Sivan
JF-Expert Member
- Jul 17, 2020
- 923
- 1,228
Mkuu up
upo sahihi na umepiga hesabu vizuri kweli, napenda kujua Hoja yako (mzizi) hoja yako au main point.Tatizo ni hesabu.....
Upate 100% kwenye kuku ndani ya miezi 3....Huu ni wendawazimu hapa ndipo upatu ulipo Huyo hakuwa anawalipa wateja wake kwa mauzo ya kuku stop that rubbish.
Halafu crowd funding/capital raising lazima uwe na business proposal.....mf mr kuku alikuwa anahitaji bilioni 5 kwa project yake ya kuku milioni moja basi ilibidi aweke hizo details public....sio ishu ya njoo ofisini hapana as long as unakusanya mtaji kwa umma maana yake lazima uweke details za mtaji hitajika ukishafikiwa unafunga zoezi la kukusanya mtaji.
Ajabu ni kuwa mr kuku yeye anakusanyaga mtaji full time. UPATU UPATU.
Tufanye hesabu ya Miezi 3 kwa broiler kwa mtu aliwekeza laki 7 (kuku100 anavyodai mr kuku).
Miezi 3 maana yake akifuga kwa wiki 4 atauza batch 3.
Tu assume everything is okay
Faida ya kila kuku tufanye ni elfu 2 (kwa broiler hi ni faida ya juu sana kama umewahi kufuga UTAELEWA HILI.
Kuku 100 x 2000(faida) x 3(miezi 3 ya gawio linapotolewa) unapata laki 6.
GAWIO anatoa laki 7 wakati amepata laki 6...kumbuka hiyo laki 6 hazitoshi hata gawio la mwekezaji bado yeye hajapata kitu hapo.
UJINGA NI MZIGO MZITO