Fahamu zaidi kuhusu la ugonjwa wa Vitiligo na tiba yake

Hii huwa kama inakukera ni kupaka makeup tu, ila haina tiba
 
Utapoteza garama nyingi sana mkuu, Ugonjwa huu hauna tiba aise. Hata Michael Jackson alikufa nao.
Sikukatishi tamaa jaribu kutafuta tiba mkuu.
 
Anapatikana hospital gani na mkoa gani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu pole Sana mimi pia Nina vitiligo,imenisumbua Miaka karibia kumi Sasa... Nimeshaangaika Sana. Saiv nimeamua kumuachia Mungu... Ila kajaribu Dawa za kimasai.. pia Kuna Dawa hospital zinasaidia isiongezeke. Kamuone Dermatologist regency au muhimbili anaweza kukushauri zaidi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huu ugonjwa kuna maumivu yoyote ubayapata?
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huku nlishaenda...aisee wale hawana msaada kwa ugonjwa huu...wanakuonesha tu picha zawatu waliopona but hawasaidiii kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dada mbona nakupm haiendi naomba number yako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii koment imemaliza kila kitu
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah kuna watu hapa wanesema walipona kabisa lakini hawataki kutoa ushirikiano wa wazi mara njoo pm mara nitumie email yako watu bana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari wanajukwa,

Kama nilivyoeleza hapo juu, Naomba msaada waushauri wa kitaalamu either wa tiba za asili au za kisasa juu ya tatizo la vitiglo kwa ambao wamesha experience na kujua japo ata kwa kuuthibiti usisambae zaidi au kupunguza.

Natanguliza shukrani
 
Ungeandika maelezo yake kidogo ni ugonjwa wa nini, dalili zake na madhara yake. Huenda kuna mitishamba ya kutibu ila jina ni tatizo ila kupitia dalili watu wakaugundua na ukawa na jina tofauti na hilo la kisomi.
 
Ungeandika maelezo yake kidogo ni ugonjwa wa nini, dalili zake na madhara yake. Huenda kuna mitishamba ya kutibu ila jina ni tatizo ila kupitia dalili watu wakaugundua na ukawa na jina tofauti na hilo la kisomi.
Vitiligo ni ugonjwa wa ngozi ambao unasababisha ngozi kuwa na mabaka mabaka meupe kwa sababu ya kupoteza melanin. Vitiligo inaathiri watu wa rangi yoyote ya ngozi japo kwa watu wengine huwa inaonekana zaidi kutokana na rangi yake ilivyo sanasana kwa watu wenye ngozi nyeusi. Pia inatokea katika umri wowote mara nyingi katika umri chini ya miaka 40.
 
Matibabu hutegemea na makubaliano ya mtu mwenye tatizo na daktari wake.

1. Dawa za kupakaa ili kusaidia kusaidia uzalishaji wa melanin.

2. Kuchora tattoo ili kuzuia kuonekana kwa sehemu zilizoathiriwa (skin camouflage).

3. Kupunguza melanin maeneo ambayo hayajaathiriwa ili kuleta ufanano na sehemu zilizoathiriwa (depigmentation).

4. Upasuaji pia hufanyika (skin grafting). Ukiwa na tatizo hili ni vizuri kumuona mtaalamu wa magonjwa ya ngozi (Dermatologist) ili uweze kusaidiwa pia ukiona dalili za tatizo hili inashauriwa kujilinda na jua na kutochora tattoo ambazo haujashauriwa na mtaalam wa magonjwa ya ngozi.
 
Ninaomba nipingane na wewe. Mimi nilikuwa na hili tatizo na nilipona kabisa. Anayetaka dawa ani pm nimwelekeze. Ni miaka mingi imepita lakini ninaimani kwa Mkono wa Mungu, bado ile dawa ipo.
Nakupataje mkuu kwa mawasiliano
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…