Fahamu zaidi kuhusu Mr Kuku

Upo sahihi kabisa,inabidi kujiuliza maswali ya msingi Sana Kuna watu wamesoma uhasibu tena na Masters wanazo na wamepigwa hapa kilaini,ni maajabu mtu akupe guarantee ya faida ya kiasi hicho,wakati huo huo hakuna regulator
Tamaa hufifisha uwezo wa AKILI

Kuna sehemu nyingi za kuwekeza jiulize why kwa mr kuku jibu ni return kubwa [emoji1787] hapo utajua tamaa mbaya yaani msomi anaweka elimu yake pembeni hahoji kitu anapagawa na return.

Mabenki hawatoi hiyo 100% kwa miezi 6 ndio maana wadau walikimbilia kwa mr kuku.

Mr Kuku nilimsikia mwaka jana dada yangu alipotaka kuwekeza alinitafuta kwa ajili ya ushauri. Nilimkatalia.

Sijawahi kuikubali hii model na siikubali....Mimi nafuga najua ninachosema. Huwezi kunidanganya kwa hoja nyepesi TUENDE TUKAONE KUKU /SHAMBA [emoji1787][emoji91]

SHAMBA LIKIWEPO NA KUKU WAKIWEPO HAWA JUSTIFY HIYO 7M KWA 52M KWA MWAKA.
 
Kwanink unaBase sana na mahesabu ya yeye kupata chake, chake yeye atajua anapata wapi na anapataje Our minding Business ni Clients wanapata huduma iliyotangazwa kwa 100% Yes nini kujipa jukumu la CIA ikiwa raia wanaweka mizigo na kupewa double.
Sasa ndugu hapa ndio nakushangaa,Mr kuku yeye angetoa wapi hela ya ziada just in case anapata hasara?zaidi ya kutumia fedha za wanachama wapya kulipa wa zamani?na swala la kulipa double ni la muda tu,kwa sababu Sasa hivi watu bado walikuwa wanaingia kwa wingi hivyo anapata pesa za kulipa wale wa zamani ila kadri jinsi ambavyo watu wangepungua kuwekeza au kuacha kabisa kwa sababu yoyote Ile basi shida kubwa ingekuwa hapo, unahitaji darasa kidogo la hichi kitu, ndio maana huu utapeli uliitwa pyramid upo miaka mingi kwa nchi za wenzetu,kuku wametumika tu hapa kama cover
 
Mr. Kuku
Amewapiga Kuanzia Wasiojua Kusoma Mpaka Wanaojua Kusoma, Darasa La Awali Mpaka Ph'D
Kwenye Fursa Ujue Wewe Mwenyewe Ndiyo Fursa
 
Upo sahihi kabisa,inabidi kujiuliza maswali ya msingi Sana Kuna watu wamesoma uhasibu tena na Masters wanazo na wamepigwa hapa kilaini,ni maajabu mtu akupe guarantee ya faida ya kiasi hicho,wakati huo huo hakuna regulator
Forex tulijionea hapa watu walipigwa wakahifadhi maumivu ila baada ya muda walifunguka ukweli wa moyoni [emoji23]hata hili halina muda waliopigwa watajitokeza tu

Yaani investment kubwa kama hii tuwe na ushuhuda mmoja tu wa mtu aliyelipwa wakati waliowekeza walikuwa zaidi ya 500+

Mr Kuku anaahidi kuwalipa watu huku anajenga mabanda,anajenga kiwanda cha chakula,anafungua ofisi.....watu kweli wanaelewa biashara.[emoji23]

Faida ya kiwanda itarudi leo au kesho....huo mtaji uliowekwa hapo unamlipaje mwekezaji mwenye hela uliyoitumia huko.

Wamejenga mabanda and other cost.


Hii biashara bila kujalisha ameanza lini ILIKUWA KWENYE NGAZI YA UWEKEZAJI HAIJA MATERIALIZE KUTOA FAIDA.
 
Nimetoa Hesabu huko juu ili watu waelewe why ni PYRAMID ila watu hawaelewi tu kitu chepesi kama hicho.

Achana na makosa ya kisheria ,sijui kodi,.... bado hiyo faida haiwezekani.

Tuna kazi kubwa na wasomi wa kisasa, mtu anauliza Je kama alikuwa anatoa hela yake mfukoni kuwalipa wawekezaji? Kama watu wanalipwa kwa hela za wawekezaji wapya shida nini [emoji38]
 
Mkuu upo sahihi jaribu kufikili basi mfuml uwo unaousema wewe hauwezi chukua muda ku Collapse mfano intake ya kwanza wametokea wawekezaji 10 kilammoja 1M sawa na wameweka 10M sasa intake inayokuja wakija tena 10 wote wamewekeza 1M sawa na 10 iyo pesa haitoshi kuwalipa intake ya kwanza maana wanahitaji 20M sasa 10M anaitoa wapi So kila muda unavypkwenda hii 10M i azidpigia miaka minne kwahiyo hili lingewezeka a indapo tu mtu atayelipa hatoitaji kulipwa double.

Unajaribu kulazimisha kuwa uwo mfumo utaCollapse endapo wawekezaji watapungua sio kweli uwo mfumo una Collapse hata flow iwe ileile kisa ila DOUBLE ni kubwa i atosha kulipua mfumo ndani ya intake za mwaka mmona tu try to brainstorm.

Okey tuache huko, Inahitaji ubongo kuelewa hoja zangu minajaribu kukuonesha mfumo ume oparate vizuri ndani ya miaka mitatu unachohitaji kujua ni nini kilicho mpeleka mahakamani full stopo ila kusema kupigwa nani kapigwa kupigwa wanaweza kuwa wamepiga ila sio vilakilaki vya raia mkuu kuna sehemu tofauti iliyopogwa...mfuml ungekuwa una oparate hata miaka 30 mbele still watu wangepata return zao bila tatizo.
 
Kuna watu wanauliza yeye anapata nn sio swali la muhimu....

Iko hivi yeye amebeba RISK 100% kwa maana hiyo ATAWALIPA WAWEKEZAJI NO MATTER WHAT

Sasa umeweka 7m baada ya Miezi 4 akakupa 14m..

Initial investment 7m

Faida 7m

Swali la yeye anapata nn linaanzia hapo kwenye hilo Gawio ulilopewa...

Mfano....Kabla ya kuamua kiwango cha gawio naamin walifanya profit projection ndipo wakaamua investors wapewe 100% miezi 4 na wao waliobeba dhamana labda wapate 100% ( win to win situation).

Profit projection [emoji91]
 
Hapo bado hujafanya analysis vizuri. Kuna gharama hujaziweka kuanzia na ununuzi wa vifaranga, chakula, madawa, mishahara, etc.
Ukichukuwa hayo ni dhahiri huwezi hata nusu ya anachoahidi.
Hii ni upatu at the best.
wajinga ndio waliwao.
 
Hu
Hujaeleweka ujajijibu swali wanapata nini wao hata sijaelewa ulivyouliza.
 
Hapo bado hujafanya analysis vizuri. Kuna gharama hujaziweka kuanzia na ununuzi wa vifaranga, chakula, madawa, mishahara, etc.
Ukichukuwa hayo ni dhahiri huwezi hata nusu ya anachoahidi.
Hii ni upatu at the best.
wajinga ndio waliwao.
Mfanyabiashra na Mkazi wa Oysterbay jijini Dar es Salaam, Tariq Machibya miaka (29) maarufu kama Mr Kuku, akiwa kortini Kisutu kusubiria kusomewa kesi inayomkabili.

Mfanyabiashra na Mkazi wa Oysterbay jijini Dar es Salaam, Tariq Machibya miaka (29) maarufu Mr Kuku, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi.

Mshtakiwa amesomewa mashtaka yake leo Agosti 10,2020 na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon, mbele ya Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Godfrey Isaya.

Akisoma hati ya mashtaka, Wakili Wankyo amedai mshtakiwa anakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi namba 60/2020 ambapo katika mashtaka hayo saba yanayomkabili mshtakiwa huyo, yapo ya kusimamia na kuendesha biashara haramu ya upatu; kupokea maingizo ya fedha kutoka kwa umma bila kuwa na leseni na mashtaka matano ni kutakatisha fedha.

Miongoni mwa mashtaka hayo ni kati ya Januari 2018 na Mei 2020, katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar Es Salaam, mshtakiwa anadaiwa kusimamia biashara ya upatu.

Pia anadaiwa kujihusisha na biashara ya upatu kwa kukubali na kukusanya fedha kutoka kwa umma, akijifanya kwamba watafanya ujasiliamali wa ufugaji wa kuku na wangepata faida ya asilimia 70 ya mtaji wa awali waliowekeza kwa miezi minne na asilimia 90 ya mtaji wa awali waliowekeza kwa kipindi cha miezi sita, kiasi ambacho ni kikubwa katika biashara kuliko mtaji uliokusanywa.

Wankyo amedai kati ya April 26, 2019 na Januari 26, 2020 maeneo ya Jiji la Dar Es Salaam, alijihusisha na miamala ya Sh 6.4bilioni kwa kutoa fedha hizo kutoka katika akaunti inayosomeka kwa jina la Mr Kuku Farmers Ltd iliyopo katika benki ya CRDB, wakati akijua kuwa fedha hizo ni zao tangulizi la biashara haramu ya upatu.

Upande wa mashtaka umedai kuwa kesi niya uhujumu uchumi na upelelezi katika shauri hilo haujakamilika na Hakimu Isaya ameahirisha kesi hiyo hadi Agosti 24, mwaka huu.
 
Mk
Mkuu naomba ujibu swali hili.

Huo upatu alikuwa ana Opearate vipi na yeye alikiwa anapataje faida.

Nipe maelezo kimfano wa figure za fedha.
 
Ipi hoja yako iliyofanya u-attach hii taarifa ??
 
Mashtaka 7

1.Kuendesha biashara haramu ya Upatu

2.Kukusanya mtaji kwa umma bila kuwa na leseni.

3-7.Matano yanahusika na utakatidhaji fedha

Tuwekane sawa HAJASHTAKIWA KWA KUTAKATISHA FEDHA PEKEE.
 
Ipi hoja yako iliyofanya u-attach hii taarifa ??
Nilitaka uone mashtaka yanayomkabili ili mjadala tuutazame pia kwa jicho la kiserikali/kisheria.

Nataka tuone kwanini wamemkamata na kumshtaki huyu jamaa.
 
Najisikia huruma jinsi ambavyo na wewe bado unaamini hii kitu kwa nguvu zote,ila pia majibu yako hayapo strait,unakubali kuwa ingecollapse wakati huohuo unakataa,pia unadhani hela zilikuwa zikiingizwa kwa awamu kitu ambacho si kweli maana ingecollapse mapema zaid,kilichochelewesha kukollapse ni kwa kuwa watu walikuwa wanaendelea kuwekeza kila siku,pitia uzi vizur Kuna watu wameelimisha vizuri Sana na kama hujui pyramid vizur bado utakuwa hutuelewi
ngoja nikupe sababu zinazofanya Mr kuku kuwa na makosa
Moja,kukusanya cash deposits lazima uwe na kibali cha benki kuu (unakua bank au saccos) kitu ambacho sijui kama alikuwa nacho,
Pili,kama alitaka kukusanya mtaji kwa njia ya share lazima awe listed na dse,
Kuna condition ngumu Sana kuwa listed ikiwemo kuandaa mahesabu yaliyokaguliwa kila baada ya miezi minne (quarterly) lengo ni kulinda fedha za uma
 
Unafafanua vyema.. kwa uzoefu wako ww, hizo returns na faida pengine zingetakiwa ziwe kwa mwaka au walau miez 9 sio?
 
Mashtaka 7

1.Kuendesha biashara haramu ya Upatu

2.Kukusanya mtaji kwa umma bila kuwa na leseni.

3-7.Matano yanahusika na utakatidhaji fedha

Tuwekane sawa HAJASHTAKIWA KWA KUTAKATISHA FEDHA PEKEE.
Jamaa inabidi uwe critical kuview jambo.

Suala lipo hivi umeitwa UPATU kwasababu biashara haina leseni mzee mbali na hapo isingeitwa upatu...upatu unaouzungumzia wewe humu na wao wanavyomaanisha hapo ni vitu viwili tofauti.

✔Wao wanaita upatu kwamaana biashara ilihusu kuchangisha watu, wameita haramu kwa maana ya leseni hakuna.

✔wewe unasema upatu kwamaana yako ambayo eti watu wakichanga wanalipwa na wataochanga mbele.

Umeona tofauti kwahiyo elewa hoja tunazokupinga hapa jukwaani.
 
Mjini pesa ipo nyingi sana kwenye mifuko ya wajinga sema tu hatujajua jinsi ya kuzibeba na kutokomeza umaskini, saivi Ontario twitter anatoa laki laki subili bomu litakalo pigwa hamtoamini zaidi ya M500
Alikufanya nn ? mbona mtu poa sana ? hebu jaribu kua na mtu karibu umjue mwenyewe na sio kuambiwa na watu
 
Nilijaribu kukupa interval ili tusichanganyane basi wanalipa kilasiku still utahitaji kuwalipa kilasiku kwa double je double money unaitoa wapi namba makinika na mzizi hoja kuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…