Fahamu mbinu ya kugawa makundi ya nyuki uliyonayo kujaza mizinga mipya isiyo na nyuki

Fahamu mbinu ya kugawa makundi ya nyuki uliyonayo kujaza mizinga mipya isiyo na nyuki

Siwajibu;
Binafsi nafurahi kuona mfugaji aliyeanza kazi ya ufugaji tayari. Mimi nipo Mkoa wa Mwanza tunaweza kuwasiliana na kubadilishana zaidi mawazo na ujuzi.

Kwa post hii unaweza kuendelea kuongeza mizinga mipya na kuijaza Kwa njia ya kugawa makundi badala ya kutega kugonja nyuki wingie wenyewe jambo ambalo litakuchukua muda mrefu.

Wasiliana nami; +255 622 642620
Asante mkuu, nipo Mwanza pia ntakwepo hadi mwezi wa kwanza, kazi ya ufugaji naifanyia Tabora na kuhusu kuingia nyuki haijanisumbua hata kidogo mizinga yote 10 imeingia ndani ya mwezi mmoja
 
Asante mkuu, nipo Mwanza pia ntakwepo hadi mwezi wa kwanza, kazi ya ufugaji naifanyia Tabora na kuhusu kuingia nyuki haijanisumbua hata kidogo mizinga yote 10 imeingia ndani ya mwezi mmoja
Asante tuwasiliane Jumanne ili uke kwangu hapa Mwanza mjini namba nimetoa.
 
Screenshot_20220930-003934~2.png

Haya maua yanajulikana Kama Golden Shower yanasaidia kupendezesha Nyumba lakini hulisha chakula Nyuki.
 
Pole Kwa kuchelewa kujibu, ngoja nikujibu.

Kuhusu kibanda: Nadhani picha unazoona zina uhalisia, katika kibanda mizinga upangwa lakini Kwa nafasi na kitalaam. Katika kibanda mizinga inapaswa kupanga kitalaamu.

Nyuki Wadogo: Hawa pia hufugwa na kuweka kwenye mizinga ya kienyeji au ya kisasa. Ila lazima mfugaji atambue nyuki Wadogo wanachangamoto kubwa kufugwa kuliko hao wengine.
Nitaweka tofauti zao kidogo hapa,
1. Nyuki Wadogo upatikanaji wao siyo Sawa na nyuki wakubwa ambao unatega wanakula, lazima ukanunue mbegu ili uwafuge.
2. Ni wepesi kuhama au kukuambia wanapokabiliana na changamoto kidogo. Hii ndiyo sababu waliowafuga wengi wamebaki na mizinga na nyuki hao (Wadogo) wakubwa hawapo wameondoka.

Siku tukijali niaandika Kwa kifefu na kufanya zaidi. Kwa sasa mfugaji anayetaka kufugwa kibiashara tunamshukuru kufugwa nyuki wakubwa maana ndiyo wanatoa pia asali nyingi kuliko Wadogo.
Kitaalamu mizinga inapangwaje bandani.
 
Yes, tunapoangalia eneo linalofaa ni lazima kuwa na uhakika wa malisho ya nyuki. Hivyo kama wewe unashamba na lipo jirani na msitu isiwe mbali sana (walau Mita 200-300) shamba lako litafaa kufuga maana nyuki watenda msitunikupata malisho yao.

Umegusia la maji, hili ni muhimu sana kwa nyuki. Ni vyema eneo liwe na maji, lakini hili siyo tatizo sana maana ni rahisi kujenga mabakuli ya kunywesha maji nyuki wako. Lakini lazima.ndani kuwe na both vitakavyoelea ili nyuki wakanyage kunywa maji maana nyuki hawajui kuogelea.

View attachment 1924100
Unaweza kuchimbia beseni, au kujenga kibwawa cha saruji Kwa ajili ya nyuki kunywa maji na ukahakikisha kinakuwa na maji msimu wa kiangazi zaidi. Ila ni lazima uweke vya vya kuelewa ili nyuki wakanyage kunywa maji.

View attachment 1924101
Mfano wa vitu unavyoweza kuweka nyuki wakanyage kunywa maji.
Mkuu naona uko vizuri sana kwenye hii Sekta ya Ufugaji Nyuki. Naweza kupata mawasiliano yako, maana mimi pia nataka kwa baadaye nijihusishe na kilimo hiki cha ufugaji nyuki.
 
Mkuu naona uko vizuri sana kwenye hii Sekta ya Ufugaji Nyuki. Naweza kupata mawasiliano yako, maana mimi pia nataka kwa baadaye nijihusishe na kilimo hiki cha ufugaji nyuki.
Mawasikiano yangu Call/What's App ni +255622 642620.
 
Kitaalamu mizinga inapangwaje bandani.
Mizinga kupangwa inapaswa kuachiwa nafasi isibanane japo hili wakati mwingine hutegemeana na ukubwa wake kibandani chako na mizinga yake. Kibandani chako kikiandaliwa kitalaam nafasi Kati ya mzinga na mzinga tutakuelekeza. Lakiki kwa ufupi hakikisha kila mzinga unakuwa kwenye reli yake ukijitengemea, isibanane na usipandishe au kubebabisha mzinga tofauti juu ya mwingine.
Hi hapa moja ya picha ya vinanda vyetu vya mizinga ya Nyuki.

Screenshot_20221015-003348.png
 
Karibu kwa mnaofuga au mnaotarajia kuanza, ulizeni tupeane ujuzi kwa kiasi nilichonacho.

..bado nina maswali kuhusu nyuki wadogo.

..nimevutiwa na taarifa kwamba nyuki hao hawang'ati.

..taarifa nyingine iliyonivutia ni kuhusu ubora wa asali yao.

..lakini kuna pia wana dis-advantage ya kuzalisha asali kidogo.

..swali langu ni kukosa uzalishaji wao wa mazao mengine kama maziwa ya nyuki, nta, venom, etc ukoje?

..pia kama uko mbali na msitu hauwezi kutengeneza kichaka / malisho ya nyuki ktk eneo lako ukafuga nyuki? Na kichaka / malisho hayo yanatakiwa kupandwa mazao gani?
 
Ukifuga Nyuki wadogo, huwezi kupata maziwa ya Nyuki, Nta, Venom zaidi ya Asali yao.

Kuhusu malisho ya Nyuki kuwaangalia au kutengeneza kipori chako, inawezekana. Lakini siyo lazima pori, bali unaweza kupanda miti ya malisho ikiwemo maua mbalimbali japo angalizo malisho yanapaswa kupandwa kwa wastani sababu yakizidi nyuki hupunguza uzalishaji asali. Nitakazia hili.
Watu wengi hudhani ukiwa na malisho mengi unaweza kuvuna Asali zaidi ya Mara 3 kwa mwaka sababu maua/malisho yanakuwa wengi na ya uhakika, lakini naomba nikuonye kufanya hivyo sababu wakiwa na hakika ya chakula kupatikana hawatahangaika na kusindika Asali.

Hii ndiyo sababu Mkoa was Singida wenye ukame umekuwa ikizalisha zaidi Asali. Sababu Nyuki wanalazimika kusindika Asali wakijua njaa unakuja (Asali ni chakula chao wanachokisindika kwa ajili ya kula wakati wa kiangazi ambako hakuna maua kutokana na ukame au kiangazi.
 
Nimejifunza kitu hapa
 
Back
Top Bottom