Fahamu zaidi kuhusu Mr Kuku

Mkuu up
upo sahihi na umepiga hesabu vizuri kweli, napenda kujua Hoja yako (mzizi) hoja yako au main point.
 
Vimoradi miradi hivi vya sungura mara sijui samaki mara kuku mara nyanya huwa siviamini, ni bora ifanye mwenyewe at your own pace na kujijengea uwezo taratibu, asije mtu akaja kukupa plan ya kuingiza hela haraka haraka, ni utapeli tu
Maana wajinga ni wengi wanazaliwa kila leo mkuu
Alafu Hao wajinga WAKIAMBIWA ukweli Wanakuwa wakali kama MBOGO [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 
Ni miezi sita mkuu nilisaau hiki.
 
Na
Napenda kujua hoja yako, point kuu.
 
Kumbe Jamaa ni Tapeli tu kama kina Ontario ilikuwaje akaaminika na wakulungwa? Au alitumia Ndumba na Ngaye?
Siyo ndumba alitumia mfumo wa maisha yetu hakuna taarifa za kutosha kuhusu uwekezaji na wawekezaji wadogo, kati na wakubwa. Hata watoa vibali nao hawapo makini kujua hali za baadhi ya hao wawekezaji, kwa hiyo wanakua na uwezo wa kushawishi na hatimae kujipagia fedha kwa ulaghai. Na zaidi wengi kupenda mkato kufikia mafanikio
 

Subiri zamu yako, ni suala la muda tu!
 
Sasa aliwatapeli vipi na miradi ilikua inaendelea na watu walikua wanapata hela zao kama kawaida?
 
Mjini pesa ipo nyingi sana kwenye mifuko ya wajinga sema tu hatujajua jinsi ya kuzibeba na kutokomeza umaskini, saivi Ontario twitter anatoa laki laki subili bomu litakalo pigwa hamtoamini zaidi ya M500
 
Licha ya kuwa kinyume na Sheria,Nani mwenye uhakika kuwa anapata faida?anaandaa hesabu?anakuwa regulated na Nani? Alichokifanya jamaa ni kama public listing (kuuza share) amabyo Ina Sheria zake na miongozo.kama anapata hasara then ni upatu maana anawapa pesa watu wa zamani kwa kutumia hela za hawa wapya na hata kama anapata faida Nani anayejua,nimeamini watanzania bado ni rahisi Sana kuibiwa tena wasomi
 
Share maana yake unakubali kupokea faida/hasara kwasababu na ww ni sehemu ya mmliki wa kampuni.

Share maana yake GAWIO sio fixed....sio uweke 7m kwa mwaka upewe 52m kama kampuni haikupata faida unadai gawio kutoka wapi.

Kampuni ina HISA ngapi zina thamani gani

Kwani lengo ilikuwa kukusanya sh ngapi au mtaji kiasi gani au ni ukusanyaji endelevu wa pesa kutoka kwa wawekezaji wapya?

Jamaa alichokuwa anakifanya kibiashara HAKIWEZEKANI HESABU ZINAKATAA.


KUHUSU ALIWEZAJE KUWALIPA WADAU.

TUMEONA ILE VIDEO MOJA YA SHUHUDA WA 7M KUWA ALILIPWA 14M AKAWEKEZA TENA AKALIPWA AKAWEKEZA TENA AKAWA ANASUBIRIA KULIPWA.


Maelezo haya yanaibua maswali kwamba je huu ndo ulipwaji unaongelewa kuwa "amelipwa akawekeza tena so pesa yake haikutoka kwenye mzunguko"

Angefanya kwa mfumo wa HISA ingekuwa easy tu kwamba mwekezaji apewe faida MTAJI ubaki ukilipa faida na mtaji how will you run the business? Je hii ndo sababu ambayo ilimfanya akusanye pesa kila siku?

KWASASA TUFUATILIE KESI MAANA ANA MAKOSA SABA.

HESABU ZINAKATAA BUSINESS MODEL YAKE ILA ANA NAFASI YA KUJITETEA MAHAKAMANI.
 
Mkuu up

upo sahihi na umepiga hesabu vizuri kweli, napenda kujua Hoja yako (mzizi) hoja yako au main point.
Hakuna biashara ya hivyo ndugu yangu...ww nikikupa 7m as running capital plus infrastructure hutaweza kutengeneza hiyo faida ya 49m kwa mwaka. Tuanzie hapo.

1.Je alikuwa anawalipa wawekezaji?

2.Kama ndiyo, Je aliwezaje kuwalipa hao watu kwa mfumo ambao haupo?

3. Je ni pesa ya kuku kama alivyodai ?

Kwa maoni yangu kama kweli (mind you nimeona testimonial moja tu YouTube ya mtu aliyelipwa) Kama kweli alikuwa anawalipa wawekezaji basi alitumia pesa za wawekezaji wapya kulipa wa zamani. Usiniulize kuhusu kuku wale waliokuwa wanafugwa, faida yake kamwe haiwezi kuwalipa wawekezaji NEVER EVER. NI MAKUSANYO MAPYA KULIPA WAWEKEZAJI WA ZAMANI.

JE KUNA TATIZO KATIKA MFUMO HUU SERIKALI SI WANGEMUACHA AENDELEE KUKUSANYA HELA KWA WATEJA WAPYA KULIPA WAWEKEZAJI WA ZAMANI? WEWE UNAONAJE?
 
Unajua hesabu

Chukua 18 Billion gawanya miaka mitatu aliyo oparate Mrkuku ambzo ni siku 360×3 then uoate Figure kwasiku alikuwa anakusanya kihasi gani then uwangalie kuana uharisia...there is extra thing than upatu.
Hoja yangu haijajikita kwenye makusanyo sana sana nimejielekeza kwenye biashara aliyokuwa anafanya.

Mm na ww hatujui makusanyo ya bilioni 17 yamegawanyikaje kwasababu tunaweza kuigawa sawasawa tusiwe sahihi.

Ukiangalia Hesabu zangu utaona naangalia sana namna ya kuzalisha faida ili yeye abaki na chake na amlipe muwekezaji.

Na mimi nipo Open minded kujifunza kutoka kwa huyu jamaa [emoji120]
 
Mtu ulipiga hesabu vizuri kihasi kile sikutegemea utoe hoja hiyo ya waliotoa mwanzo wanapewa pesa ya wataotoa baadae...umeahinda kuona kama ili lifanikiwe kihasabu mmiliki wa mradi hatopata faida na itambidi atoe pesa yake ya mfukoni kuwalipa Once mtu akitoa 700K alipwe 1.4M je sichizi huyo.

Okey, Kilichonifanya niww interested na hoja yako ni kuchunguza na kupiga mahesabu ya kampuni ili upate conclusion kwamba inawezekanaje hii inamuhusu nini client ikiwa flow ya malipo yao hakuna aliye tapeliwa ndani ya miaka yote minne.

What i strictly Mrkuku hakutaperi wewe shilingi 300 yako there is million Dollar Mind behind it you need to know.
 
Kwanink unaBase sana na mahesabu ya yeye kupata chake, chake yeye atajua anapata wapi na anapataje Our minding Business ni Clients wanapata huduma iliyotangazwa kwa 100% Yes nini kujipa jukumu la CIA ikiwa raia wanaweka mizigo na kupewa double.
 
Huyu ndugu si anatafutwa na polisi au alishakamatwa?
 
Mkuu huna hoja yoyote unayotetea client walikuwa wanalipwa wakati huna hata uhakika na hoja yako.... Mm nimetizama hesabu maana ndio zipo public.


Kupitia Hesabu nimeona kuna ulaghai, siwezi kukaa kimya. Nimeikataa business model before hajakamatwa mr kuku na hata sasa NAIKATAA

Kwasasa tukutane Kisutu kila kitu kitajulikana.
 
Upo sahihi kabisa,inabidi kujiuliza maswali ya msingi Sana Kuna watu wamesoma uhasibu tena na Masters wanazo na wamepigwa hapa kilaini,ni maajabu mtu akupe guarantee ya faida ya kiasi hicho,wakati huo huo hakuna regulator
 
Jamaa unachekesha Business model like biashara ndio inaenda kufanyika...unachofanya wewe unachambua idea na mchakato mzima wa biashara ambao uchambuzi huo uliitajika uufanye kabla ya biashara ijaanza kuOperate sasa biashara isha Operate miaka minne hizo calculation zanini huu muda wa kuView je Model iliwapa watu kama ilivyosema au hapana.

Sasa unafanya uchambuzi aiseee maisha hayaa.
 
Upo sahihi kabisa,inabidi kujiuliza maswali ya msingi Sana Kuna watu wamesoma uhasibu tena na Masters wanazo na wamepigwa hapa kilaini,ni maajabu mtu akupe guarantee ya faida ya kiasi hicho,wakati huo huo hakuna regulator
Watu wamepigwa vipi ??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…