Fred Katulanda
JF-Expert Member
- Apr 1, 2011
- 380
- 550
Habari wadau;
Leo naomba nidokeze namna ya kugawa Mzinga wenye nyuki ili kujaza mizinga yako mipya isiyo nyuki kwa njia ya haraka badala ya kutumia njia ya awali ya kuwatega na kungoja waingie jambo ambalo linaweza kukuchelewesha na kuchukua muda mrefu.
Kwa mnaofuga au mnaotarajia kuanza ufugaji njia hii inaweza kufanywa yeyote ilimradi aelewe maelekezo haya kwa usahihi na kuzingatia ili aepuke kuwafanya nyuki kukimbia ndani ya Mzinga waliokuwemo.
Mbinu hii ya kugawa makundi itawasaidia kujaza mizinga mipya kwa kasi na inaweza kabisa kujaza mizinga 3 kutokana na mzinga mmoja wenye nyuki, ingawa kupata idadi kubwa ya mizinga utakayoijaza hutegemea na uimara wa Koloni au ukubwa wake lakini na idadi ya viunzi au fremu zenye majana ambayo hayajafikia kuwa nyuki kamili.
Sasa ili kufanikisha jambo hilo hakikisha nyuki ndani ya Mzinga wako wamekaa muda mrefu na Koloni lako lina nguvu na kubwa, kisha fanya yafuatayo;
1. Hakikisha una mizinga yenye nyuki tayari hivyo chagua mzinga Bora wenye Koloni zuri ikiwezekana kuliko na uzalishaji mkubwa wa asali ili utumie kuwagawa.
2. Hakikisha mizinga mipya ambayo unataka igawia nyuki inafanana au inaingiliana zile (Fremu za ndani au viunzi) ili utakapohamisha kutoka mzinga mmoja kwenda mwingine isiwe shida ziweze kuingiliana.
3. Zoezi hili lifanyike jioni au usiku wakati nyuki wote wakiwa wamerejea ndani ya Mzinga na siyo mchana.
4. Fungua mzinga wenye nyuki (Hapa lazima uzingatie ubora wa Koloni kama nilivyoeleza kwenye namba 1.), pulizia moshi kuwafanya nyuki wako watulie na.....;
5. Chukua au toa Fremu ndani ya mzinga yenye Majana (Watoto wa nyuki walio katika hatua ya Lava na Pupa), kisha kaziweke kwenye mzinga mpya na sehemu ya nyuki wakubwa.
6. Pamoja na Fremu zenye Majana ahakikisha unakuwa na fremu yenye Majana na kiasi cha asali na kama haipo weka fremu yenye asali sanjari na zile zenye majana ndani ya mzinga mpya.
7. Eneo ulipotoa Fremu au viunzi kwenye mzinga uliokuwa na nyuki rejesha au weka fremu mpya tupu zisizo na masega ili nyuki waanze kuzijenga upya.
8. Fukinika mzinga yako yote miwili na itundike juu ya mti au kibandani maana utakuwa na mzinga mpya wenye nyuki pia.
9. Kumbuka mzinga mmoja unaweza kuugawa kwa kuweka fremu hizo zenye majana hadi ukapata mizinga 2 au 3 lakini itategemea na ukubwa ama wingi wa fremu zenye majana nada wake.
10. Kumbuka kuacha pia fremu zingine zenye majana katika mzinga uliokuwa na nyuki ili nao kuuacha jai nai.
11. Hakikisha hatua yako hiyo haitaamuaisha Malkia kwenye mzinga uliokuwa na nyuki, kwani wao wataandaa Malkia mpya kutokana na majana. Maana Malkia hurutubishwa na nyuki wafanyakazi kutokana na majana ya.nyuki kike ambayo wao huyatambua.
NB: Kwa ajili ya kusaidia wasioelewa zaidi naweka picha kuonesha aina ya masega ambayo unapaswa kuchukua fremu zake ili kugawa Mzinga ili kukupa picha ya jinsi utakavyo ziona na kuzichukua.
Ukiangalia picha hii kuna, Pollen ambayo NI chakuka huonekana hivyo ndani ya masega angalia nilipozungusha Rani ya blue.
Nimeeleza majana ambayo ukiyaona ndani ya Mzinga wako katika fremu ni hayo ambayo yapo katika hatua mbili, hapo nilipozungusha rangi ya kijani yakiwa katika hatua ya Lava na kwenye rangi nyekundu yakiwa hatua ya Pupa. Fremu au kiunzi kikiwa na muonekano huo ichukue kwa ajili ya kugawa.
Na picha hii itakusaidia kutambua, hatua za nyuki kujua na kupatikana kwa Majana wakiwa katika hatua za Lava na Pupa. Lakini namna nyuki anavyoanza hatua za yai mpaka kukamilika kuruka.
Unaweza kujisomea makala zingine za Nyuki;
Uvunaji wa Sumu ya NyukiUtegaji
Nyuki waingie kwenye mzinga
Asanteni naomba kuwasilisha, kwa msaada zaidi tupigie +255622 642620.