Fundi mahiri wa ujenzi
JF-Expert Member
- Dec 10, 2012
- 4,159
- 2,844
- Thread starter
- #21
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nisaidie nifahamu tofauti kati ya beam na lentel.Unaweza kuanza nayo kwenye zege la chini na Beam pia
Beam ni Mkanda wa zege + nondo uliopo chini ya mlango na dirisha na mzunguko wa zege wa juu wakati lintel ni Mkanda wa zege + nondo Ambao zinazoziba sehemu za wazi Za dirisha na mlangoNisaidie nifahamu tofauti kati ya beam na lentel.
Mkuu Nimekupata. Je, nihakuna mwana jf atakaenufaika kwa mm kuweka namba zangu? Je, Kuna mtu amekulazimisha kutumia namba yangu?Mkuu sijakuelewa ulivyohitimisha kizembe wakati mjadara umeuanza sensitive? Nilitegemea utaelezea sababu zote lakini umeishia kuelezea sababu moja tu ukahitimisha na kwa masirahi binafsi kwa kutoa namba, kulikua na haja gani ya kuanza na mjadala si ungeanza na masilahi ndo unahitimisha na mjadala. Weka vizuri hapo ili tuweke kwenye ansadi. Mfano elezea sababu zako kama ulivyoziorodhesha, location,soil,uimara,nyakato n.k
Sent using Jamii Forums mobile app
Mungu akubariki sana,utafika mbali zaidi na zaidiHapa nitaelezea Sababu za msingi zinazosababisha majengo yanayofanana kujengwa kwa gharama tofauti.
Tuzungumzie mchoro wa nyumba ya vyumba vitatu vya Kulala kimoja kati ya hivyo ni master bedroom, sitting room, dining, kitchen ,public toilet na store.
Mchoro aliununua ndugu anaitwa Juma, baada ya Juma kununua Alitoa copy akawapa majirani zake wawili Hasani na John.
Hawa wote walijengewa na fundi mmoja ambae ni mimi. Lkn Kila mtu kutumia gharama tofauti kusimamisha boma.
SABABU ZA MSINGI ZA KUFANYA GHARAMA ZA UJENZI ZITOFAUTIANE :
1. location
2. Uimara
3.land type. (slop au tambalale)
4.soil type
5.nyakati.
HAPA NITAZUNGUMZIA UIMARA
Msingi wa nyumba imara utajengwa Kama ifuatavyo.
. Utachimbwa kwenda chini urefu WA mita moja au zaidi.
. Utaanza na zege yenye ratio nzuri kabla ya kujenga tofali
.Utajengwa kwa tofali imara
.Utawekewa Beam yenye kusukwa nondo na ratio nzuri
.Utamwagiliwa maji ya kutosha.
ILI HAYA YOTE YAFANYIKE LAZIMA UMPATE FUNDI MZURI.
Juma aliomba nyumba yake nimjengee kwa viwango hivyo, ndio maana nilitumia tofali nyingi,cement nyingi, nondo nyingi, mchanga mwingi, kokoto nyingi, ring za kutosha, maji mengi nk. Ktk kujenga msingi.
John alisema uwezo wake mdogo , yeye alihitaji tuchimbe futi moja kwenda chini baada ya hapo tujenge tofali, hakuishia hapo pia alisema tusiweke Beam.
Kilichotekea ni utofauti wa Tshs zaidi ya million nne kati ya hiyo misingi miwili.
Kiufupi Juma alitumia 6mil
John Tshs 2.8mil
Hasani Tshs 4mil.
Kilichotofautisha ni uimara WA kujenga msingi. Hawa wote ni majirani.
Mpaka tunamaliza boma Juma alitumia 18m
John 7m
Hasani 12m.
Nyumba zote hizi zikipigwa rangi vizuri hutoweza kujua madhaifu ya awali mpaka pale utakapoanza kuona nyufa (expansion joint)
Hoja yangu hapa ni kwamba unapotokea mjadala wa gharama za ujenzi LAZIMA tuzingatie vitu mhimu vinavyosababisha gharama kuwa kubwa au ndogo.
Ushauri.
1.Tusipende kukimbilia kununua nyumba wakati hujui ilijengwa kwa viwango vipi.
2.Jenga nyumba imara ogopa vya Bei cheee
3.Nyumba kuijenga si lelemama, ili kumudu anza mdogomdogo. Ukiwa na 5m anza hata msingi.
Ukihitaji fundi, usisite kunitafuta, Hakina utaenjoy service yangu.
0655173113
Asante, na iwe kama ulivyo nena
Hilo nitaliongelea nitakapoelezea soil type mkuu. Asante kwa kupitia uzi wangu.Mleta mada nakupongeza kwa kuipenda kazi yako. Ila nakuomba pia uwe unatumia ushauri wa wataalamu wa ujenzi. Namaanisha uchote maarifa kwa Architects, Engineer na Quantity Surveyor. Mie nimesoma ujenzi na nimepitia maelezo yako naona kama hayajajitosheleza pengine ni kutokana na ufahamu wa kitaalamu. Kwa mfano, nyumba sio lazima iwe na ground beam, kuna sababu hupelekea iwepo au isiwepo.kwa hiyo wakati mwingine mnaongezea gharama za ujenzi zisizokuwa za lazima kwa kigezo/kauli mbiu ya nyumba imara
Sent using Jamii Forums mobile app
Hahahahahaha waja hamkosi maneno ya shomboUnamuita fundi My unatafuta uchumba hapa kisa umesikia ni fundi mzuri.
Shenzi kabisa...
Huwezi kumwaga jamvi kabla ya kuweka mfumo wa maji, kama umefanyiwa hivyo jiulize wewe mwenyewe kwanza juu ya aina ya fundi uliyemtumia, yawezekana ulimtafuta mtu cheap.Kwanini nyumba zetu huwa zina majiko ndani lakini hazina sehemu za kutolea moshi nje?! Tangu kwa archtecture mpaka kwa civil engineer.
Kwanini mjenzi haachi maeneo ya kuweka vyoo, anamwaga zege kisha anakuja kutindua zege, wakati alifahamu tangu mwanzo kutawekwa mfumo wa maji machafu, na hata maji masafi, kwanin yasiwekwe wakati wa ujenzi wanasubiri jadi nyumba inaisha wanaanza gharama za kutindua zege na ukuta?!
Mnaposoma huwa hamfundishwi au ni ujinga wa wataalam wetu?!
We muongo mafundi wote mnajenga na kutindua, kuhusu chimney inahitajika kwenye majiko yote popote sio lazima kuwe na baridi, sema hamjui lakini sio kusingizia baridi.Huwezi kumwaga jamvi kabla ya kuweka mfumo wa maji, kama umefanyiwa hivyo jiulize wewe mwenyewe kwanza juu ya aina ya fundi uliyemtumia, yawezekana ulimtafuta mtu cheap.
Kuhusu kutindua kuta kwaajili ya wiring, hili huwezi kwepa labda zitengenezwe tofali zenye mifeleji.
Kuhusu sehemu ya kutolea moshi, hii inategemeana na location, always zinawekwa sehemu zenye baridi kali kwaajili ya kuwasha moto wa kuleta joto. Be blessed
Siwezi kuzuia unachokiwaza. Binadamu tunatofautiana Sana.We muongo mafundi wote mnajenga na kutindua, kuhusu chimney inahitajika kwenye majiko yote popote sio lazima kuwe na baridi, sema hamjui lakini sio kusingizia baridi.
Architecture anachora nyumba haweki chimney, ok unawrza kusema ni kazi ya structure engineer lakini naye haweki.
Masaki zile nyumba zilijengwa na wazungu zina chimney, wao hawana joto pale?!
Ok sawa kila la kheriSiwezi kuzuia unachokiwaza. Binadamu tunatofautiana Sana.
Binadamu tunamapungufu mengi sana, na mimi ni miongoni mwa watu wasio kamilika.Concept ilioulizwa ya chimney na wewe ulivyoijibu umenikata maini sana. As a layman najua chimney niku direct moshi usisambae ndani.
Wewe huenda ukawa fundi mzuri lkn jitahidi uongeze knowledge zaidi.
Pia nimekuona customer care yako sio nzuri. Work on that area. Majibu unayoyatoa hapa kwa watu ambao unaona wanakupinga kwa namna moja au nyingine siyo kabisa.
Samahani kama nimekukwaza. Samahani sana.