Fahamu zaidi kuhusu kinga ya Ukimwi iitwayo PEP

Kaboom

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2011
Posts
10,828
Reaction score
15,001
PEP (Post - Exposure Prophylaxis) ni matibabu anayopewa mtu after been exposed to HIV ili kukukinga kuwa HIV positive.

Matibabu haya yanatakiwa kutolewa as soon as possible baada ya mtu kuwa exposed na HIV (ndani ya masaa 72) i.e kama zishapita siku tatu( masaa 72) matibabu haya hayawezi kufanya kazi

Matibabu haya hutolewa kwa muda wa mwezi mmoja (4weeks).

Swali: Mbona hiki kitu akizungumziwa sana na watoa huduma ya afya na wadau wanaohusika na mapambano dhidi ya ukimwi?

Je, ni gharama ama kuna side effects kubwa?



Ufafanuzi wa kina kuhusu (PEP)

PrEP ni nini?
Pre-exposure prophylaxis (PrEP) inamaanisha matumizi ya kila siku ya dawa za kujikinga dhidi ya maambukizi ya virusi vya HIV kwa mtu ambaye hana virusi hivyo, lakini yumo katika hatari ili kupunguza uwezekano wa kuambukizwa virusi vya HIV.

PrEP ina ufanisi wa kiwango kipi?
Ikitumika kuambatana na maagizo, PrEP inaweza kupunguza hatari ya kuambukizwa virusi vya HIV kwa zaidi ya asilimia tisini (90%). Hata hivyo, kwa sababu haikupi kinga dhidi ya maambukizi ya magonjwa mengine ya zinaa au mimba zisizotarajiwa inapaswa kutumiwa pamoja na kinga za aina nyingine kama vile mipira ya kondomu.

PrEP huzuia virusi HIV vipi?
Ukitumia dawa za kukinga maambukizi ya virusi vya HIV (PrEP) kulingana na maagizo uliopewa, dawa hizo hujenga kizuizi ambacho huzingira seli za mwili ili kuzilinda kutokana na maambukizi.Kwa mfano,ukijihusisha na tendo la ngono na mtu aliye na virusi ama kugusa majimaji kutoka kwa mwili wa mtu aliye na virusi vya HIV,PrEP inaweza kuzuia virusi kusababisha maambukizi mwilini mwako.

PrEP ina manufaa gani?
Ukitumia PrEP kwa kuzingatia maagizo uliyopewa,unaweza kupunguza kwa kiwango kubwa hatari ya kuambukizwa virusi vya HIV ,na kwa hivyo kukupa amani moyoni mwako.Hata hivyo, kwa sababu haikupi kinga dhidi ya maambukizi ya magonjwa mengine ya zinaa au mimba zisizopangwa,inapaswa kutumiwa pamoja na njia zingine za kinga kama vile kondomu kila wakati.

Dawa za PrEP zina athari gani?
Baadhi ya watu wanaotumia dawa za PrEP, huadhirika japo tu kwa
muda mfupi.

Ningali na kinga dhidi ya HIV nikikosa kumeza tembe
moja ya PrEP?

Ukikosa kumeza tembe moja au zaidi,unapunguza kwa kiwango kikubwa uwezo wa PrEP kukupa kinga kamili dhidi ya maambukizi ya virusi vya HIV.Utafiti
umeonyesha kuwa PrEP hukupa kinga bora dhidi ya HIV ikitumiwa kila siku kuambatana na ushauri wa mhudumu wa afya.

Tembe ya dawa za PrEP hutumiwa namna gani?
• Meza tembe moja kwa siku.

• Unahitaji kuzitumia kwa takriban siku saba kabla ya kujihusisha na tukio lolote ambalo linakuweka katika hatari ya kuambukizwa virusi vya HIV.

• Endelea kutumia dawa hizo kama ungali katika
hatari ya kuambukizwa virusi vya HIV.

Nifanye nini nisipomeza tembe ya PrEP kwa siku moja?
Meza tembe moja pindi unapokumbuka na kisha uendelee kumeza jinsi ulivyoshauriwa na mhudumu wa afya.

Nani anaweza kutumia PrEP?
Mtu yeyote ambaye hajaambukizwa virusi vya HIV lakini yumo katika
hatari kubwa ya kuambukizwa.

Ama kama una mpenzi ambaye:
• Anafahamika kuwa na virusi vya HIV lakini hatumii dawa za
kupunguza makali ya virusi vya HIV (ARVs)

Aidha:
• Anatumia dawa za kupunguza makali ya virusi vya HIV bila kuzingatia maelezo ya kuzitumia na kwa hivyo mwili wake haujafaulu kukandamiza virusi.

Na pia ikiwa:
• Una mpenzi au wapenzi ambao hawaijui hali yao ya HIV
• Una zaidi ya mpenzi mmoja
• Unaugua magonjwa ya zinaa mara kwa mara
• Unatumia dawa za kulevya za kujidunga
• Unashiriki ngono ili kupokea zawadi za fedha au zawadi za aina nyingine
• Unatumia dawa za kupunguza makali ya virusi vya HIV mara kwa mara baada ya kujihusisha na mambo yanayokuweka katika hatari ya kuambukizwa virusi vya HIV
• Mtu anayenuia kupata mtoto lakini yumo kwenye ndoa ambapo mmoja ana virusi vya HIV
• Hautumii mipira ya kondomu kila wakati au wakati mwingine unasahau kutumia unaposhiriki ngono
• Mtu ambaye mara kwa mara mipira ya kondomu hupasuka wakati anashiriki tendo la ngono
• Mtu ambaye ameshindwa kumshawishi mpenzi wake kutumia mipira wa kondomu ingawapo haijiui hali yeke ya HIV. Kwa maelezo zaidi tafuta ushauri kutoka kwa mhudumu wa afya.

Naweza gawa tembe za PrEP kwa watu wengine?
Usishiriki dawa zako na mtu mwingine, PrEP inapaswa kutumiwa na mtu aliyepata ushauri huo kutoka kwa mhudumu wa afya.

Ikiwa natumia dawa za PrEP,naweza kuacha kutumia mipira ya kondomu ?
Haupaswi kuacha kutumia mipira ya kondomu. PrEP sio chanjo.

Kuna tofuati gani katika ya dawa za kuzuiamaambukizi kabla ya tukio la hatari (Pre-Exposure
Prophylaxis) na zile za kuzuia maambukizi baada ya tukio la hatari Post-Exposure Prophylaxis (PEP)? Ingawaje PrEP na PEP hutumiwa na watu ambao hawana virusi vya HIV ili kuzuia maambukizi,dawa hizo ni tofauti.

PrEP inatumika kabla ya tukio ambalo linaweza kusababisha hatari ya
kuambukizwa virusi vya HIV ilikupunguza uwezekano wa maambukizi.PEP
inatumika baada ya tukio ambalo huweka mtu katika hatari ya kuambukizwa virusi vya HIV kabla ya masaa 72 hayajapita.

HIV Tukio ambalo huweka mtu katika hatari ya kuambukizwa Siku 7 Kabla masaa 72 hayajapita PrEP PEP

Dawa za PrEP zinazuia magonjwa ya zinaa na mimba?
Dawa za PrEP hazina uwezo wa kuzuia magonjwa mengine ya zinaa
wala mimba zisizotarajiwa. Dawa hizo zinapaswa kutumiwa kwa pamoja
na mipira ya kondomu .

Wanawake ambao wanatumia dawa za PrEP lakini hawako tayari kushika mimba,wanapaswa kutumia mbinu nyingine za kupanga uzazi.

Baadhi ya michango muhimu kutoka kwa wadau waJF
----
----
----
----
----
 
Ni ngumu kumeza ..tunaloweka.....mmedinyana jana hujui ka mwenzio anao...unakimbilia kupewa dawa ndani ya saa 72?

1. Unapima siku ya kwanza. Hakuna viashiria.

2. Unarudi baada ya mwezi/miezi3 ...kuthibitisha

Nahisi mnanichanganya kwa kusema masaa 72, vinginevyo uwe unatambua wazi umefanya na mwathirika
 
Nahisi mnanichanganya kwa kusema masaa 72, vinginevyo uwe unatambua wazi umefanya na mwathirika.

Si kila mkidinyana..ndo mana nikasema baada ya kuwa exposed na HIV( mf:umefanya mapenzi na muathirika na ukagundua mapema kabla ya hizo siku tatu).
 
UKIMWI mnavyouchukulia sivyo ulivyo, huu ni mradi kama BRT tu, by the way huwezi jua km umeathirika within 72 hours unless otherwise uwe unafahamu kama uliyefanya nae mapenzi ni muathirka. is ol I knw.
 
UKIMWI mnavyouchukulia sivyo ulivyo, huu ni mradi kama BRT tu, by the way huwezi jua km umeathirika within 72 hours unless otherwise uwe unafahamu kama uliyefanya nae mapenzi ni muathirka. is ol I knw

Huwezi kujua kama umeathirika ndani ya masaa 72 ndio..Na wala ukienda clinic hawakupimi kama umeathirika au hujaathirika.

Wanachofanya ni kukuuliza maswali, kwa nn umehamua kufanya PEP kabla hawajakuanzishia hiyo dozi
 
Lengo kubwa la PEP ni kukinga watoa huduma za afya dhidi ya maambukizi baada ya kupata majeraha wakati wa kutoa huduma. Majeraha haya yanahusisha kumwagikiwa damu, kujichoma sindando, ama kujikata na vitu vyenye ncha kali wakati wakitoa huduma.

Huduma hii pia hutolewa kwa watu waliobakwa kama kinga ya virusi.

WHO | Post-exposure prophylaxis (PEP)

Post-exposure prophylaxis (PEP) is short-term antiretroviral treatment to reduce the likelihood of HIV infection after potential exposure, either occupationally or through sexual intercourse. Within the health sector, PEP should be provided as part of a comprehensive universal precautions package that reduces staff exposure to infectious hazards at work.

Post-exposure prophylaxis to prevent HIV infection, Fact sheet - 1 December 2014

Key facts
WHO | Post-exposure prophylaxis to prevent HIV infection

Globally, there were an estimated 35 million people living with HIV, of whom 13 million were on antiretroviral treatment (ART) at the end of 2013.

People can be accidentally exposed to HIV though healthcare work or due to exposures outside healthcare setting, for example, through unprotected sex or sexual assault.

Antiretrovirals (ARVs) have been used to prevent infection in case of accidental exposures for many years. This intervention is called post-exposure prophylaxis (PEP) and involves taking a 28-day course of ARVs.

PEP should be offered, and initiated as early as possible, for all individuals with an exposure that has the potential for HIV transmission, and ideally within 72 hours.

If started soon after exposure, PEP can reduce the risk of HIV infection by over 80%. Adherence to a full 28-day course of ARVs is critical to the effectiveness of the intervention.

Recent evidence shows PEP uptake has been insufficient: only 57% of the people who initiated PEP have completed the full course and rates were even lower at 40% for victims of sexual assault.
 
Asante kwa kunielewesha mkuu ray lee

Huwezi kujua kama umeathirika ndani ya masaa 72 ndio..Na wala ukienda clinic hawakupimi kama umeathirika au hujaathirika..wanachofanya ni kukuuliza maswali, kwa nn umehamua kufanya PEP kabla hawajakuanzishia hiyo dozi
 
Last edited by a moderator:
rpg Sio lazima iwe kwa watoa huduma za afya tu, kama ni kinga basi kila mtu anaweza kupatiwa!
 
Mbona madaktari wana ngoma au haijui?

Hii inafanya kazi kama utawahi kuanza matibabu(ndani ya siku tatu toka virusi kuingia mwilini)..so sio watu wote wanajijua wamepata virusi ndani ya muda huo.

Watu wengi wanajijua wanavirusi baada ya kupimwa na kukutwa navyo ina maana hapo inakuwa ishapita siku,miezi au miaka kadhaa tangu virusi kuingia mwilimi..so haya matibabu yanakuwa hayana maana kwa kipindi hicho
 
Watu naona wanahisi wamebaniwa. Ni hizo ARV tu. Ila hata wahudumu wa afya huwa wanaogopa kutumia, sijui kwa nini.
 
Mtu mwenye akili timamu hata akisikia tu yule ana ukimwi hawezi kumgusa, halafu mtu adinyane tena pekupeku huku akijipa matumaini ya kutumia PEP!!

Kaka naona umekuja kiushindani na sio kwa lengo la kuelimishana.Ndo mana nikakujibu vile nikijua na ww utajiongeza..wapi nimesema mtu ukazini makusudi na mtu aliyeathirika kwa vile kuna PEP??..

What if unafanya mpnz na mtu zen baadae/kesho yake unaambiwa yule ni mwathirika?..vipi kama ndugu yako wa damu ni muathirika na home ndo mnamuuguza zen ikatokea contamination yeyote kwa bahati mbaya??..wat bout ma-nurse na wauguzi wengine wa afya wanaowahudumia waathirika, nao wako kwenye risk ya maambukizi..sababu ziko nyingi,zote hizo hujaziona??
 
nahisi mnanichanganya kwa kusema masaa 72, vinginevyo uwe unatambua wazi umefanya na mwathirika
Si kila mkidinyana..ndo mana nikasema baada ya kuwa exposed na HIV( mf:umefanya mapenzi na muathirika na ukagundua mapema kabla ya hizo siku tatu).[/QUOTE]

Mtu mwenye akili timamu hata akisikia tu yule ana ukimwi hawezi kumgusa, halafu mtu adinyane tena pekupeku huku akijipa matumaini ya kutumia PEP!!

Ukileta uzi humu halafu ukatae maswali kulingana na kile ulichosema nadhani hilo litakuwa tatizo lako.

Sidhani kama ningekuuliza maswali niliyokuuliza kama ungetoa ufafanuzi kama huu uliotoa kwenye rangi ya blue mwanzoni, lakini badala yake ukaanza kujibu kwa kejeli na kuniambia kwa dharau "another swali plz".

:A S thumbs_down::A S thumbs_down::A S thumbs_down::A S thumbs_down::A S thumbs_down::A S thumbs_down::A S thumbs_down:
 

Don't act a victim..ulikuja kubishana hapa sema labda ulikuwa hujajipanga vizuri...

Maswali mangapi yameulizwa na nimejibu??..nwei nafurahi umejishusha..[/QUOTE]
Mimi nijipange kwa hoja zako dhaifu mtu usiyejua hata ku-quote uzi wa mtu wewe, umevurugwa nini!. Yani ulipoona nimeamua kukuacha na dharau zako uliona nakuogopa sana umeona uendelee kunifuata fuata siyo? Endelea unachokitafuta utakipata muda si mrefu.

Angalia hapo juu unavyoandika hovyohovyo ndiyo uwe na hadhi ya kushindanishwa na mimi, umekopi na kupaste sehemu unatuletea humu hata kuandika vizuri hujui hayo maswali utaweza kuyajibu? Mburula wahedi....
 
grafani11 Wewe unauejua ku-quote ndo umefanya nn sasa..una-edit lakini still unakosea..naona umeanza kupiga beat hahahha!!..hizo beat wenzako wanafanya biashara we unazitoa bure.Nani huyo anayeshindanisha watu humu?? Naomba na mi nimjue
 
Last edited by a moderator:
rpg sio lazima iwe kwa watoa huduma za afya tu..kama ni kinga basi kila mtu anaweza kupatiwa

Unachosema ni kweli, nimeeleza pia kuwa watu wanaobakwa hupatiwa huduma hii! Huwa natamani kuduma hii itolewe kwa watu wanaopata ajari mbay, lakini siyo common practice kwa Tanzania!
 
Last edited by a moderator:
Unachosema ni kweli, nimeeleza pia kuwa watu wanaobakwa hupatiwa huduma hii! Huwa natamani kuduma hii itolewe kwa watu wanaopata ajari mbay, lakini siyo common practice kwa Tanzania!

Vipi Kwa hapa tz ,ma-nurse wanaopata virusi wakati wa kutoa huduma,wanapatiwa hii treatment???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…