Fahamu zaidi kuhusu kinga ya Ukimwi iitwayo PEP

Endelea kupoteza muda humu yakipita masaa 72 itakuwa mbaya zaidi PEP hazitolewi kiholela nenda hospital,
 
Nenda kituo cha afya
Ila zinamawenge balaa
Njaa inauma 24hrs
Tumbo kuuma
Kichefchefu
Homa
Na kuhalisha kwa baadh ya watu
 
Hakuna dawa inayoitwa "PEP" ila kuna huduma inayoitwa PEP.

PEP ni HUDUMA ambayo anapewa mtu yoyote yule ambaye amekumbwa na mazingira hatarishi yanayoweza kusababisha akapata maambukizi ya virusi vya UKIMWI. Huduma huwa ni sahihi mtu kupewa ndani ya masaa 72 tangu kupatwa na kadhia hiyo hapo juu.

Katika kupewa huduma ya PEP muhusika ataanzishiwa dozi ya kumeza vidonge vya kufubaza virusi vya UKIMWI (ARV) kulingana na muongozo husika wa kimatibabu wa nchi husika.

Dawa za kufubaza virusi vya UKIMWI (ARV) zipo tofauti tofauti na zinafanya kazi katika "mechanism" tofauti tofauti kulingana na dawa husika, mara nyingi dawa hizi huwa zipo katika combination mfano ni :

Dawa 2 za ARV zimewekwa katika kidonge kimoja au Dawa 3 za ARV zimewekwa katika kidonge kimoja..

Kwa muongozo uliopo sasa, mtu anayepewa huduma ya PEP atapewa vidonge vya ARV ambavyo ni kidonge kimoja chenye combination ya dawa tatu

TLE (Tenifovir + Lamivudine + Efavirenz)

Hiyo dawa ya miwsho EFAVIRENZ ndo huwa inaleta shida maana side effects zake ni kumfanya mtu kupata maruweruwe na ndoto za kutisha.

Kwa kuliona hilo asa hivi kuna combination mpya ambayo ni TLD

(Tenifovir + Lamivudine + Doultagvir)

Kuondolewa kwa Efavirenz imefanya asa hivi kumeza ARV kwaajili ya huduma ya PEP ni jambo la kuvumilika kidogo tofauti na hapo zamani.
 
[emoji106]
 

Umeshapata msaada Mkuu??
 
Oooh kumbe dawa zinazotumika ni ARVs!? Nilikuwa najua pengine kuna dawa kabisa zinazoitwa PEP
 

Dolutegravir
 
Mh pagumu hapa
 
Vizuri, elezea pia kuhusu PrEP na tofauti ilyopo kati ya PEP na PrEP
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…