Fahamu Umuhimu wa Kufanya Management Audit na Performance Appraisal

Fahamu Umuhimu wa Kufanya Management Audit na Performance Appraisal

Masokotz

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2018
Posts
3,713
Reaction score
6,121
Habari za wakati huu;
Kwanza nianze kwa kuwapa pongezi wale wote ambao wamejitosa na kuamua kuanzisha biashara zao ndogo na za kati.Changamoto ni nyingi na muda ni mchache na Fursa nazo ni nyingi.Watu wengi wanaposikia neno audit huwa wanchofikiri cha kwanza kabisa ni Financial Audit.Hata hivyo Audits ziko za aina nyingi kam vile Safety audity,Operations Audit,Compliance Audit etc.Pia ipo Management Audit ambayo huwa tunaiita ni Mama wa Audit nyingine.Sababu kubwa ya kuiita hii mama ya Audit nyingine ni kwa sababu Audits nyingine zote zikiwa na aina yoyte ya kasoro basi ni ishara ya Kasoro katika Usimamizi yaani Managment.Ndio maana Findings zote hurudishwa kwao ili waseme watachukua hatua gani.

Leo nataka nizungumze kuhusu Umuhimu na namna ya kufanya Management Audit.Kabla ya kuzama ndani nitoe angalizo kwamba hata kama biashara au kampuni yako ni ya mtu mmoja usichukulie poa swala la kujifanyia audit kwani hata kama uko peke yako bado unahitaji kujifanyia Audit na kufanyiwa audit.Usifikiri kwamba kwa sababu uko peke yako basi utakuwa unafanya kazi kama askari wa zimamoto kukimbia kila inapotokea dharura ya moto.Matatizo mengi na changamoto mengi za kibiashara huwa zinaanza taratibu na kukua taratibu hadi kufikia kuleta madhara.Na unapofanya Audit inakusaidia kutambua tatizo kabla halijaleta madhara.

Ni wakati gani ni mzuri wa kufanya Management Audit?Unaweza kufanya Management Audit wakati wowote ule wa biashara yako.Wakati mzuri ni wakati ambapo kuna utulivu wa kiuendeshaji.Ni muhimu kufahamu kwamba unapofanya Audit ni lazima uanze kwa kufanya self assessment kabla ya kutafuta msaada kutoka nje.Hata hivyo unaweza kuleta mtaalamu wa nje kwa ajili ya kukuongeza katika kufanya self assesment na kukufanyia external assessment.

Unapofanya Managment Audit lengo ni kufanya "360 degree evaluation" ya mfumo wako mzima wa usimamizi na kuhakiki iwapo usimamizi wako unakidhi viwango kuendana na aina ya biashara,eneo ulipo na kanuni na taratibu bora za kibiashara.

Je ungependa Kuifanyia kampuni au biashara Management Audit?Je unajifanyia au kuifanyia biashara yako Management Audit?Je Unaona faida za kufanya management Audit?Karibu tujadili
I wapo unahitaji ushauri au msaada zaidi wa kufanya Management Audit tuwasiliane kwa email:masokotz@yahoo.com
 
Back
Top Bottom