Sam Gidori
Senior Member
- Sep 7, 2020
- 165
- 417
- Kivinjari (Browser) ni programu ya Kompyuta au Simu ambayo hufanya kazi ya kupangilia, kuleta na kuonesha maudhui kutoka kwenye tovuti. Unapobonyeza kiungo (link), unatumia kivinjari kutembelea tovuti hiyo.
- Takwimu kutoka tovuti ya Global Stats Counter zinaonesha kuwa kivinjari cha Chrome kinachomilikiwa na Kampuni ya Google ndicho kivinjari kinachotumiwa na watu wengi zaidi, kikitumiwa na zaidi ya asilimia 64 ya watumiaji wote wa intaneti duniani, ikifuatiwa na kivinjari cha Safari kinachomilikiwa na kampuni ya Apple, zote za nchini Marekani.
- Hata hivyo, si vivinjari vyote vinavyotumiwa na watu wengi ni salama. Baadhi ya vivinjari salama zaidi ni pamoja na Firefox, Iridium Browser, Tor Browser nk.
- Kufahamu zaidi kuhusu vivinjari salama, soma:
Zifahamu 'Browser' salama zaidi uwapo mtandaoni
Browser kwa lugha ya Kiswahili huitwa Kivinjari. Hii ni programu ya Kompyuta au Simu ambayo hufanya kazi ya kupangilia, kuleta na kuonesha maudhui kutoka kwenye tovuti Ifahamike kuwa 'Browser' ni kiungo muhimu kwa watumiaji wa Mtandao Wa Intaneti. Zifuatazo ni Browser salama zaidi; 1: Firefox...
www.jamiiforums.com