Hio machine iko poa kabisa mzee baba,ingawa wabongo watakwambia ni jini mafuta mzee baba.
Na hizi ndinga foleni za dar ndo zinafanya yaonekane yanakula wese lkn ukiwa nalo mikoani huko hakuna foleni unapiga nalo misele kawaida tu mkuu.
Progress ina engine kama 4 hivi:
1.1JZ-GE hii ina cc 2500
2.JZ-GE hii ina cc 3000
Hizi ulaji wake ni kama vile brevis,cresta,mark 2/Verossa zenye engine kama hizo hapo juu,CC 2500 zinatosha kabisa kwa misele/safari/mbio.
CC 3000 kula wese inakula heavy kiaina.
Na hizo hapo juu ndizo engine common hapa bongo.
3.1JZ-FSE hii ni cc 2500
4.2JZ-FSE hii ni cc 3000
Hii engine ya 3&4 zenyewe zinatumia technology ya D4 ambayo wanalalamika zinabagua mafuta(ukiweka mafuta machafu tu inaanza kuzingua),sijawahi kutumia hizo gari yenye D4 so hayo malalamiko hua nayasikia tu kwa mafundi,lk pia wabongo ukitaka kuuza gari yako ukawaambia tu hii ina D4 jua imekula kwako maana wameshalibatiza jina baya.
Khs service parts zinaingilia na hayo magari mengine kwa hio ni zinapatikana tu,kwny body parts kama taa hapo ndipo sina uhakika kama ziko nyingi huko madukani.
Inshort mimi napenda hayo magari yanayoitwa jini mafuta,kwa hio kama mimi ningekua wewe ningelinunua bila kujiuliza mara 2.
ambazo engine zake hizi ni common tu maana zipo kwny magari kama brevis,cresta,mark 2.