Fahamu zaidi kuhusu Mr Kuku

Carly ulikuwa ugeuzwe fursa mwalimu wangu, umechomokea kwenye mdomo wa mamba..
Mr. Kuku afikishwa Mahakamani akikabiliwa na mashtaka saba ikiwemo kufanya Biashara Haramu ya Upatu
Says S.O.T your student.. 🤣
 
1.Uwepo wa wafanyabiashara wengine wanaofanya UPATU sio justification ya anachofanya mr kuku

2.Kukusanya mtaji kwa umma lazima uwe na kibali cha benki kuu na mamlaka ya mitaji na masoko na IJULIKANE UNAKUSANYA KIASI GANI KWA LENGO GANI KIASI HICHO KIKITIMIA KAMA ULIVYOAINISHA KWENYE PROPOSAL BASI ZOEZI LINASITISHWA....Hapa ndipo tatizo linapoanzia

3.Huyu Mr Kuku alikuwa ndo anaanza kuwekeza... kununua eneo,kujenga mabanda,....kama sehemu ya mtaji unawekwa huko maane yake RETURN yake sio ya miezi 3

4.Kuna vigezo vinahitajika kufikiwa kwa kampuni ili iweze kuruhusiwa kukusanya mtaji kwa umma sio start up

5.Mimi nafuga NAWAMBIA UKWELI HUWEZI KUPATA FAIDA YA 70% KWA MIEZI 3 HAPA NDIPO UPATU ULIPO....AJABU MR KUKU ALIKUWA ANATOA GAWIO LA 70% NA KUBAKIA NA FAIDA YAKE KWAHIYO LABDA ALIKUWA ANAPATA 100% ANATOA 70% KWA MWEKEZAJI ANABAKI NA 30%

Dada yangu alitaka kuwekeza aliponitafuta nilimzuia kwa kumpa FACT leo amenishukuru.
 
UPATU maana yake rahisi ni kuwa mr kuku hakuwa anatoa GAWIO kupitia faida za kuendesha mradi bali ni makusanyo ya wawekezaji wapya yanatumika kulipa wawekezaji wa zamani.

Yaani muda wote anakusanya mtaji hakuna deadline, no target....

Hata kwenye bond mwaka jana tumeona NMB walikusanya mtaji kwa njia ya bond kutoka kwa wawekezaji...time frame miaka 3 faida baada ya kutoa kodi kwa milioni 50 wanatoa milioni 13.2 kwa miaka 3.

Nmb waliruhusiwa kuuza bond wakilenga kukusanya bilioni 300 I think....Ndio ni muhimu ijulikane unalenga kukusanya kiasi gani na BOT waliwapa Nmb time frame ya lini mwisho wa kununua bond na target ya amount.

Kwahiyo kwa 50m kwa mr kuku ndani ya miezi 3 anakupa 35m huu ni utapeli usiohitaji degree wala elimu hata ya cheti tu kujua unaibiwa.

Wawekezaji mliambiwa bei gani ilikuwa inahitajika au mkiambiwa kuna kuku 280,000 mnapagwa mnaweka hela[emoji23]Poleni.Amekuasanya bilioni 17 ana kuku broiler 280,000 na mnasema alikuwa anauza broiler 1 sh 4500 maana yake kuku wote 280,000 ni bilioni 1.2 na yeye amekusanya bilioni 17 hao wawekezaji wengine ATAWALIPAJE?


Kwa mfumo wa serikali hapo mmeumia hela zimeenda hizo zilizotumika na hata zilizopo benki no gawio[emoji91]
 
Huyu ni tapeli,si ndio huyuhuyu aliwapiga hela watu katika mradi wake wa kukopesha kupitia mtandao wa L-PESA?
 
Tatizo watanzania tunapenda vitonga sanaaaaa,,, Yaani tunataka kuingiza pesa tukiwa ghetto tumelala
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]nimekumbuka mwanangu jrn anaingiza pesa kalala yani anawapiga watu hatari na wanatyma kwa ushawishi tu wa maneno
 
We mbona ulikuwaga unamtetea Sana inaonekana mko kundi moja so unajifanya kutokea nyuma ya keyboard ili kuwaaminisha watu. Pumba..... Sana.
 
We mbona ulikuwaga unamtetea Sana inaonekana mko kundi moja so unajifanya kutokea nyuma ya keyboard ili kuwaaminisha watu. Pumba..... Sana.
Kwahio tunatakiwa wote tumkosoe?

Usiwe kama Nyumbu, tumia akili yako uelewe na sio kufata tu mkumbo.
 
Kwahio Kuku alokua akifuga alikua anakula na familia yake? Ungekua kweli una ufahamu ningekuelewa kama ungesema cash flow yake ya mauzo ya Kuku hayakulingana na matarajio ya wawekezaji. Unaiweka kama vile hakua na project yoyote ya kutengeza hela. Acheni uzushi, fatilieni muelewe.

Na hizo hesabu zako ni za kitoto sana. Hio bilioni 17 ni lugha tu ya kimahamaka, una uelewa mdogo. DPP anavuta statement yako yote na kuhesabu all the CREDITS bila kujali kuna Debit zilipita. Na hata kama kweli watu wamewekeza Bilioni17, kwani wote waliwekeza siku moja?

Shule muhimu hapa
 
Tatizo ni hesabu.....

Upate 100% kwenye kuku ndani ya miezi 3....Huu ni wendawazimu hapa ndipo upatu ulipo Huyo hakuwa anawalipa wateja wake kwa mauzo ya kuku stop that rubbish.

Halafu crowd funding/capital raising lazima uwe na business proposal.....mf mr kuku alikuwa anahitaji bilioni 5 kwa project yake ya kuku milioni moja basi ilibidi aweke hizo details public....sio ishu ya njoo ofisini hapana as long as unakusanya mtaji kwa umma maana yake lazima uweke details za mtaji hitajika ukishafikiwa unafunga zoezi la kukusanya mtaji.

Ajabu ni kuwa mr kuku yeye anakusanyaga mtaji full time. UPATU UPATU.

Tufanye hesabu ya Miezi 3 kwa broiler kwa mtu aliwekeza laki 7 (kuku100 anavyodai mr kuku).

Miezi 3 maana yake akifuga kwa wiki 4 atauza batch 3.

Tu assume everything is okay

Faida ya kila kuku tufanye ni elfu 2 (kwa broiler hi ni faida ya juu sana kama umewahi kufuga UTAELEWA HILI.

Kuku 100 x 2000(faida) x 3(miezi 3 ya gawio linapotolewa) unapata laki 6.

GAWIO anatoa laki 7 wakati amepata laki 6...kumbuka hiyo laki 6 hazitoshi hata gawio la mwekezaji bado yeye hajapata kitu hapo.

UJINGA NI MZIGO MZITO
 
Kuna clip moja ilisambaa sana jamaa aliweka milioni 7 akapata 14 baada ya miezi 3 akawekeza tena miezi 3 akapata milioni 26 akawekeza tena hiyo 26m akawa anatarajia kupata 52m baada ya miezi 3.

HESABU NDO TATIZO LETU WABONGO[emoji23]

YAANI 7M NDANI YA MIEZI 9 IMEFIKA 52M

Kuna mama mmoja anasaga meno aliweka milioni 50 alikuwa anatarajia kupata milioni 100 baada ya miezi 3. Alipoambiwa ukweli kama ulivyo UJINGA hauchagui umri akapuuzia akaweka pesa.
 
Unapotosha.. ni return ya 100% ni kwa wawekezaji wa miezi 6 na 70% kwa miezi minne.
 
Unapotosha.. ni return ya 100% ni kwa wawekezaji wa miezi 6 na 70% kwa miezi minne.
Nashukuru kwa hayo marekebisho ila Hata ww bado hujaiweka sawa 100% ni miezi 4 sio miezi 6.

Kwahiyo ukiweka 50m ndani ya miezi 4 unapata 50[emoji23]unakuwa na 100m unaweka 100m miezi 4 unapata 200m then unaweka milioni 200 miezi 4 ya mwisho una 400m (ndani ya mwaka tu [emoji23]).

Kwa 50m ndani ya miezi 12 una 400m
Return 100% kila miezi 4.

Haya fanya hiyo hesabu ya broiler kwa miezi 4 yako uone utapata nini. Na nimekupa super profit 2000 kwa kila kuku + everything is okay.

Wakati huo mnasema alikuwa anauza kuku bei cheap tu [emoji848]mnajitekenya na kucheka wenyewe yaani kuku bei cheap halafu return kubwa [emoji1787]

Milioni 7 hadi milioni 52 kwa mwaka. Mimi ni mfugaji nasema ninachokifanya kila siku naijua hii industry.

UJINGA NI MZIGO MZITO.
 
Wewe unawachoma hao wengine. [emoji16][emoji16][emoji16]..
Lakini hyo ni biashara gani ambayo HAINA HASARA?
Sent from my SM-G928F using JamiiForums mobile app
 
Hio zamani, mwaka jana
 
kuna watu wamelalamika kuwa hawapi hilo gawio afu kisheria hairuhusiwi kukusanya hela kwa watu kwa style hiyo

Kama kweli anaugakika huo kwanini asifanye kama yule dada mzungu wa kichaga nae anafuga kuku wengi zaidi ya laki 2 na hakusanyi hela kwa watu
 
Hapo kuku bado hawajafa.,na vipi kuhusu masikini alikuwa nalo la uhakika?.
Sent from my SM-G928F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…