Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Definition of Risk TakersHoja kama hizi utawadanganya nazo hao wajinga wajinga wanaowaletea ninyi fedha zao na siyo mimi! Maisha yangekuwa rahisi namna hii mnayodanganya hii dunia isingekuwa na maskini. Ni suala la muda tu lakini ukweli utajulikana na wajinga wanaowapa fedha zao watabaki wanalia na kuomboleza.
Did you think that I dont know the meaning of risk taker! I do dude! BTW the difference between lazy, fools who embrace imposibles and risk takers is bigger that our universal. Those who are investing their money in the Kuku project are fools.Definition of Risk Takers
Certain types of people enjoy taking risks, while others prefer stability and are averse to any type of risk. A risk taker is someone who risks everything in the hope of achievement......
Kusikia Kwa Kenge Hadi Atoke Damu Puani Na MasikioniKenge kusikia.................... . ...
Janjajanja Primary School Imefaurisha Wanafunzi Wote Lakini Hawajui Kusoma Na KuandikaWameshapigwa Pini hawa jamaa
Vipi hatima ya hawa jamaa na wateja wao imeshajulikana?Wameshapigwa Pini hawa jamaa
Haaaa mm nilishajua mda sana kuna dalili za Utapeli ndani yake.Habari wana chamvi, nimesoma uzi kuhusu mada tajwa hapo juu nami nataka kushirikishana uzoefu wangu kuhusu huyo 'mwekezaji".
Huyo bwana anaitwa Tariq, mwaka juzi 2018 nilisoma bandiko lake fb kuhusu mradi wa kilimo cha nyanya cha umwagiliaji, ahadi ilikuwa nzuri kuhusu faidi ambapo kiwango cha chini cha hisa ilikuwa 36 na kila hisa 5000/= hivyo unapata 180,000 /=
Baada ya miezi mitatu unapata 360,000/= nilitamani kuwekeza japo nilikuwa na shaka, niliongea nae akanielewesha kwamba uwekezaji ni kupitia vikundi vya watu 15, hivyo akaniunganisha na wadau tukawa na kikundi cha What App tulikuwa mikoa tofauti ila mm niliiona na advantage kwa kuwa mradi ungefanyika jirani.
Tukaanza taratibu za katiba usajili wa kikundi, kabla ya kusajili kikundi akasema tutume fedha ili mradi uanze kuendana na wakati ili kuwahi soko la nyanya.
Baada ya kutoa fedha tulipitia ubabaishaji mwingi sana, mara mradi wa arusha hauwezekani kuna shamba moro, wadau wakataka kwenda moro baada ya muda akasema kule eneo linapitiwa na reli mradi utakuwa Tanga akatutumia vi picha vya eneo na ka tank. Wadau wakalazimisha wakaenda Tanga kufika hakuna kinachendelea.
Tukaanza harakati za kukamilisha katiba na mkataba ili tujipange kwa hatua zaidi. Baada ya muda sana akasema amepata hasara hivyo fedha iliyobaki atawekeza mradi wa kuku uliopa kigamboni. Tukaendelea kupambana na kufuatilia.
Baada ya mwaka baada ya kuwa na maamuzi ya kwenda vgombo vya sheria ndo akaturudishia mitaji yetu na kuahidi faida baada ya muda. Baada tu ya kurudisha mitaji hakuwa anapokea simu wala kujibu hoja za group la What App ambalo tulianzisha. Baada ya kuanza tena harakati za kutaka kufuatilia faida akatoka katika kundi kwa jazba na kusema tufanye tunavyotaka hayupo tayari kuendelea na sisi.
Kama ambavyo mmeona tangazo lake ndivyo alivyo huwa hajibu wala kutoa ufafanuzi wa kina kuhusu hoja.
Pamoja na kwamba uoga wako ndo umaskini wako ila kwa wawekezaji wa kibongo bora kuwa mwoga. "invest on your own risk"
Nawatakia wakati mwema.
Na ndo hyo inafyekelea vichwa vya watu mbaliTatizo watanzania tunapenda vitonga sanaaaaa,,, Yaani tunataka kuingiza pesa tukiwa ghetto tumelala
Jamaa anaidea nzur sana hasaa kma ataamua kuliboresha wazo lake. Au kma atatokea mtu mwenye mtaji mkubwa ambae hana nia ya kufanya utapeli akaamua kufanya hyo kitu.
Unaweza kujiuliza kitu simple kabis kama ikiwa anayo hio plani ya biashara inayoweza kukupa return on investment ya 100% kwa miez 3 yaani 180000 ikupe 360000, kwanin asiende bank kuchukua mkopo ili afinance hio biashara yake manake bank watamchaji riba ambayo haitafika 20% kwamwaka?? Jibu nikua hawez kwenda kuitapeli bank
Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
"hawez kwenda kuitapeli bank"
😂😂 Tuishi hapo. Kaangalia mnyonge wake nani.Kaka [emoji3][emoji3]..