Fahamu zaidi kuhusu la ugonjwa wa Vitiligo na tiba yake

Fahamu zaidi kuhusu la ugonjwa wa Vitiligo na tiba yake

Hii huwa kama inakukera ni kupaka makeup tu, ila haina tiba
 
Utapoteza garama nyingi sana mkuu, Ugonjwa huu hauna tiba aise. Hata Michael Jackson alikufa nao.
Sikukatishi tamaa jaribu kutafuta tiba mkuu.
 
Pole ndugu yangu. Usimsahau Yesu daktari bingwa aliyepo dunia nzima.
Sarakasi zako zinapoishia ye ndo atakapoanzia.
Kwa hiyo mueleze tatizo lako na dozi yake ni ya papo kwa hapo.
Nimeona wengi wakiponywa nae zaidi ya huo ugonjwa unaokusumbua.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
Anapatikana hospital gani na mkoa gani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu pole Sana mimi pia Nina vitiligo,imenisumbua Miaka karibia kumi Sasa... Nimeshaangaika Sana. Saiv nimeamua kumuachia Mungu... Ila kajaribu Dawa za kimasai.. pia Kuna Dawa hospital zinasaidia isiongezeke. Kamuone Dermatologist regency au muhimbili anaweza kukushauri zaidi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huu ugonjwa kuna maumivu yoyote ubayapata?
Mkuu pole Sana mimi pia Nina vitiligo,imenisumbua Miaka karibia kumi Sasa... Nimeshaangaika Sana. Saiv nimeamua kumuachia Mungu... Ila kajaribu Dawa za kimasai.. pia Kuna Dawa hospital zinasaidia isiongezeke. Kamuone Dermatologist regency au muhimbili anaweza kukushauri zaidi

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
WAPIGIE HAWA JAMAA WA KOREAN MEDICAL CLINIC WAPO KARIAKOO MTAA WA MAHIWA NA LIVINGSTONE KARIBU NA MSIKITI WA MTORO NI MA-SPECIALISTS KWENYE ISSUE HIYO, FUATILIA WEBSITE YAO NI: koreadermatologicalclinic.blogspot.com utakuta na mawasiliano yao hapo.

kila la heri
Huku nlishaenda...aisee wale hawana msaada kwa ugonjwa huu...wanakuonesha tu picha zawatu waliopona but hawasaidiii kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama unadhani mimi nafanya biashara ya kuuza dawa, kaa na ugonjwa wako. Unadhani watu niliowaandikia hiyo dawa wakapona walinipa hata shilling moja?

Huna haja ya kuniita tapeli. Ugonjwa wako, halafu unanitukana mimi niliykwisha kupona tena kwa sh. thelathini elf tu. Watu nakutana nao kwenye mikutano na vyombo vya usafiri nawaandikia dawa siwafahamu hawanifahamu. Halafu leo eti kune pm unaona nitakutapeli. Pole .
Dada mbona nakupm haiendi naomba number yako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii koment imemaliza kila kitu
Pole sana mkuu,

Sitaki kukukatisha tamaa ya kupona lakini ukweli ni kuwa vitiligo, (mabaka meupe mno) haitibiki. Ni miongoni mwa magonjwa ya auto immune, yaani kinga ya mwili inashambulia cells zinazoitwa melanocyte ambazo ndio zinazotengeneza rangi nyeusi tuliyonayo.

Shida hii ni kasoro ya kuzaliwa na inafata ukoo japo si kila mtu katika ukoo aweza pata. Shida hii inawapata watu wa rangi zote.

Na ajabu ni kuwa pamoja na kuwa wazungu ni weupe but akiwa na vitiligo huwa inaonekana wazi (very conspicious) Dawa nyingi zimejaribiwa but hakuna iliyoibuka tiba.

Baadhi ya watu wakitumia prednisolone au hydrocortisone ya kupaka waweza pata nafuu but ni baada ya muda mrefu.

Tiba ya uhakika ni kuikubali hali hiyo, na kuipuuza kwa sababu haiumi, wala haiwashi. Otherwise nimeona watu wakipoteza fedha nyingi na hawakupona.

Kama unaishi karibu na hospitali kubwa kama Muhimbili, KCMC, Bugando au Mbeya waweza pata ushauri wa Dermatologist.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah kuna watu hapa wanesema walipona kabisa lakini hawataki kutoa ushirikiano wa wazi mara njoo pm mara nitumie email yako watu bana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
1592741644585.png
Habari wanajukwa,

Kama nilivyoeleza hapo juu, Naomba msaada waushauri wa kitaalamu either wa tiba za asili au za kisasa juu ya tatizo la vitiglo kwa ambao wamesha experience na kujua japo ata kwa kuuthibiti usisambae zaidi au kupunguza.

Natanguliza shukrani
 
Ungeandika maelezo yake kidogo ni ugonjwa wa nini, dalili zake na madhara yake. Huenda kuna mitishamba ya kutibu ila jina ni tatizo ila kupitia dalili watu wakaugundua na ukawa na jina tofauti na hilo la kisomi.
 
Ungeandika maelezo yake kidogo ni ugonjwa wa nini, dalili zake na madhara yake. Huenda kuna mitishamba ya kutibu ila jina ni tatizo ila kupitia dalili watu wakaugundua na ukawa na jina tofauti na hilo la kisomi.
Vitiligo ni ugonjwa wa ngozi ambao unasababisha ngozi kuwa na mabaka mabaka meupe kwa sababu ya kupoteza melanin. Vitiligo inaathiri watu wa rangi yoyote ya ngozi japo kwa watu wengine huwa inaonekana zaidi kutokana na rangi yake ilivyo sanasana kwa watu wenye ngozi nyeusi. Pia inatokea katika umri wowote mara nyingi katika umri chini ya miaka 40.
download.jpg
 
Habari wanajukwa.
Kama nilivyoeleza hapo juu, Naomba msaada waushauri wa kitaalamu either wa tiba za asili au za kisasa juu ya tatizo la vitiglo kwa ambao wamesha experience na kujua japo ata kwa kuuthibiti usisambae zaidi au kupunguza. Natanguliza shukrani
Matibabu hutegemea na makubaliano ya mtu mwenye tatizo na daktari wake.

1. Dawa za kupakaa ili kusaidia kusaidia uzalishaji wa melanin.

2. Kuchora tattoo ili kuzuia kuonekana kwa sehemu zilizoathiriwa (skin camouflage).

3. Kupunguza melanin maeneo ambayo hayajaathiriwa ili kuleta ufanano na sehemu zilizoathiriwa (depigmentation).

4. Upasuaji pia hufanyika (skin grafting). Ukiwa na tatizo hili ni vizuri kumuona mtaalamu wa magonjwa ya ngozi (Dermatologist) ili uweze kusaidiwa pia ukiona dalili za tatizo hili inashauriwa kujilinda na jua na kutochora tattoo ambazo haujashauriwa na mtaalam wa magonjwa ya ngozi.
 
Ninaomba nipingane na wewe. Mimi nilikuwa na hili tatizo na nilipona kabisa. Anayetaka dawa ani pm nimwelekeze. Ni miaka mingi imepita lakini ninaimani kwa Mkono wa Mungu, bado ile dawa ipo.
Nakupataje mkuu kwa mawasiliano
 
Back
Top Bottom