Fahamu vitu vinavyotofautisha gharama za ujenzi kwenye majengo yenye kufanana mchoro

Fahamu vitu vinavyotofautisha gharama za ujenzi kwenye majengo yenye kufanana mchoro

Ndio Maana huwa tunamchukua Fundi mchundo unampeleka site Na powder anachora kulingana na maelekezo yako. Ili kuepuka hizi gharama zenu.


Mfano, Mimi ninawakubali Sana Themibuider kwa Ramani nzuri na muonekano WA kuvutia WA Jengo, Ila bei yao Sasa

Sent using Jamii Forums mobile app
330m bati
3600ft 2by4
1620ft 2by2
yaani nyumba ya 12*10m inatumia bati 300?
 
Ando Limited ni superbrand miaka minne mfululizo kwa bizaa zao east africa. Na nimeona nyumba zaidi ya miaka 10 hazioneshi dalili hata kidogo ya kupauka
Na kunajamaa angu ameezekea Alaf Limited
Lakini zimesha anza kupaika. Nipeni uzoecu wenu
Weweweeee sio kweli Alaf alitumia Babu mpaka kitukuu kinatumia uliza kwanza Simba Dumu ina miaka mingapi ndio uje hapa Alaf itadumu na kudumu[emoji123]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Nimekupata. Je, nihakuna mwana jf atakaenufaika kwa mm kuweka namba zangu? Je, Kuna mtu amekulazimisha kutumia namba yangu?

Kuhusu kumalizia hizo sababu zilizosalia nitamalizia soon boss wangu si unajua sisi wachezea tope tunavyokuwa na mda finyu wa kukaa nyuma ya keyboard!
Haahaa mafundi mna mineno sana[emoji16]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapa nitaelezea Sababu za msingi zinazosababisha majengo yanayofanana kujengwa kwa gharama tofauti.

Tuzungumzie mchoro wa nyumba ya vyumba vitatu vya Kulala kimoja kati ya hivyo ni master bedroom, sitting room, dining, kitchen ,public toilet na store.
Mchoro aliununua ndugu anaitwa Juma, baada ya Juma kununua Alitoa copy akawapa majirani zake wawili Hasani na John.

Hawa wote walijengewa na fundi mmoja ambae ni mimi. Lkn Kila mtu kutumia gharama tofauti kusimamisha boma.

SABABU ZA MSINGI ZA KUFANYA GHARAMA ZA UJENZI ZITOFAUTIANE :

1. location
2. Uimara
3.land type. (slop au tambalale)
4.soil type
5.nyakati.

HAPA NITAZUNGUMZIA UIMARA
Msingi wa nyumba imara utajengwa Kama ifuatavyo.
. Utachimbwa kwenda chini urefu WA mita moja au zaidi.
. Utaanza na zege yenye ratio nzuri kabla ya kujenga tofali
.Utajengwa kwa tofali imara
.Utawekewa Beam yenye kusukwa nondo na ratio nzuri
.Utamwagiliwa maji ya kutosha.
ILI HAYA YOTE YAFANYIKE LAZIMA UMPATE FUNDI MZURI.

Juma aliomba nyumba yake nimjengee kwa viwango hivyo, ndio maana nilitumia tofali nyingi,cement nyingi, nondo nyingi, mchanga mwingi, kokoto nyingi, ring za kutosha, maji mengi nk. Ktk kujenga msingi.

John alisema uwezo wake mdogo , yeye alihitaji tuchimbe futi moja kwenda chini baada ya hapo tujenge tofali, hakuishia hapo pia alisema tusiweke Beam.

Kilichotekea ni utofauti wa Tshs zaidi ya million nne kati ya hiyo misingi miwili.

Kiufupi Juma alitumia 6mil
John Tshs 2.8mil
Hasani Tshs 4mil.

Kilichotofautisha ni uimara WA kujenga msingi. Hawa wote ni majirani.

Mpaka tunamaliza boma Juma alitumia 18m
John 7m
Hasani 12m.
Nyumba zote hizi zikipigwa rangi vizuri hutoweza kujua madhaifu ya awali mpaka pale utakapoanza kuona nyufa (expansion joint)

Hoja yangu hapa ni kwamba unapotokea mjadala wa gharama za ujenzi LAZIMA tuzingatie vitu mhimu vinavyosababisha gharama kuwa kubwa au ndogo.

Ushauri.
1.Tusipende kukimbilia kununua nyumba wakati hujui ilijengwa kwa viwango vipi.
2.Jenga nyumba imara ogopa vya Bei cheee
3.Nyumba kuijenga si lelemama, ili kumudu anza mdogomdogo. Ukiwa na 5m anza hata msingi.

Ukihitaji fundi, usisite kunitafuta, Hakina utaenjoy service yangu.
0693179844


UPDATES
tuendelee na mjadala wetu. Hapo awali tulijadili jinsi namna gani uimara wa nyumba unavyoathiri gharama za ujenzi. Leo tujadili namna location inavyoathiri gharama za ujenzi.

NAMNA LOCATION INAVYOSABABISHA GHARAMA ZA UJENZI KUWA TOFAUTI.

Mungu aliumba ardhi ktk mionekano tofauti. Kuna tambalale, milima na mabonde.
Ujenzi ktk Eneo tambalale unagharama nafuu kulinganisha na Eneo lenye slope . Lakini pia ujenzi wa Eneo tambalale lililoko Chanika mkoni DSM Unaweza kuwa na gharama tofauti na ujenzi wa Eneo tambalale lililoko msasani mkoani DSM. Hivyo hivyo ujenzi wa DSM unagharama kubwa kuliko ujenzi wa Mbeya.

SABABU ZA KUTOFAUTISHA GHARAMA KATI YA ENEO TAMBALALE NA LENYE SLOP.

sanasana hapa kimbembe huwa ktk kujenga msingi wa nyumba.

Msingi uliotumia tofali 1500 katika eneo tambalale, msingi huohuo ukitaka kuujenga ktk eneo lenye slope unaweza kutumia tofali 2300 au zaidi kulingana na ukali wa slope.
Tukumbuke kwamba Kwa kadri tofali zinavyoongezeka ndivyo na material mengine yanavyozidi kuongezeka kitu ambacho hupelekea kuongezeka kwa gharama za fundi. Si ajabu kumalizia 10mil ktk msingi wa nyumba ya Vyumba vitatu ktk Eneo LA slope.

Hivyo basi kama hutaki kutumia gharama kubwa kwenye ujenzi epuka kununua viwanja vilivyo na slope.

Jambo lingine linaloathiri ktk location ni upatikanaji wa material.
Mfano mtu anaejenga mbezi beach atanunua tani 18 Za mchanga zaidi ya 450.000 Tshs wakati mtu wa Chanika atanunua Kwa 220,000tshs.

Pia boma utakalojenga kwa 8mil Mbeya, DSM utalijenga Kwa zaidi ya 15mil. Sababu Mbeya tofali ni cheap, labour ni cheap nk.

JE, WAJUA KWAMBA KUNA MFUMO MPYA WA MAJI TAKA AMBAO HAUJAZI MASHIMO YA VYOO! USIHANGAIKE NA MFUMO WA ZAMANI. PATA MFUMO MPYA UACHANE NA GHARAMA ZA KUITA GARI ZA KUNYONYA UCHAFU.

Kwa ujenzi imara na wakisasa tutafutane 0693179844
Aise umenipa fundisho. Ebwana sasa wee kiservant kota unaweza jenga kwa bei gani?
Total sqm isizidi 60.
 
Fundi rafiki yangu anajenga nyumba mbili tambarare kwenye kichanga mwanza mara ya kwanza fundi alimwambia mawe tripu Kumi kila msingi mifuko 30 cement msingi wa kwanza akachimba cm 60 akamwambia aongeze mawe trip 6 chini kulikuwa na mawe ndo maana hakuendelea.sasa presure imekuja huu msingi wa pili fundi kachimba cm 90 kaweka mawe trip 16 kamwambia rafiki aongeze tripu 10 jumla ziwe 26 hapa rafiki anawaza amfukuze asubiri likizo asimamie
 
Fundi rafiki yangu anajenga nyumba mbili tambarare kwenye kichanga mwanza mara ya kwanza fundi alimwambia mawe tripu Kumi kila msingi mifuko 30 cement msingi wa kwanza akachimba cm 60 akamwambia aongeze mawe trip 6 chini kulikuwa na mawe ndo maana hakuendelea.sasa presure imekuja huu msingi wa pili fundi kachimba cm 90 kaweka mawe trip 16 kamwambia rafiki aongeze tripu 10 jumla ziwe 26 hapa rafiki anawaza amfukuze asubiri likizo asimamie
Mkuu tafuta qualified engineer hakikisha akupe cv zake usiokote okote mafundi kwa kutaka mteremko mwisho wa siku garama zake zitakukosti zaidi unavyofikiri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom