mwakani naolewa
Senior Member
- Jul 25, 2024
- 148
- 426
mwaka 1982 february taree 26 ipo miamba mitano ilihisi inaweza kuitikisa serikali kwa kuteka ndege ya Tanzania ATC. ndege hiyo ilikua inatoka mwanza inakuja Dar es salaam imetua saa 11 jioni, kwa kipindi hicho uwanja wa ndege wa Mwanza ulikua hauna ulinzi kwahiyo hao jamaa watano walikuwemo miongoni mwa abiria waliokua katika ndege hiyo. Ndege ilipoanza tu kupaa saa 11;45 wale watekaji wakainuka na kuanza process za kuiteka ndege . walitumia bunduki za miti, walikua na mabomu(handgrunet)ambazo sio za ukweli . madai yao makubwa walitaka Rais Nyerere ajiuzulu kwa wakati huo kwakuwa yeye kama raisi alikua hafanyi kazi nzuri akiwa madarakani. walisemaa kwamba wao ni vijana ambao wako wengi wamejiunga na kutengeneza kikundi chao ambacho kinatetea haki za Watanzania. Hawa vijana walikua ni ndugu wote watano (Saidi Memba na Musa Memba) ambao walikua ni ndugu wakuzaliwa na walikua na shemeji yao ambaye ni kaka wa mke wa mmoja wapo. kulikua na mwengine Mohamedi Ali Abdallah na, Idi Abdallah nao pia walikua ni ndugu. Walikua wao watano na familia zao nazo zilikuwepo. Kiongozi wao ambaye alikua Said Memba alimuamuru Rubani aiongoze ndege ikatue uwanja wa Kenyata Kenya, wakatua na hapo wakaanza kuamrisha kua Nyerere ajiuzulu, wakati huo Nyerere alikua hajui kitu akiwa safarini, baada ya kufika ndo watu wakampa taarifa kua kuna watu wameteka ndege na wanataka ajiuzulu kwa wakati huo waziri wa habari na uchukuzi bw Malechella ndiye aliyepewa ndamana ya kuhakikisha anawakamata hawa watekaji na ndege inarudi salama. Waziri Malechella alifunga safari na kwenda kenya ili kuhakikisha ndege inarudi Tanzania. lakini kutokana masharti ya wale watekaji ndege ilishindikana kuja Tanzania ikapaa na kwenda kutua Qatar. Uongozi wa Qatar airport walikataa ugeni wa ndege ile paka rubani alipowasiliana nao na kuwaomba atue ili ajaze mafuta kisha aendelee na safari kwa sababu ndege imesafiri kwa muda mrefu
wakajaza mafuta na ndege ikaelekea paka uwingereza wakatua kule lakini taarifa zilikua zimekwisha fika hivyo wakaishikilia ile ndege na balozi wa Tanzania nchini uwengereza Oscar Cambona alikuja akashuhulikia suala hilo mpaka likaisha. baada ya hapo inasemekana walihukumiwa kwa sirii sana, haijulikani hukumu yao ilikua ya miaka mingapi. pengine Oscar Cambona ndiye aliyekua anawaongoza hawa vijana? wangepata wapi ujasiri huu?