Fred Katulanda
JF-Expert Member
- Apr 1, 2011
- 380
- 550
Kutega Mizinga ili iweze kuingia nyuki ni sehemu ya utalaamu unapaswa kufanyika kwa makini. Wafugaji wapya wengine wamekuwa wakitega bila kupata mafanikio kutokana na kukosa ujuzi, hapa ninawaletea namna ya kufanikisha utegaji na nyuki waweze kuingia ndani ya mzinga.
Hatua za kufuata;
1. Chukua Nta yako kisha iyeyushe kwenye moto ikiwa ndani ya chombo na uweke kwenye mchirizi ya viunzi (Fremu) ya mzinga wako,
2. Chukua majani aina ya Malumba (Nitakuwekea picha) sugua kuta za ndani ya mzinga wako.
3. Chukua kigaye au kipande cha bati na weka mkaa wa moto kicha chukua vipande vya Nta na Majani hayo (Malumba) na uyachome kufukiza ndani ya mzinga wako wa nyuki.
4. Funika vyema mzinga wako kisha kautundike kungoja nyuki waingie.
5. Hakikisha wakati wa kutundika mzinga wako mlango wa mzinga unakuwa mashariki au magharibi.
6. Tega mzinga wako kuanzia Miezi ya Agosti hadi April hasa (Machi na April ndivyo vipindi vizuri zaidi kwa upangaji makundi).
Pichani juu ni mmea ambao unajulikana kwa jina la Malumba unaotumika kusungua na kuchona ndani ya Mzinga ili kuita nyuki.
Mara baada ya kutega nyuki wakaingia ndani ya Mzinga wako, mizinga mingine siyo lazima utege upya bali unaweza kugawa makundi ya nyuki uliyopata na kujaza mizinga mingine, ni Kwa namna gani, fuatilia hapa.
Makala nyingine za ufugaji nyuki hizi hapa;
Ni nini husababisha asali kuganda?