Fahamu utajiri uliopo kwenye uwekezaji wa dhamana za Serikali (Treasury Bills & Bonds)

Mkuu masharti ya kufungua benki tanzania na duniani kote ni lazima uwe na Security Fund ambayo unaiweka BOT na si chini ya Bilioni 10 ambayo in case ukafilisika wateja wako watapata magawio yao kama kawaida baada ya kufuata utaratibu husika...Rejea Twiga Bancrop baada ya kufilisika majuzi juzi!!! Kisha Sheria ya BOT katika investment yoyote ya kibenki hapa naamanisha All Fixed accounts ambazo zinaendeshwa Sheria ni kwamba mteja hatakiwi kupata hasara hata kama Benki ilipata hasara katika biashara iliyokuwa inafanya na hiyo pesa yako...wewe gawio lakp linabaki palepale regardless of all storms!
 

shackoor ,

Mkuu,

Hapo Sawa Sawa.

Basi , narudi Tanzania kuchukua pesa kwa tajiri Bishop Kakobe , nikawekeze kabisa hiyo 3B.
 
Asante sana. Hii ndio faida kubwa ya JF
 
kwa hiyo benki ikifilisika utakipata kiasi kilekile ulichokuwa nacho kwenye a/c??
 
Watanzania walio wengi wamezoea kukopa kwenye mabenki/ taasisi ya biashara. Hati fungani ni kinyume, ni benki/ taasisi ya biashara inakopa kutoka kwa wananchi. Kama ilivyo kwa mikopo mingine benki pia huaidi riba, na ndio inayofanya hati fungani kuwa na faida baada ya kuiva

Mabenki ya biashara yana maeneo kadhaa ya kukopa hela inapotokea imetetereka au ikiwa na uhitaji wa kujitanua, inaweza kukopa benki kuu, benki nyingine za biashara, ikauza hisa ili kuongeza mtaji, au kukopa kwa wananchi kwa kuuza hati fungani

Hati fungani hutofautiana na hisa kwa kuwa yenyewe haikupi umiliki wa kampuni husika bali inakufanya uwe ni mtu unayeidai kampuni husika. Hati fungani huiva na mtu hutakiwa kwenda kuvuna hela yake pamoja na ongezeko la ria ambalo lilikubaliana wakati wa mauzo

Hati fungani ni uwekezaji mzuri ikiwa mtu hawezi kufanya biashara nyingine zinazotaka mikikimikiki. Kwa mfano NMB waliwahi kuuza hati fungani huku wakiweka riba ya 10%, maana yake mtu atakapovuna tapata asilimia kumi zaidi ya kiwango alichoweka

Signed
Oedipus
 
Asante kwa andiko lako mkuu vipi unauelewa wowote kuhusu Forward Fx swaps?
 
Mkuu rejea source yako na uje na uhakika.
Swala sio source mkuu, makampuni hayafanani ndio maana nimekuambia kwa NMB wanalipa 10% per annum, sasa unaweza kuta makampuni mengine yakalipa tofauti bila kukiuka sheria za CMSA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…