MWANZO MPAKA UFUNUO NI SISI
Sehemu ya pili (2)
Imeandaliwa na kuandikwa na Dogoli kinyamkela
Tunaendelea na sehemu yetu katika andiko letu Hili.
Tuna Adam (Atom) ambayo ndiyo chanzo Cha vitu vyote vya kifizikia.
Pia tuna kukata kata Atom ambayo kule ndiyo tunaambiwa kutoka kwenye ubavu wa Adam, hapa Ni tendo la kuzizidisha spishi (species) kwani Kadri atom inavyokatwa katwa ndiyo inaizidisha nguvu, au nishati kwenye maisha.
Tukija Eva mwenyewe Ni Kama mawazo, au Yale mabadiriko ya ukuaji wa spishi ( species), Ule uwezo wa kufanya maamuzi, Hivyo Basi kwa kutumia mawazo yetu tunnaweza kufanya maamuzi yalio sahihi au batili.
Nyoka tumeona kwamba yeye Ni ni uti wa mgongo, ambao ndiyo kishawishi Cha mwili.
Tumechagua kile ambacho tulikiona kinafaa ambayo Ni uovu(evil) na hapo moja kwa moja tunakuwa tumejiondoa kwenye bustani ambao Ni ule upande wa kulia unaohusika na masuala yote ya kiroho, tuko kwenye ufizikia au upande wa kushoto.
Hizi pande mbili ambazo tunazichagua na kupambana nazo ziko ndani yetu kwa kila mmoja wetu, Huu upande wa kushoto ndiyo Cain ambao unahusika na mambo ya kifizikia, kidunia, hisia, Tamaa za kiakili tulizo nazo, Lakini upande wa kulia wenyewe unahitaji turudi na kuwa wamoja na Mungu, huu upande wa kulia ndiyo Abel, upande ambao unahusika na mambo ya kiroho.
Tunaona upande wa kushoto una uwezo wa kuuua upande wa kulia ambao Ni upande wa kiroho.
Wana wa Mungu wakaingiliana na watoto wa kike wa binadamu, hapa Ni zile tamaa zetu za kihisia zikiwa zimechanganyana na Ile upande mtakatifu ndani yetu, Na hapa ndipo dini zinapoibuka, ndani ya dini Kuna Mambo mengi tu mazuri ambayo wamekuwa wakiyafanya Kama kuwasaidia wahitaji, kuomba na kuimba huku wakimtukuza Mungu, lakini zimejichanganya naa huu upande wa Cain au wa kusboto, hivyo kujiona kwambaa wao ndiyo wenye upendeleo mkubwa kutoka kwa Mungu kuliko wengine, na hapa ndiyo majivuno (egos) yanapoibuka Sasa.
Wakawa na tamaa na kuanza kuwatala watu, na majivuno yakajiingiza ndani, hivyo tumelitengeneza bomu hatari la majivuno (egos) ndani yetu ya kujiona sisi Ni Bora kuliko wale, huku wale nao wakijiona wao Ni Bora kuliko wengine.
Kwenye dini tuna Ile dhana ya mgawanyo wa mema na mabaya.
Wote tumehusika kwenye kuitaka kata Atom/manii(sperm), mgawanyo wa Adam na Eva na maelezo yote ambayo tumeyaona huko juu.
MADARAJA/HATUA ZA UFAHAMU
DUNIA/Udongo(EARTH)
Dunia inawakilisha akili na machafuko, na hapa ndiyo tunakuja kupata uwili ndani ya asili ya kila kitu ndani yetu. Bila uwili hakuna machafuko, Kama ilivyoelezewa kwenye habari ya safina ya nuhu kwamba wanyama waliingia kwa pea pea yaani mke na mume, hiyo Ni hatua ya kwanza kabisa ya uzingativu (meditation) katika hii Hali yetu ya kifizikia. huko mbeleni tutaliangalia zaidi hili.
MAJI(WATER)
Maji yanawakilisha hatua inayofuata ya ufahamu, Tunapokuwa kwenye uzingativu (meditation) Kisha maji yakaanza kutiririka au sauti ndani yetu Basi hapa tunakuwa tunapaa na kuingia kwenye viwango vya kiroho.
Na haya ndiyo mafuriko Sasa ambayo yanasafisha machafuko yooote Yale ya kiakili ndani yako, Na hii inatokea pale unapokuwa katika uzingativu (meditation) wa amani ndani yako. Na huu ndiyo ubatizo kamili, na ubatizo Wala hautokea kwa kutumbukizwa au kuzamishwa au kumwagiwa maji.
Na hapa Sasa mahusiaano yetu na ulimwengu huu yanabadirishwa na Kama tambiko Basi hii ndiyo hatua ya kwanza la zoezi la kubadirishwa kutoka kuwa wa kidunia na kuingizwa kwenye ulimwengu wa roho.
Rejea ubatizo wa yohana mbatizaji hauna tofauti na hii habari ya safina.
HEWA/UPEPO (AIR)
Hapa Sasa tunaenda viwango vya juu, tunanyanyuka kutoka ule ufahamu wa maji na kuingia kwenye ufahamu wa hewa ambao unatuwekq huru kutoka kwenye mawazo na kuunganishwa kwenye Ile amani ya ndani.
Hatua ya kwanza Ni akili (mind) ambayo iko katika mawimbi ya beta 26 (beta waves) kwa mzunguko wa sekunde moja.
Hatua ya pili na ya tatu Ni mawimbi ya alpha (alpha waves) ambayo Ina mizunguko 14 kwa sekunde moja.
Lakini tunapoja hapa kwenye hewa mapigo yanapungua mpaka na kuwa mawimbi ya theta ambayo ina mizunguko 8 kwa sekunde moja.
Na hatua ya mwisho Ni mawimbi ya Delta ambayo ina mizunguko 4 tu kwa sekunde.
Hivyo kitendo chakuwa kwenye uzingativu au utulivu wa kiroho (meditation) kisayansi kabisa kinashusha hii mizunguko ya kiakili (mind), hivyo Basi mti wa ujuzi na mambo ya kiulimwengu yenyewe yapo kwenye hii mizunguko 26 kwa sekunde moja, na matokeo yake Ni machafuko, majungu, chuki, husda, nk.
Lakini pia hataa kusikiliza muzuki kunaweza kuyashusha haya mawimbi kutoka beta mpaka alpha, lakini siyo kitu Cha kudumu, yaani utayashusha kipindi kile unasikiliza na baada ya hapo yanarudi Tena.
Inabidi tutambue lengo letu kwenye akili Ni Nini ili tuweze kumjua yuleee kristo ndani yetu ili tuweze kuwa huru na kuwa kote kwa wakati mmoja.
Kitendo Cha kutoka mawimbi ya alpha mpaka theta Ni kile kitendo Cha bahati nyekundu inapofunguka ndani yetu, Na hapo Sasa tunaingia katika nchi ya ahadi tuliyoahidiwa,kutokana na kutokuwa na mawazo yenye chuki na machafuko Na hapo tunakuwa wamoja na Ile Roho iliyo ndani yetu.
Na hiyo ndiyo maana ya tutanyakuliwa kumlaki Bwana yesu mawinguni.
MOTO
Ubatizo wa Moto unakuja baada ya ule ubatizo wa hewa, na hapa ndiyo utakaso wa roho kupitia nafsi.
Kila kitu kiwezacho kuhimili moto, mtakipitisha katika moto, nacho kitakuwa safi, pamoja na haya kitatakaswa kwa hayo maji ya farakano, na kila kitu kisichouhimili Moto mtakipitisha katika hayo maji.
Sehemu za kiroho Zina mwanzo na mwisho, lakini pia Ni za milele, Ulimwengu wa roho una hatua zake tulishafundishana huko nyuma kwamba ukitoka hatua moja unaenda nyingine, Na tuko kwenye hiyo safari wote Ila kabla ya kubatizwa kwa Moto kwanza inatakiwa uanze kubatizwa kwa maji, ubatizo tumeshauzungumzia huko juu na sio Ile ambao wengi walikuwa wanaujua.
AKILI MPYA (renewed mind)
Baada ya hizo hatua za juu kukamilika, Sasa tunaingia kwenye kuzaliwa upya, Hapo Sasa tunakuwa Wamoja na baba yetu, wamoja na Mungu wetu, hapo tunakuwa Sisi Ni yeye na yeye Ni sisi.
Hatua hizo tunafanikiwa kuzifikia na kuzivuka tukiwa katika meditation au tajajudi ya Hali ya juu, inayopelekea kunitambua sisi wa kweli, Na hapo ndiyo tunakuwa tumeufikia ule.ufahamu wa kristo ndani yetu kupitia tajajudi (meditation).
Thomaso Akamwambia " bwana sisi hatujui uendako, nasi tutaijuaje Njia??.
Yesu Akamwambia Mimi ndimi Njia ya kweli na uzima, mtu haji kwa baba Ila kwa Njia ya Mimi.
Ulikuwa nami mwalimu wako Dogoli kinyamkela
Itaendelea.