Fahamu siri kubwa na faida ya DIGITAL MARKETING katika biashara yako

Fahamu siri kubwa na faida ya DIGITAL MARKETING katika biashara yako

Allmeads

New Member
Joined
Sep 7, 2021
Posts
3
Reaction score
2
deniskalinichenko210300088.jpg

MASOKO YA KIDIGITAL I(digital marketing) ni nini?

MASOKO KWA NJIA YA KIDIGITALI ni matumizi ya mtandao yaliyoanza kuibuka kuanzia miaka ya 90 mpaka 2000 yaliyokuwa na lengo la kuendeleza shughuli za kunadi masoko kwa uuzaji bidhaa mitandaoni/ na services (shughuli) kwa kutumia vifaa vya rununu(mobile devices), mitandao ya kijamii (Social networks), injini za utafutaji (search engines), na njia zingine kufikia watumiaji. Wataalam wengine wa masoko wanachukulia masoko ya kidigitali kuwa ni mapinduzi mapya katika ulimwengu wa kimasoko na wenye kuhodhi njia mpya ya kukaribia wateja na njia mpya za kuelewa jinsi wateja wanavyoishi ikilinganishwa na njia masoko ya awali.

Wafanya biashara wakubwa na makampuni makubwa duniani yameshajikita sana katika njia hii ya kisasa ya masoko ambapo inatofautishwa sana na njjia ya awali. Hii imedhihirishwa na tovuti ya investopedia mwaka 2020.



FAIDA ZA DIGITAL MARKETING NI NINI?

WhatsApp Image 2021-09-06 at 21.35.02 (1).jpeg

Kwa kuwa ulimwengu wa matumizi ya kidigitali katika dunia ya sasa umelenga sana ktk matumizi ya simu za viganjani /simu janja na kumpyuta. Hii imepelekea sana biashara nyingi nazo kuhamia huko ili kulenga hadira kubwa iliyo huko. Masoko ya kidigitali husaidia kufikia hadhira kubwa kuliko vile ungeweza kupitia njia za za kizamani, na walengwa ambao wana uwezekano mkubwa wa kununua bidhaa au huduma yako. Kwa kuongezea, njia hii mara nyingi ni ya gharama nafuu zaidi kuliko matangazo ya awali kama ya redio au televisheni, na hukuwezesha kupima mafanikio kila siku kwa kutumia mfumo (System). Ili kuona kama inaleta matokea chanya (Impact).

FAIDA KUU ZA DIGITAL MARKETING

Kuna faida nyingi tu za njia hii adhimu ya kutafuta masoko kidijitali, ila nitagusia tu faida kuu kama ifuatavyo.

1. Unaweza kupanga na kulenga kusudio lako kwa (hadhira) yenye uwezekano mkubwa wa kuwa wateja wako.

Kwa njia za kizamani kama Runinga, majarida, au ubao wa matangazo (billboards) ni ngumu kufanya tathmini ya matokea chanya ukilinganisha na njia hii ya kisasa

Mfumo wa Masoko ya kidigitali, kwa upande mwingine, hukuruhusu kutambua na kulenga hadhira maalum iliyokusudiwa, na kutuma Tangazo katika hadhira hiyo iliyobinafsishwa ( mfano jamii furum au website yoyote..)



Kwa mfano, unaweza kuchukua faida ya huduma za Blogs au website kuonyesha matangazo kwa hadhira fulani kulingana na vigeuzi kama vile umri, jinsia, eneo, maslahi, network providers, au tabia ya utumiaji wa injini ya utafutaji (search engine). pia, unaweza kutumia mikakati ya CPC (cost per click) au SEO (search engine optimazitaion) kusambaza matangazo yako kwa watumiaji ambao wameonyesha kupendezwa na bidhaa au huduma yako, au ambao wametafuta maneno maalum katika injini za utafutaji (keywords) ambayo yanahusiana na tasnia yako.

2. Utafiti
Tracking-1024x653.jpg

Masoko ya kidigitali hukuwezesha kufanya utafiti unaohitajika kutambua mnunuzi wako, na hukuruhusu kuboresha mkakati wako wa uuzaji kwa muda ili kuhakikisha kuwa unafikia matarajio ya uwezekano wa kununua. Juu ya yote, uuzaji wa dijiti husaidia soko kwa vikundi vidogo ndani ya hadhira yako kubwa. If you sell multiple products or services to different buyer personas, this could be a cutting edge method.

3. Ni ya gharama nafuu zaidi kuliko njia za kizamani

Mifumo ya Masoko ya kidigitali hukuwezesha (kama wewe ni advertiser/mfanyabiashara) kumiliki dashbodi itakayokuwezesha kupanga bajeti na kufuatilia kampeni kila siku (monitoring), njia hii itakuwezesha kupunguza gharama za kutangaza biashara yako. Mfumo utakuwezesha kutathmini matokeo chanya ya uwekezajji wako (Return on investment ROI). ITAENDELEA.....
 
Sawa mkuu, hebu lete mambo. Kuna viashiria kuwa kwa hapa Tanzania wanachanganya sana hii kitu ya Digital Marketing as a whole na Social media kama yenyewe
 
Back
Top Bottom