Fahamu vitu vinavyotofautisha gharama za ujenzi kwenye majengo yenye kufanana mchoro

Mkuu sijakuelewa ulivyohitimisha kizembe wakati mjadara umeuanza sensitive? Nilitegemea utaelezea sababu zote lakini umeishia kuelezea sababu moja tu ukahitimisha na kwa masirahi binafsi kwa kutoa namba, kulikua na haja gani ya kuanza na mjadala si ungeanza na masilahi ndo unahitimisha na mjadala.

Weka vizuri hapo ili tuweke kwenye ansadi. Mfano elezea sababu zako kama ulivyoziorodhesha, location,soil,uimara,nyakato n.k

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Nimekupata. Je, nihakuna mwana jf atakaenufaika kwa mm kuweka namba zangu? Je, Kuna mtu amekulazimisha kutumia namba yangu?

Kuhusu kumalizia hizo sababu zilizosalia nitamalizia soon boss wangu si unajua sisi wachezea tope tunavyokuwa na mda finyu wa kukaa nyuma ya keyboard!
 
Mleta mada nakupongeza kwa kuipenda kazi yako. Ila nakuomba pia uwe unatumia ushauri wa wataalamu wa ujenzi. Namaanisha uchote maarifa kwa Architects, Engineer na Quantity Surveyor.

Mie nimesoma ujenzi na nimepitia maelezo yako naona kama hayajajitosheleza pengine ni kutokana na ufahamu wa kitaalamu. Kwa mfano, nyumba sio lazima iwe na ground beam, kuna sababu hupelekea iwepo au isiwepo.kwa hiyo wakati mwingine mnaongezea gharama za ujenzi zisizokuwa za lazima kwa kigezo/kauli mbiu ya nyumba imara

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mungu akubariki sana,utafika mbali zaidi na zaidi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hilo nitaliongelea nitakapoelezea soil type mkuu. Asante kwa kupitia uzi wangu.
 
Kwanini nyumba zetu huwa zina majiko ndani lakini hazina sehemu za kutolea moshi nje?!

Tangu kwa archtecture mpaka kwa civil engineer.

Kwanini mjenzi haachi maeneo ya kuweka vyoo, anamwaga zege kisha anakuja kutindua zege, wakati alifahamu tangu mwanzo kutawekwa mfumo wa maji machafu, na hata maji masafi, kwanini yasiwekwe wakati wa ujenzi wanasubiri hadi nyumba inaisha wanaanza gharama za kutindua zege na ukuta?!

Mnaposoma huwa hamfundishwi au ni ujinga wa wataalam wetu?!
 
Huwezi kumwaga jamvi kabla ya kuweka mfumo wa maji, kama umefanyiwa hivyo jiulize wewe mwenyewe kwanza juu ya aina ya fundi uliyemtumia, yawezekana ulimtafuta mtu cheap.

Kuhusu kutindua kuta kwaajili ya wiring, hili huwezi kwepa labda zitengenezwe tofali zenye mifeleji.
Kuhusu sehemu ya kutolea moshi nadhani utamaduni na mazoweya ndio husababisha tusahau kuviweka. Be blessed ona mfumo wa maji ukiwekwa kabla ya zege
 
We muongo mafundi wote mnajenga na kutindua, kuhusu chimney inahitajika kwenye majiko yote popote sio lazima kuwe na baridi, sema hamjui lakini sio kusingizia baridi.

Architecture anachora nyumba haweki chimney, ok unawrza kusema ni kazi ya structure engineer lakini naye haweki. Masaki zile nyumba zilijengwa na wazungu zina chimney, wao hawana joto pale?!
 
Siwezi kuzuia unachokiwaza. Binadamu tunatofautiana Sana.
 
Concept ilioulizwa ya chimney na wewe ulivyoijibu umenikata maini sana. As a layman najua chimney niku direct moshi usisambae ndani.
Wewe huenda ukawa fundi mzuri lkn jitahidi uongeze knowledge zaidi.

Pia nimekuona customer care yako sio nzuri. Work on that area. Majibu unayoyatoa hapa kwa watu ambao unaona wanakupinga kwa namna moja au nyingine siyo kabisa.
Samahani kama nimekukwaza. Samahani sana.
 
Binadamu tunamapungufu mengi sana, na mimi ni miongoni mwa watu wasio kamilika.
Elimu haina mwisho, nitajitahidi kujua zaidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…