Fahamu mzunguko halisi wa Jua na Sayari zinazolizunguka

dosho12

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2023
Posts
596
Reaction score
1,475
Wengi tumekuwa na mawazo ya kuwa dunia inalizunguka jua ambalo limetulia sehemu moja halizunguki wala kutembea ila kiuhalisia mambo yapo tofauti na unavyofikiria. wakati dunia na sayari zingine zikilizunguka jua, jua pia linafanya mzunguka mkubwa kwenye space likizunguka galaxy ya milk way likifanya hivyo kwa kutuchukua sisi na sayari zote ikiwepo dunia kwenye mzunguko huo



Galaxy ya milk way ni kubwa ikiwa imebeba nyota zenye idadi kubwa na sayari zake, gesi, vumbi na uchafu mwingi ikiwa na upana wa ( 100,000 light years)

miongoni mwa kitu cha kuvutia kuhusu galaxy yetu ni mzunguko wake kama gurudumu kubwa la duara linalopelekwa na upepo, mzunguko huo hufanya gesi na nyota zilizomo kuzunguka kwa mduara. Jua letu na sayari zake linapatikna kwenye mmoa ya mikono/mbawa zake umbali wa (25,000 light years) kutoka katikati ya galaxy

Kama vile dunia linavyolizinguka jua, jua linazunguka kwenye center ya galaxy ya milk way kwa kasi ya maili 143 kwa sekunde liki kamilisha mzunguko wote baada ya miaka millioni 230, mzunguko huo sio kama duara kabisa ila lina panda na kushuka kwenye galactic plane likitumia miaka millioni 60 kila likipanda na kushuka

Sio tu jua linalotembea bali hata galaxy pia zinatembea na kwa sasa galaxy yetu ikiwa inaelekea kwenye galaxy ya karibu inaitwa Andromeda.

galaxy ya milk way pamoja na galaxy zingine zilizopo kwenye kundi la galaxy linaloitwa Local Group likiwa na takribani galaxy 54 zote zikiwa zinaelekea kwenye mvutano mkubwa wa ajabu unaoitwa The Great Attractor,

pia hapo siyo mwisho ulimwengu wetu wote unatanuka kwa kasi kubwa na kufanya galaxy kuwa mbali mbali kuliko ilivyokuwa zamani
 
Wakati yakitokea hayo sisi huku tunakanyagana, tunatekana, tunauana na kuchinjana as if tunapambania kufika huko
 
Wazungu wanatupiga chai balaa
 
According na hiki ulicho elezea naomba nikuulize je unaelewa nini kuhusu mfumo wa Heliocentric na Geocentric?? 😎🀝🏽
Heliocentric inasema kuwa dunia na sayari zote zinalizunguka jua na geocentric inasema dunia ndio center ya universe na vitu vyote vinaizunguka dunia
 
Katika Galaxy la Milk way, solar system yetu inazunguka Kuelekea kati au nje?

Nini kitatokea tukifika kati au andromela na milk way zikikutana?
Zitaungana, hilo la kwanza sijakuelewa vzr
 
nimesoma mara nyingi kuhusu dark mater na dark energy ila sizielewi vizur
Dark Matter na Dark Energy kwa nilivyoelewa ni sawa na mtu aje na hesabu 4 + _ = 10; yaani penyewe huioni hiyo 6 hapo ila kwasababu ya hiyo namba 10 unajua kabisa hiyo nafasi "kitu chenye uzito kipo"
Dark matter na dark energy nayo ndio hivyo hivyo; kwa jinsi wanavyoutazama ulimwengu (the observable universe) hesabu katika makadilio ya uzito ni kwamba kuna asilimia kama 60% ambayo hawaioni Wala kui-detect ila kutokana na asilimia 40% wanayoiona inavyo-behave basi jibu ni kuwa kuna visivyoonekana lakini vipo (Dark Matter na Dark Energy)
 
Na ndio zinazosababisha Anti gravity au ?
 
You half man half genius πŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™ŒπŸ€ž
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…