Fahamu zaidi kuhusu mafuta ya ndege

Fahamu zaidi kuhusu mafuta ya ndege

KING MIDAS

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2010
Posts
8,589
Reaction score
16,936
NDEGE HUTUMIA MAFUTA GANI?

Aviation Fuel ni mafuta yanayotumiwa kwa kuendeshea injini za ndege.
Kimsingi zipo kama aina nne za mafuta zinazotumika katika usafiri wa anga.
Mafuta ya ndege.jpg

1> Jet A-1 ambayo ambayo kwa uhalisia ni mafuta ya taa

2> Jet B, Mchanganyiko wa mafuta ya taa na petroli

3> Avgas ambayo ni kama petrol ya ndege.

4> Biokerosene ambayo ni mchanganyiko wa mafuta ya taa na mimea.

1> #JetA_1

Mafuta haya pia huitwa JP-1A hutumiwa ulimwenguni kote katika injini za turbine (injini zenye mfumo wa 'jet na turboprops')
Haya ni kama mafuta ya taa yaliyosafishwa kwa uangalifu ambayo yapo fanisi kuwaka kwenye joto la kiwango cha 38 °C na kiwango cha chini -47 °C.

Mafuta haya taa yanasafishwa kwa ustadi mkubwa sana na baada ya kusafishwa yanachanganywa na kiwango kadhaa cha viambatanishi vinavyo wezesha kuwaka katika hali iliyodhibitiwa, kuzuia viumbe kukua ndani yake kama fangasi, bakteria, pia kuzuia kuganda kwenye ubaridi wa -30°C n.k
Ndege za kijeshi mfano za NATO hutumia mafuta haya na viongezeo maalum zaidi na kuitwa jina la #Jet_Propellant_8 (JP-8).

2> #JetB

Mchanganyiko wa mafuta ya taa na petroli.
Mafuta haya hutumiwa sana katika ndege za kijeshi.
Mchanganyiko huu maalum wa daraja la Jet B, pia huitwa JP-4 ambapo Petroli asilimia 65% na Mafuta ya Taa asilimia35%.
Haya hutumiwa zaidi kwenye sehemu zenye ubaridi sana kwa sababu yanaweza kuwaka kwa joto la 20°C.
Lakini pia injini lazima ziwe zimeundwa maalum kwa matumizi ya mafuta haya.

3> #AvGas (Aviation Gasoline)

Hii ni kama Petroli maalum kwaajili ya ndege hasa zile zenye injini za piston.
Mafuta haya katika usafiri wa anga kawaida hutumiwa tu katika injini za Piston hasa ndege za michezo,ndege ndogo za kibinafsi ambazo zinahitaji mafuta ya kuongezwa kiasi kikubwa cha octane.

Kwahiyo Avgas ni kama petroli iliyoongozwa octane 100 ili kukidhi mahitaji haya.
Hapa Ulimwenguni ni aina ya #Avgas100LL tu ambayo bado inapatikana kirahisi na ndege zilizo na injini ya petroli tu ndiyo zinaweza kuendeshwa na avgas, ndege zinazotumia turbine au zile zilizo na injini za mfumo wa kerosene/dizeli zinahitaji jetA.

Kwa kuwa avgas ni ghali kutokana na kiwango cha chini cha uzalishaji, njia ndefu za usambazaji, na udhibiti wa ubora.

4> #Biokerosene

Biokerosene mchanganyiko wa mafuta ya taa na nishati ya mimea ambayo imeanza kutumiwa na tasnia ya usafiri wa anga.

Tafsiri kutoka mitandaoni.
 
nilisikia korosho zinatoa mafuta ya ndege sasa sijui ndio yapi katika hayo......vipi kuhusu vyombo vya angani mf roket nk
 
Jet A1 Blue color, ni mepesi Sanaa kuliko hata petrol hivyo huwa tuna mix na grease au hata Oil

It's very flammable

Wale wa Block C Airports wanielewa
 
Kwa mchanganuo wako wa michanganyo minne uliitaja.Basi kumbe asilimia kubwa ndege hutumia mafuta ya taa.
 
Back
Top Bottom