Dr. Said
Senior Member
- Nov 16, 2010
- 126
- 533
Ningependelea unifafanulie jinsi ya kumkatalia mteja wako kumpa mkopo, tatizo ukitoa mkopo na mteja kapotea. Je kuna njia gani za kuepusha hilo
Unafanya biashara gani?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ningependelea unifafanulie jinsi ya kumkatalia mteja wako kumpa mkopo, tatizo ukitoa mkopo na mteja kapotea. Je kuna njia gani za kuepusha hilo
Dr, namba moja ndio ina maana tu, namba mbili na tatu zinakuja automatic! Hivyo, endelea kututafutia njia zingine hizo mbili! Mpaka sasa umetaja njia moja tu!
Nasubiri majibu hapaNingependelea unifafanulie jinsi ya kumkatalia mteja wako kumpa mkopo, tatizo ukitoa mkopo na mteja kapotea. Je kuna njia gani za kuepusha hilo
Utakuta hata duka huna, lkn unajifanya kushauri.Kama wewe ni mfanyabiashara au mjasiriamali unayehangaika kuongeza kipato cha biashara yako basi baada ya kufahamu njia tatu hizi utaona kuongeza kipato kwenye biashara yako ni rahisi kuliko kumsukuma mlevi.
Bila ya kupoteza muda tuanze mara moja
1. Ongeza Idadi Ya Wateja (Increase the Number of Customers)
Kipato cha biashara yako inatokana na wateja wanaonunua bidhaa au huduma unayotoa. Bila ya wateja huna biashara.
Na kila ukiwa na wateja wengi ndivyo kipato chako kinakuwa kikubwa.
Je Wateja Wako Utawapata Vipi?
Wateja hupatikana kwa kutangaza (wewe au watu wengine) uwepo wa biashara (au bidhaa/huduma) yako pamoja na kufanya mauzo (sales) baada ya wateja kuja kwako.
Bila ya matangazo watu wapya watakuwa hawafahamu biashara (au bidhaa/huduma) zako.
Kwa hivyo ni muhimu kuwa na formula ya matangazo yenye kuhakikisha wateja wapya wanakuja kila siku katika biashara yako.
Na matangazo unaweza kufanya kwa njia mbili.
Japokuwa njia hii ya kwanza (kuoneza idadi ya wateja) ni muhimu kwa kila biashara, njia hii sio rahisi na inaweza ikakugharimu kwa kiasi kikubwa kama utakuwa unalipia matangazo.
- BURE – Kuwa na duka au ofisi sehemu iliyo mbele za nyuso za watu, kuongea na watu ana kwa ana, kutumia mitandao ya kijamii n.k
- Kulipia matangazo – Hii itakusaidia kuwafikia maelfu ya watu kwa mpigo na kwa haraka kwa kuwekeza pesa kwenye jukwaa lenye watu wengi.
Na ndio maana kutegemea njia hiyo pekee biashara yako itakuwa hatariani, na ndio maana unahitaji kutumia na njia ya pili ambayo ni ku…..
2. Ongeza Idadi Ya Mauzo Ya Kila Mteja (Increase the Unit of Sales)
Kama kila mteja anakuingizia wastani wa shilingi elfu kumi kwa kila manunuzi, inabidi ujitahidi kumshawishi mteja huyo kununua bidhaa za ziada zitakazokufanya uongeza mapato kwa kila manunuzi.
Kama utaweza kuongeza wastani wa mauzo kutoka Tshs. 10,000 hadi Tshs. 20,000 kwa kila mteja, utakuwa ushaikuz biashara yako kwa 200% bila ya kuongeza idadi ya wateja.
Na uzuri ni kuwa wateja hawa tayari wanakujua, wanakupenda na wanakuamini. Kazi yako kubwa ya kufanya ni kuwapatia bidhaa za ziada na wewe unaongeza kipato kwa urahisi.
Swala la kujiuliza ni bidhaa gani ya ziada unayoweza kuwauzia wateja wako juu ya kile kitu wanachonunu kila siku?
Kama wewe upo katika biashara ya kuwatengenezea wateja wako tovuti, basi watahitaji kusajiliwa domain name na kurushiwa tovuti yao hewani au watahitaji kutengenezewa logo.
Kwa hivyo badala ya kumuuzia huduma ya kuwatengenezea tovuti ambayo pengine itakuingizia $500 peke yake, unaweza ukaingiza $20 ya usajili wa jina la tovuti hilo na $160 ya urushaji na $50 ya logo.
Kwa hivyo badala ya kuingiza $500 kwa kila mteja utakuwa unaingiza $730.
Unaweza hata ku ofa kuwatengenezea kurasa za mitandao ya kijamii ya Facebook, Twitter na Instagram kwa $100.
Kwa hivyo badala ya kutengeza $500 ya awali kipato chako kimekuwa ni $830 ambayo ni ongezeko la kipato chako cha awali kwa 66%.
Na uzuri ni kuwa haikugharimu pesa yoyote kuongeza kipato hicho na hutumii nguvu kubwa kumshawishi mteja huyo kwani alikuwa yupo tayari kufanya manunuzi kwako (yaani keshakuamini tayari).
Na hii unaweza kufanya katika biashara yoyote hata kama una kiduka kidogo cha kuuza vitu vya kuhitajika majumbani.
Kwa mfano ukiuza siagi unaweza kutoa ofa kwa mteja wako anunue na jam kwa bei pungufu.
KFC na McDonalds ni mahodari sana katika hili.
Ukiweka oda ya burger, wanakuuliza “je utapenda tukuwekee na chipsi katika hiyo burger?” ukisema ndio wanakuuliza tena “utapenda tukuwekee na kinywaji gani?”
Wewe na yako ilikuwa ni burger pekee yake lakini umejikuta unanunua na chipsi na soda.
3. Ongeza Idadi Ya Mauzo Endelevu (Increase the Frequency of Sales)
Jambo la tatu la muhimu kufanya ni kuhakikisha wateja wako wanarudi kwako mara kwa mara kununua bidhaa au huduma unayotoa.
Unaweza kufanya hivi kwa:
Nikitoa mfano wa mteja wako aliyetaka umtengenezee tovuti, kipato endelevu kwako hapo ni
- Kuuza bidhaa au huduma zinayopendwa na wateja wako
- Kuwasiliana na wateja wako mara kwa mara kuwajulisha kuhusu OFA ya bidhaa au huduma mpya unayotoa.
Vile vile unaweza ukampa OFA ya kumanage social media account zake kwa yeye kukulipa $200 au zaidi kwa mwezi.
- Domain Registration - $20/mwaka
- Hosting - $160/mwaka
Asikwambie mtu,
Hakuna kipato kitamu kama kipato endelevu
Unaweza kuwa na wateja 10 na ukaishi kama mfalme kwa sababu una kipato endelevu.
Chukulia mfano huduma hiyo ya social media marketing ambayo unawatoza wateja wako $200 kwa mwezi.
Ukiwa na wateja 10 tayari unaingiza $2000 ambayo ni Milioni 4.5 kwa hela zetu za madafu kila mwezi.
Japokuwa sio kila biashara inakuruhusu kuingiza kipato endelevu kama mfano niliotoa lakini unaweza kuwa mbunifu na kuhakikisha biashara yako inakupa kipato endelevu kwa wateja wako.
Mfano mzuri ni kuwasiliana na wateja wako wanaopenda kununua kwako mara kwa mara kila unapoleta mzigo mpya na kuwapa kwa bei ya OFA kama watachukua idadi fulani.
Ukifanya hivyo utakuja kugundua kuwa 80% ya mafanikio ya biashara yako inatokana na wateja wako wachache mno.
Hizo ndizo njia 3 pekee za kufanya kukuza biashara yako.
Je wewe unafanya njia ngapi?
Comment chini.
Ni mimi mwenye kujali mafanikio yako,
Dr. Said Said
MIMI NAUZA SPARE ZA PIKIPIKI WATEJA WANGU WA KUBWA N BODABODA KWAIYO KIUKWELI NAENDA KWA WATEJA KUONGEA NAO LAKINI UKIFIKA WANAKWAMBIA WANATAKA MKOPO NAFANYE HAPO KAKA..Ningependelea unifafanulie jinsi ya kumkatalia mteja wako kumpa mkopo, tatizo ukitoa mkopo na mteja kapotea. Je kuna njia gani za kuepusha hilo
Utakuta hata duka huna, lkn unajifanya kushauri.
Biashara haipo simple kama unavyoelezea broo.
Ww ni sawa na wale inspirational speakers, wanayafnya maisha yanaonekana simple lkn ukiingia mtaani uloambiwa yte uyafanye ndo utafanikiwa yanabuma.
Au maprofesa na madokta wa vyuoni wanafundisha uchumi wakat wao hata duka hawajawah kufungua au kuuza.
Biashara sio rahis kama ulivyoelezea.
MIMI NAUZA SPARE ZA PIKIPIKI WATEJA WANGU WA KUBWA N BODABODA KWAIYO KIUKWELI NAENDA KWA WATEJA KUONGEA NAO LAKINI UKIFIKA WANAKWAMBIA WANATAKA MKOPO NAFANYE HAPO KAKA..
Shukran kaka