipa furaha ya moyo(amani),kuona jambo kabla halijatokea,imenipa maisha mazuri mno kutoka nilipo kua ad sasa nilipo siwe vyema kupita bhakharesa ila Nina pata ninacho kitaka sio yaan ninacho kiitaj kupata iwe kula nk bas napata kwa wakat na nafanya nacho hitaji kwa wakat nk,mkuu faida n mingi mno siwez zimaliza apa
 
JINSI YA KUFANYA ILI ULIMWENGU UKUSIKILIZE

Imeandaliwa na kuandikwa na Dogoli kinyamkela
1736633030314.jpg


💞UMSIKILIAYE NDIYE AKUSIKILIZAYE

🗣️Kuna vitu katika jamii vikifanyika vinachukuliwa Kama uchawi au kiini macho, Siyo kwamba kiini macho hakuna, vipo na vinafanyika kila siku pasipo wengi wetu kuvitambua Kama Ni viini macho.

✍️Ulimwengu wote unaouona hauna tofauti, yaani Ni kitu kimoja Ila katika matoleo(version) tofauti tofauti. Na hapa ndipo tunakuja kupata ulimwengu mkubwa na ulimwengu mdogo, lakini yote kwa yote ulimwengu Ni mmoja tu nao Ni One-Verse badala ya Universe.

🤔Tuachane na hiyo mada maana nitakuja kuilezea siku nyingine kwa upana zaidi, Ila leo nataka niwaambie je tunawezaje kuusikiliza ulimwengu nao ukatusikiliza!!!

👌 Kwanza inabidi uelewe kwamba karibia elements zote ambazo hazionekani kwa macho ya damu na nyama Basi zinapatikana ndani ya mwili wa mwanadamu,ambazo hizo elements tukizichanganya changanganya ndiyo tunakuja kupata zile element nne za msingi.

🗣️Kwa mantiki hiyo Basi huu mwili wa damu na nyama Ni udhihilisho halisi wa vile vyote visivyoonekana.

🤝Hakuna mtu ambaye hawezi kumsikiliza rafiki yake kipenzi, Na hakuna mtu ambaye hawezi kumsikikiza ndugu yake, kwa nini kwa sababu mnasikilizana na kuelewana.

👊Sasa Kama sisi tunasikilizana marafiki kwa ndugu vipi kwa zile element ambazo ndiyo sisi wenyewe!!!

👉Katika SoMo lijalo Kuna kitu nitashea nanyi ambacho Ni maswali niliyoulizwa na watoto kutoka shule Fulani, na mengine niliulizwa na wazazi kutoka kwenye shule hiyo hiyo tukiwa kwenye moja ya semina za maadhimisho ya Uhuru.

🗣️Huu ulimwengu unaoonekana kwa macho ya damu na nyama Ni udhihilisho tu wa uleeee ulimwengu usioonekana kwa macho ya damu na nyama, na ulimwengu usioonekana ndiyo umeuumba ulimwengu unaoonekana.

🤔Katika SoMo lijalo nitaliezea hili kwa kina Sana, Sasa turudi kwenye mada yetu ya Leo, Kuna wengi sana ambao wamekuwa wakipenda Sana wasikilizwe na ulimwengu lakini hawajui wanasikilizwa vipi.

🗣️Labda nikudokeze tu kidogo kwamba wewe kuusikiliza ulimwengu hiyo Ni Sanaa Kama Sanaa zingine lakini ulimwengu kukusikiliza wewe hayo ndiyo MAAJABU Sasa.

✍️Ulimwengu unaongea na sisi kwa Njia nyingi Sana na tofauti tofauti, ulimwengu unaongea na sisi kupitia maumbo, muziki, michoro, Namba zinazojirudia, ndoto,nk.

✍️Kupitia hivyo vitu nilivyoviorozesha hapo Basi unaweza kung'amua jumbe ambazo ulimwengu unataka wewe uelewe.

🤔Kwenye maumbo na baadhi ya michoro Kuna Siri nyingi Sana za ulimwengu Ni kazi kwako kuweza kuzigundua hizo siri.

🎶Kwenye miziki tunayoisikiliza Kuna jumbe nyingi Sana za Siri ambazo ulimwengu unataka tuzifahamu hivyo Ni kazi kwetu kuzigundua hizo siri.

♾️Kwenye namba zinazojirudia na kwenye ndoto pia Kuna jumbe nyingi Sana za Siri ambazo ulimwengu unajaribu kuongea nasi na Ni jukumu letu kuzielewa Ila kila siku kila saa kila dakika ulimwengu unazungumzia na sisi.

🗣️Katika kuelewa ulimwengu unazungumza Nini hii Ni Sanaa lakini kubwaa zaidi Ni wewe kuuambia ulimwengu ukitakacho na ulimwengu ukatusikiliza na haya ndiyo MAAJABU yenyewe.

✍️Ulimwengu unahitaji uzifuate kanuni pia ili uweze kupokea maekelezo kutoka kwako, Lakini kitu kingine ili ulimwengu ukusikilize, ulimwengu unataka utambue kwamba wewe Ni ulimwengu pia.

😳Ulimwengu hautaki ujitofautishe nao maana ulimwengu unachukulia kwamba kila kitu Ni Ulimwengu.

⚛️Hivyo ukitaka ulimwengu uanze kukutii inabidi uondoe utofauti uliokuwepo Kati yako na vyote vilivyo ulimwenguni na ujione wewe Ni sehemu ya vyote yaani ujione wewe Ni vyote na vyote Ni wewe.

☯️Chochote utakachokitendea kitendee jinsi vile wewe unavyotaka kutendewa maana vyote Ni wewe na wewe Ni vyote.

🗣️Mfano unapouona mti chukulia kwamba umejiona wewe maana ndani ya mti Kuna Siri zako, unayaona maji chukulia Kama umejiona wewe maana kwenye maji Kuna Siri zako mule ambazo unatembea nazo kila siku.

✍️Unapoyaona madini chukulia Kama umejiona wewe maana madini Ni sehemu yako pia, Unapowaona wanyama na wadudu chukulia Kama umejiona wewe maana wewe Ni vyote.

✍️Hewa ilipo Basi jua Ni wewe maana wewe Ni vyote na vyote Ni wewe, Baada ya kujiona wewe kwenye vyote Sasa Kuna nishati ambayo itaanza kimiminika kuelekea kwenye kila kiumbe na kuanza kutambua kwamba Sasa wewe umekuwa mmoja wa wamiliki wa vyote kwa maana umetambua kuwa wewe Ni vyote.

🗣️Kila kiumbe kitaanzaa kukutii na mwishowee ulimwengu wote utakutii, Hapo utakuwa na uwezo wa kusema chochote nao ulimwengu wote ukakusikiliza, lakini zingatia katika Yale utakayoyataka Basi yawe ya heri kwenye mzunguko wa maisha haya ya kawaida maana Ikiwa na athari mbaya Basi ulimwengu utakutii na mwisho wa siku utakuadhibu pia.

Ulikuwa nami mwalimu wako Dogoli kinyamkela
🙏🙏🙏🧘🧘🧘🙏🙏🙏
 
Huu ulimwengu unaoonekana kwa macho ya damu na nyama Ni udhihilisho tu wa uleeee ulimwengu usioonekana kwa macho ya damu na nyama, na ulimwengu usioonekana ndiyo umeuumba ulimwengu unaoonekana.
Wanasayansi wanaita dark energy na dark matter hyo dark energy wanasema ni mystery force ambayo hawajui inatokana na nini na inakadiriwa kuchukuwa 68% ya ulimwengu kisha dark matter inachukuwa 27% na hyo iliyobaki ndio 5% ndiyo inayoonekana inachukua binadamu, wanyama, mimea, nyota na sayari na kila kitu unachokiona
 
Back
Top Bottom