Fahamu utabiri wa Marais wote wa Tanzania kutoka kwa wazee wa kale

Ametabiri sawa. Yule mtu mmoja kaiba kura( hiyo haina ubishi,nadhani,kwa sababu sasa hivi Bunge ni pure,it is not contaminated by members of the Opposition),na sasa mtu mwingine atachukua madaraka,yaani,Samia,ambaye,according to him,atatawala kwa muda mfupi.
Welle,ni vizuri kusema kweli lakoni nadhani Pharaoh alikuwa anawachinja wati wanaotabiri kwamba utawala wakel utakuwa mfupi.
Unamtisha mtabiri?
Tena mtabiri huyo Jeje alishafariki!!!
 
Mapigano anayoyazungumzia yalikua ya Shujaa LEMBESYA.
Maana yake kapambana na mtangulizi wake 'kunjerekela' AKA Toyota Crown
yaani NANASI.
Bw.Shujaa alishindwa kwenye box la kura hivyo akang'ang'ania kupita kwa kishindo.
LISO TUNGU maana yake ni jicho kubwa 'eliso' /jicho/ Tungurumuke *kubwa"
Maana yake daktari, chief aliyepo wakati huu.
SASA HUYU LISO TUNGU ATAPIGWA NA JIWE (sio shujaa)Ambaye ndio anafuatia baada ya hapa tulipo.

Sasa huyu mujee baada ya utawala wa Liso kupinduka kwa kupigwa na jiwe kubwa akapotelea hapo
Hapa umeeleza nini, mbona bado haiekeweki?!
 
Nakumbuka Sheikh yahaya aliwahi kutabiri pia "baada ya jakaya atakuja rais mkali sana lakini hatadumu atafariki kisha atakuja rais mwanamke" miaka ile niliona kama chai kuongozwa na raisi mwanamke.... kumbe imetimia
 
Ndiyo,Farao alikuwa anawatisha watabiri,anawaambia,"Nyie watabiri tuelewane,sitaki kumsikia mtu anasema 'Farao atakufa mwaka kesho''
Si Rahisi kuzuia kilichopangwa from above,

FARAO alitoa order wauwawe watoto wote wa kiume sababu Waganga wake walimtabiria kuwa Musa amezaliwa atakayewatoa waisraeli utumwani.

Wakauwawa watoto wengi sana, bt secret mission ilikuwa hivi,

Binti wa Mfalme FARAO alikuwa na Utaratibu wa kwenda kuoga mtoni, Mamake Musa akamchukua mtoto Musa, akamweka ktk kikapu kinachoelea, akamwacha mtoto aende uelekeo wa Binti mfalme Kwa njia ya maji ya mto,

Binti FARAO akaona mtoto, akamwokota, na ni mtoto mojawapo ambaye Babake alitoa AMRI auawe,

Binti FARAO akaenda kumsihi babaye amkubali mtoto wa Adui akuzwe ndani ya IKULU ya FARAO, na FARAO akakubali.

Musa akaepuka kifo, akalelewa IKULU na muda ulipofika, Akatoka IKULU kupambana na FARAO na kuwaokoa waisraeli Kutoka mikono ya FARAO.

Jiulize, ujasiri wa mama wa FARAO ALIUTOA wapi?

Alipangalo Mungu, mwanadamu hawezi pangua.

Amen.
 
MJEE/MZEE WA MUSOMA.
Katika wilaya ya Musoma kuna eneo mashuhuri kwa uvuvi na shughuli za kilimo linaitwa Majita,hili ni eneo linalokaliwa na Wajita kwa sehemu kubwa na Wakwaya ambao pia ni jamii ya wajita.

Nilipofika katika hili eneo ambalo kwa sasa limetengwa kuwa halmashauri ambayo makao makuu yako Mrangi,kabla ya kuhama kurudi Arusha niliifatilia historia ya hili eneo na kati ya mambo mengi ya kihistoria nilvutiwa na historia ya mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Mjee.

Mjee alikuwa hajaoa na alikuwa hana makazi maalumu,alikuwa mtu wakutembea tembea leo yuko kijiji hiki na wiki kesho yuko vijiji vingine.Alikuwa hana urafiki wa karibu na watu wazima,maana huwezi mkuta akijadiliana jambo na watu wazima ama wazee bali ni watoto wadogo ndo walikuwa ni marafiki zake.

Akiingia kijijini unakuta anatembea na rundo la watoto wadogo maana watu wazima walimuona kama hazimtoshi yaani punguani,ila walikuja kujua kama hakuwa punguani pale mambo aliyokuwa anawaambia yalipoanza kutokea ikiwa ni baada ya miaka mingi kupita.

Ni mtu wa pekee ukiifatilia historia yake maana alitabiri mambo mengi na hata yeye kujitabiria angali akiwa hai kuwa baada ya kifo chake kila mwanamke katika Majita nzima atakaye jifungua mtoto wa kiume ni lazima atamuita jina lake yaani Mjee iwe kwa kupenda ama kutopenda.Hili limethibitika ndani ya majita nzima,maana kwa kila mwanamke anaye jifungua mtoto wa kiume ni lazima amuite jina la Mjee ingawa atakuwa na jina lake lingine.Hivyo hata wazee wa miaka 90 kule majita waliitwa jina la Mjee na mama zao na hili halina ubishi,hii inaendelea hadi leo.

Nilipoongea na wazee wakaniambia alitabiri mambo mengi ikiwa ni pamoja na kuja kwa wakoloni,watu kuishi pamoja yaani vijiji vya ujamaa,watu kuishi kwenye vichuguu,kiongozi wa kwanza wa hili taifa kutawala akiwa tumboni,atake fuata na utawala wake,wa pili na hata wa mwisho na pia jiwe litakalo tokea.Alipo kuwa anayaongea hayo alikuwa anatoa sauti kama ya mtu anaye lia kwa kupiga mayowe.

KUJA KWA WAKOLONI.
Ikiwa ni kabula ya kuja kwa wakoloni,mjee alipita kwenye vijiji na kupaza sauti ya mayowe huku akifuatwa na msururu wa watoto na kuwaambia watu kuwa anaona mitumbwi mikubwa inakuja akimaanisha(meli na majaazi) imebeba watu ambao ni kama watoto(yaani ni weupe).Wanakuja ili kututesa na kila tulicho nacho watatunyang’anya. Alipo kuwa anayaongea haya watu wazima walisikika wakisema haaaa ni Mjee omusasi (yaani ni Mjee punguani/kichaa) alikuwa akidharaulika sana maana alionekana hazimtoshi.

Baada ya kifo chake na miaka mingi kupita ndipo wakoloni waliivamia Tanzania na hata wengine kufika majita na watu wengi kuuwawa wale walokuonesha upinzani wa kutawaliwa na wale watu.Maeneo yaliyo tumika kwa wenyeji kujificha wakati wa mapambano ni maeneo ya Makojo hadi Chimati,ambapo maeneo ya Chimati kuna mto ambapo mafuvu na mifupa ya watu ilionekan hadi miaka ya 1985.Ndipo hapo walianza kumkumbuka Mjee kuwa yule mtu hakuwa punguwani bali mtabiri.

VIJIJI VYA UJAMAA
Mjee alitabiri pia kuanzishwa kwa vijiji vya ujamaa ambapo alisikika akisema,ameiona mitumbwi inakuja huku imejaza mashoka(yaani jimbasa),akaona watu wanachukua mashoka na kufyeka pori(yaani kandokando) na akaona watu wanaishi ndani ya hayo maeneo. Akasema anaona watu wamejaa na wengi wanauana maana wamekosa mahala pa kuishi alipo kuwa anayasema hayo watu wazima wa maeneo aliyokuwa anapita walikuwa wanamcheka,ila kwa sasa maono yake yamesha timia.

WATU KUISHI KWENYE VICHUGUU
Miaka hiyo kila nyumba iliyokuwa inajengwa lazima ujenzi wake ulikuwa ama ukitumia nyasi,juu hadi chini ama ukitumia miti. Mjee aliona watu wakiishi kwenye vichuguu nadhani alishindwa kujua ujenzi unao tumika kwa sasa kutokana na uhalisia wa mazingira ya wakati huo na tekinolojia ya wakati huu.Vichuguu ni nyumba ya mchwa ambayo hujengwa na mchwa wenyewe kwa tope,ila alivyokua anaangalia huko mbele aliona pia watu wakiishi kwenye vichuguu yaani nyumba iliyo jengwa kwa tope kama za wakati huu.Hili halina ubishi maana maono yake yalitimia na yametimia kwa watu kutumia tope( yaani tofali) kujenga nyum

MTAWALA WA KWANZA KUTAWALA AKIWA TUMBONI
Miaka ya Mjee kuzunguka hili eneo la Majita,pia aliweza kutabiri kuhusu kiongozi wa kwanza wa nchi hii,akiwa katika kutembea na marafiki zake ambao walikuwa ni vijana wadogo,alisikika akisema(kwa sauti ya juu) kuwa ameoneshwa kuwa kiongozi wa kwanza atazaliwa huku majita,pia anaona huyo mtoto akitawala nchi akiwa tumboni maana wabaya wake watamuua,akasema ameona mtoto mwingine amezaliwa mashariki huyo ndo atakuja kuitawala nchi hadi ataacha mwenyewe,na atakuwa na amri juu ya hao watu weupe maana atawaambia ondokeni nyumbani kwangu nao watamtii maana wa mwanzo hatakuwepo tena.Aliyetabiriwa hapa ni mwl J.K.Nyerere maana Zanaki (Butiama) ipo mashariki mwa Majita

Baada ya miaka mingi kupita kati ya kijiji cha Bugunda au Bulinga alitokea mama mmoja mjamzito,ilikuwa ni kama muujiza pale mtoto aliyekuwa tumboni mwa mama yake alipo mwambia mama yake kuwa amzae ili akatawale nchi.Habari hii ilienea majita nzima kwa wakati huo hadi kwa machifu wa wakati huo hii haikuwa habari njema kwa watawala wa wakati huo kwani walidhani huyo mtoto atakuja kuwanyang’anya uchifu wao.Mtoto alipoanza kukua watawala wa wakati huo wakafanya mbinu ya kumuangamiza na hilo lilifanikiwa na kutimiza usemi wa Mjee wa kusema kuwa atatawala akiwa tumboni.Lakini baada ya mwl Nyerere kuja na kuikomboa nchi ndipo walipo kumbuka maneno ya mjee. Hili lilitokea kama maono ya mjee alivyokuwa ameoneshwa.

KIONGOZI ALIYEFUATIA.
Katika kutembea kwake huku akipiga mayowe,Mjee aliendelea na utabiri ambapo aliongea bayana kuwa baada ya utawala wa huyo atakaye tokea mashariki atakuja kiongozi mwingine atakeye tokea (Kwisinga) akimaanisha kisiwani,mda ukayoyoma na Nyerere alipo staafu kiongozi aliyefuata alikuwa ni Mzee Ruksa(Mwinyi).Waalokuwa na kumbukumbu ya kile Mjee alichoongea walikumbuka maana Mzee Mwinyi alitokea Zanzibar.

ATAKEYE MFUATA HUYO
Mjee alioneshwa kuwa baada ya huyo wa kisiwani atafuatia mtawala mwingine atakaye tokea mwisho wa nchi,Mtu akiwa Musoma(Mara) mwisho wa nchi itakuwa ni mikoa ya Ruvuma,Mtwara na Lindi.Lakini huu utabiri wake ulikuja kuthibitika pale Rais aliyefuata baada ya Mwinyi alitokea mkoa ambao uko mwisho wanchi kwa mtu atakayetokea mkoa wa Mara ama Musoma mwisho wa nchi ni mikoa niloitaja hapo juu ambapo BWMkapa alitokea mkoa wa Mtwara.

KIONGOZI ALIYEFUATA
Mjee alioneshwa katika maono kuwa atafuata kiongozi ambaye ni wa kunjekekera akimaanisha atatokea kandokando ya bahari ama ziwa.Katika awamu zilizopita tayari tumeshashuhudia kiongozi akitoka pwani ya bahari ya hindi.

Baada ya huo utawala atatokea kiongozi mwingine ambaye atatoka jirani na maeneo ya Musoma.Lakini baada ya huo utawala utafuata utawala wa LEMBESYA yaani atakayesawazisha kila kitu na kuweka kila kitu sawa ila katika maono alioneshwa kuwa Utawala huu wa LEMBESYA ataupata baada ya mapigano kidogo kutokea kutoka kwa mtangulizi wake mda huo maana atajaribu kung’ang’ania madarakani japo atakuwa ameshindwa kupitia sanduku la kura na pia utakuwa utawala wa mda mfupi maana utakuja utawala wa LISO TUNGU.

Lakini huu utawala wa LISO TUNGU utadumu japo si kwamda mrefu na utaondoshwa na utawala wa JIWE maana aliona katika maono jiwe kubwa likipiga utawala wa LISO TUNGU na baada ya hapo aliona giza tupu.

WAJITA MULIOKO HUMU MWAWEZA KUTUPA TAFASIRI YA HAYO MANENO YALOKOLEZWA NA KUTHIBITISHA UWEPO WA HUYU MTU HUKO MAJITA YA ZAMANI.
Very interesting although it is a story.
 
Mimi si Mjita ila mimi ni Mkabwa niliyezaliwa Kawe Dar es salaam. Nimependa sana habari za huyu Mjee na ningependa kufahamu zaidi ya haya kwa sababu ni muda mrefu najaribu kutengeneza documentary kwa ajili ya cultural tourism ya mkoa wa Mara. Mkoa huu umejaliwa kuwa na makabila mengi sana katika eneo dogo na kila kabila lina lugha yake na culture yake tofauti na nyingine, hii inafanya mkoa kuwa unique na kama tukifanikiwa kutengeneza hii documentary inaweza kusaidia kukuza utalii wa mkoa wa Mara na tukavutia watalii wengi kama unavyojua pia tuna Butiama tunaweza kuijumuisha.....Mimi naishi Arusha Sakina napatikana 0653 067 100 jina langu Dkt Mugassa Paul Mabere
Dkt wa heshima? PhD? Dkt wa binadamu Au wanyama Au Dkt wa matunguli kama Dkt Manyaunyau

Una fahamu kuwa kuna Makabila mengi huko kwenu Mara

Je una fahamu chanzo cha makabila hayo kutokea?

Umesema kuwa yana ongea lugha tofauti, je ni kweli?

Wewe una fahamu lugha gani huko mkoa wa mara?

Wajita na wajita wakabwa

Naona bado upo katika utafiti na ukiufanyia utafiti huo Dar na Arusha badala ya kwenda Mara kwenyewe

Makabila haya Mengi yame tokana na Makabila machache ya
Kurya
Jita
Ruo

Haya Makabila ndio yame zaa Makabila mengine mengi unayo yaona huko

Nakushauri ufanye tafiti zaidi, nenda ukajifunze toka kwa wazee, wazee ni hazina
 
MJEE/MZEE WA MUSOMA.
Katika wilaya ya Musoma kuna eneo mashuhuri kwa uvuvi na shughuli za kilimo linaitwa Majita,hili ni eneo linalokaliwa na Wajita kwa sehemu kubwa na Wakwaya ambao pia ni jamii ya wajita.

Nilipofika katika hili eneo ambalo kwa sasa limetengwa kuwa halmashauri ambayo makao makuu yako Mrangi,kabla ya kuhama kurudi Arusha niliifatilia historia ya hili eneo na kati ya mambo mengi ya kihistoria nilvutiwa na historia ya mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Mjee.

Mjee alikuwa hajaoa na alikuwa hana makazi maalumu,alikuwa mtu wakutembea tembea leo yuko kijiji hiki na wiki kesho yuko vijiji vingine.Alikuwa hana urafiki wa karibu na watu wazima,maana huwezi mkuta akijadiliana jambo na watu wazima ama wazee bali ni watoto wadogo ndo walikuwa ni marafiki zake.

Akiingia kijijini unakuta anatembea na rundo la watoto wadogo maana watu wazima walimuona kama hazimtoshi yaani punguani,ila walikuja kujua kama hakuwa punguani pale mambo aliyokuwa anawaambia yalipoanza kutokea ikiwa ni baada ya miaka mingi kupita.

Ni mtu wa pekee ukiifatilia historia yake maana alitabiri mambo mengi na hata yeye kujitabiria angali akiwa hai kuwa baada ya kifo chake kila mwanamke katika Majita nzima atakaye jifungua mtoto wa kiume ni lazima atamuita jina lake yaani Mjee iwe kwa kupenda ama kutopenda.Hili limethibitika ndani ya majita nzima,maana kwa kila mwanamke anaye jifungua mtoto wa kiume ni lazima amuite jina la Mjee ingawa atakuwa na jina lake lingine.Hivyo hata wazee wa miaka 90 kule majita waliitwa jina la Mjee na mama zao na hili halina ubishi,hii inaendelea hadi leo.

Nilipoongea na wazee wakaniambia alitabiri mambo mengi ikiwa ni pamoja na kuja kwa wakoloni,watu kuishi pamoja yaani vijiji vya ujamaa,watu kuishi kwenye vichuguu,kiongozi wa kwanza wa hili taifa kutawala akiwa tumboni,atake fuata na utawala wake,wa pili na hata wa mwisho na pia jiwe litakalo tokea.Alipo kuwa anayaongea hayo alikuwa anatoa sauti kama ya mtu anaye lia kwa kupiga mayowe.

KUJA KWA WAKOLONI.
Ikiwa ni kabula ya kuja kwa wakoloni,mjee alipita kwenye vijiji na kupaza sauti ya mayowe huku akifuatwa na msururu wa watoto na kuwaambia watu kuwa anaona mitumbwi mikubwa inakuja akimaanisha(meli na majaazi) imebeba watu ambao ni kama watoto(yaani ni weupe).Wanakuja ili kututesa na kila tulicho nacho watatunyang’anya. Alipo kuwa anayaongea haya watu wazima walisikika wakisema haaaa ni Mjee omusasi (yaani ni Mjee punguani/kichaa) alikuwa akidharaulika sana maana alionekana hazimtoshi.

Baada ya kifo chake na miaka mingi kupita ndipo wakoloni waliivamia Tanzania na hata wengine kufika majita na watu wengi kuuwawa wale walokuonesha upinzani wa kutawaliwa na wale watu.Maeneo yaliyo tumika kwa wenyeji kujificha wakati wa mapambano ni maeneo ya Makojo hadi Chimati,ambapo maeneo ya Chimati kuna mto ambapo mafuvu na mifupa ya watu ilionekan hadi miaka ya 1985.Ndipo hapo walianza kumkumbuka Mjee kuwa yule mtu hakuwa punguwani bali mtabiri.

VIJIJI VYA UJAMAA
Mjee alitabiri pia kuanzishwa kwa vijiji vya ujamaa ambapo alisikika akisema,ameiona mitumbwi inakuja huku imejaza mashoka(yaani jimbasa),akaona watu wanachukua mashoka na kufyeka pori(yaani kandokando) na akaona watu wanaishi ndani ya hayo maeneo. Akasema anaona watu wamejaa na wengi wanauana maana wamekosa mahala pa kuishi alipo kuwa anayasema hayo watu wazima wa maeneo aliyokuwa anapita walikuwa wanamcheka,ila kwa sasa maono yake yamesha timia.

WATU KUISHI KWENYE VICHUGUU
Miaka hiyo kila nyumba iliyokuwa inajengwa lazima ujenzi wake ulikuwa ama ukitumia nyasi,juu hadi chini ama ukitumia miti. Mjee aliona watu wakiishi kwenye vichuguu nadhani alishindwa kujua ujenzi unao tumika kwa sasa kutokana na uhalisia wa mazingira ya wakati huo na tekinolojia ya wakati huu.Vichuguu ni nyumba ya mchwa ambayo hujengwa na mchwa wenyewe kwa tope,ila alivyokua anaangalia huko mbele aliona pia watu wakiishi kwenye vichuguu yaani nyumba iliyo jengwa kwa tope kama za wakati huu.Hili halina ubishi maana maono yake yalitimia na yametimia kwa watu kutumia tope( yaani tofali) kujenga nyum

MTAWALA WA KWANZA KUTAWALA AKIWA TUMBONI
Miaka ya Mjee kuzunguka hili eneo la Majita,pia aliweza kutabiri kuhusu kiongozi wa kwanza wa nchi hii,akiwa katika kutembea na marafiki zake ambao walikuwa ni vijana wadogo,alisikika akisema(kwa sauti ya juu) kuwa ameoneshwa kuwa kiongozi wa kwanza atazaliwa huku majita,pia anaona huyo mtoto akitawala nchi akiwa tumboni maana wabaya wake watamuua,akasema ameona mtoto mwingine amezaliwa mashariki huyo ndo atakuja kuitawala nchi hadi ataacha mwenyewe,na atakuwa na amri juu ya hao watu weupe maana atawaambia ondokeni nyumbani kwangu nao watamtii maana wa mwanzo hatakuwepo tena.Aliyetabiriwa hapa ni mwl J.K.Nyerere maana Zanaki (Butiama) ipo mashariki mwa Majita

Baada ya miaka mingi kupita kati ya kijiji cha Bugunda au Bulinga alitokea mama mmoja mjamzito,ilikuwa ni kama muujiza pale mtoto aliyekuwa tumboni mwa mama yake alipo mwambia mama yake kuwa amzae ili akatawale nchi.Habari hii ilienea majita nzima kwa wakati huo hadi kwa machifu wa wakati huo hii haikuwa habari njema kwa watawala wa wakati huo kwani walidhani huyo mtoto atakuja kuwanyang’anya uchifu wao.Mtoto alipoanza kukua watawala wa wakati huo wakafanya mbinu ya kumuangamiza na hilo lilifanikiwa na kutimiza usemi wa Mjee wa kusema kuwa atatawala akiwa tumboni.Lakini baada ya mwl Nyerere kuja na kuikomboa nchi ndipo walipo kumbuka maneno ya mjee. Hili lilitokea kama maono ya mjee alivyokuwa ameoneshwa.

KIONGOZI ALIYEFUATIA.
Katika kutembea kwake huku akipiga mayowe,Mjee aliendelea na utabiri ambapo aliongea bayana kuwa baada ya utawala wa huyo atakaye tokea mashariki atakuja kiongozi mwingine atakeye tokea (Kwisinga) akimaanisha kisiwani,mda ukayoyoma na Nyerere alipo staafu kiongozi aliyefuata alikuwa ni Mzee Ruksa(Mwinyi).Waalokuwa na kumbukumbu ya kile Mjee alichoongea walikumbuka maana Mzee Mwinyi alitokea Zanzibar.

ATAKEYE MFUATA HUYO
Mjee alioneshwa kuwa baada ya huyo wa kisiwani atafuatia mtawala mwingine atakaye tokea mwisho wa nchi,Mtu akiwa Musoma(Mara) mwisho wa nchi itakuwa ni mikoa ya Ruvuma,Mtwara na Lindi.Lakini huu utabiri wake ulikuja kuthibitika pale Rais aliyefuata baada ya Mwinyi alitokea mkoa ambao uko mwisho wanchi kwa mtu atakayetokea mkoa wa Mara ama Musoma mwisho wa nchi ni mikoa niloitaja hapo juu ambapo BWMkapa alitokea mkoa wa Mtwara.

KIONGOZI ALIYEFUATA
Mjee alioneshwa katika maono kuwa atafuata kiongozi ambaye ni wa kunjekekera akimaanisha atatokea kandokando ya bahari ama ziwa.Katika awamu zilizopita tayari tumeshashuhudia kiongozi akitoka pwani ya bahari ya hindi.

Baada ya huo utawala atatokea kiongozi mwingine ambaye atatoka jirani na maeneo ya Musoma.Lakini baada ya huo utawala utafuata utawala wa LEMBESYA yaani atakayesawazisha kila kitu na kuweka kila kitu sawa ila katika maono alioneshwa kuwa Utawala huu wa LEMBESYA ataupata baada ya mapigano kidogo kutokea kutoka kwa mtangulizi wake mda huo maana atajaribu kung’ang’ania madarakani japo atakuwa ameshindwa kupitia sanduku la kura na pia utakuwa utawala wa mda mfupi maana utakuja utawala wa LISO TUNGU.

Lakini huu utawala wa LISO TUNGU utadumu japo si kwamda mrefu na utaondoshwa na utawala wa JIWE maana aliona katika maono jiwe kubwa likipiga utawala wa LISO TUNGU na baada ya hapo aliona giza tupu.

WAJITA MULIOKO HUMU MWAWEZA KUTUPA TAFASIRI YA HAYO MANENO YALOKOLEZWA NA KUTHIBITISHA UWEPO WA HUYU MTU HUKO MAJITA YA ZAMANI.
Inasemekana huko Morogoro Chief wao alitabiri ujio wa treni na magari hata mitumbwi ya Mindu dam
 
Ninyi ni wachache tunaompenda ni wengi na ndiyo wapiga kura hasa wa nchi hii.
Hasa hasa Waganga wa Kienyeji walimpenda sana Magufuri kuliko hata matunguri yao na sasa wanalia sana maana kula yao imetetereka sana baada ya Magufuri kufariki.
 
Duuuh watakuomba ushahidi mkuu
Mapigani yalikuwepo makali;watu kwa sababu watu wengi,au baadhi ya watu walikuwa wanataka Samia ajiuzulu awape nafasi ya kuunda serikali mpya. Samia akagoma. Kama alivyosema Samia,"Nilikwenda kwenye Katiba kuuliza 'kwani Katiba imeandika nini'"?
 
Back
Top Bottom