Fahamu mbinu ya kugawa makundi ya nyuki uliyonayo kujaza mizinga mipya isiyo na nyuki

Asante mkuu, nipo Mwanza pia ntakwepo hadi mwezi wa kwanza, kazi ya ufugaji naifanyia Tabora na kuhusu kuingia nyuki haijanisumbua hata kidogo mizinga yote 10 imeingia ndani ya mwezi mmoja
 
Asante mkuu, nipo Mwanza pia ntakwepo hadi mwezi wa kwanza, kazi ya ufugaji naifanyia Tabora na kuhusu kuingia nyuki haijanisumbua hata kidogo mizinga yote 10 imeingia ndani ya mwezi mmoja
Asante tuwasiliane Jumanne ili uke kwangu hapa Mwanza mjini namba nimetoa.
 

Haya maua yanajulikana Kama Golden Shower yanasaidia kupendezesha Nyumba lakini hulisha chakula Nyuki.
 
Kitaalamu mizinga inapangwaje bandani.
 
Mkuu naona uko vizuri sana kwenye hii Sekta ya Ufugaji Nyuki. Naweza kupata mawasiliano yako, maana mimi pia nataka kwa baadaye nijihusishe na kilimo hiki cha ufugaji nyuki.
 
Mkuu naona uko vizuri sana kwenye hii Sekta ya Ufugaji Nyuki. Naweza kupata mawasiliano yako, maana mimi pia nataka kwa baadaye nijihusishe na kilimo hiki cha ufugaji nyuki.
Mawasikiano yangu Call/What's App ni +255622 642620.
 
Kitaalamu mizinga inapangwaje bandani.
Mizinga kupangwa inapaswa kuachiwa nafasi isibanane japo hili wakati mwingine hutegemeana na ukubwa wake kibandani chako na mizinga yake. Kibandani chako kikiandaliwa kitalaam nafasi Kati ya mzinga na mzinga tutakuelekeza. Lakiki kwa ufupi hakikisha kila mzinga unakuwa kwenye reli yake ukijitengemea, isibanane na usipandishe au kubebabisha mzinga tofauti juu ya mwingine.
Hi hapa moja ya picha ya vinanda vyetu vya mizinga ya Nyuki.

 
Karibu kwa mnaofuga au mnaotarajia kuanza, ulizeni tupeane ujuzi kwa kiasi nilichonacho.

..bado nina maswali kuhusu nyuki wadogo.

..nimevutiwa na taarifa kwamba nyuki hao hawang'ati.

..taarifa nyingine iliyonivutia ni kuhusu ubora wa asali yao.

..lakini kuna pia wana dis-advantage ya kuzalisha asali kidogo.

..swali langu ni kukosa uzalishaji wao wa mazao mengine kama maziwa ya nyuki, nta, venom, etc ukoje?

..pia kama uko mbali na msitu hauwezi kutengeneza kichaka / malisho ya nyuki ktk eneo lako ukafuga nyuki? Na kichaka / malisho hayo yanatakiwa kupandwa mazao gani?
 
Ukifuga Nyuki wadogo, huwezi kupata maziwa ya Nyuki, Nta, Venom zaidi ya Asali yao.

Kuhusu malisho ya Nyuki kuwaangalia au kutengeneza kipori chako, inawezekana. Lakini siyo lazima pori, bali unaweza kupanda miti ya malisho ikiwemo maua mbalimbali japo angalizo malisho yanapaswa kupandwa kwa wastani sababu yakizidi nyuki hupunguza uzalishaji asali. Nitakazia hili.
Watu wengi hudhani ukiwa na malisho mengi unaweza kuvuna Asali zaidi ya Mara 3 kwa mwaka sababu maua/malisho yanakuwa wengi na ya uhakika, lakini naomba nikuonye kufanya hivyo sababu wakiwa na hakika ya chakula kupatikana hawatahangaika na kusindika Asali.

Hii ndiyo sababu Mkoa was Singida wenye ukame umekuwa ikizalisha zaidi Asali. Sababu Nyuki wanalazimika kusindika Asali wakijua njaa unakuja (Asali ni chakula chao wanachokisindika kwa ajili ya kula wakati wa kiangazi ambako hakuna maua kutokana na ukame au kiangazi.
 
Nimejifunza kitu hapa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…