Fahamu zaidi kuhusu Mr Kuku

Fahamu zaidi kuhusu Mr Kuku

Hao broiler walikuwa hawaishi?[emoji16][emoji16]
Kwahio Kuku alokua akifuga alikua anakula na familia yake? Ungekua kweli una ufahamu ningekuelewa kama ungesema cash flow yake ya mauzo ya Kuku hayakulingana na matarajio ya wawekezaji. Unaiweka kama vile hakua na project yoyote ya kutengeza hela. Acheni uzushi, fatilieni muelewe.

Na hizo hesabu zako ni za kitoto sana. Hio bilioni 17 ni lugha tu ya kimahamaka, una uelewa mdogo. DPP anavuta statement yako yote na kuhesabu all the CREDITS bila kujali kuna Debit zilipita. Na hata kama kweli watu wamewekeza Bilioni17, kwani wote waliwekeza siku moja?

Shule muhimu hapa

Sent from my SM-G928F using JamiiForums mobile app
 
Wabongo tusiwe wepesi wa kushikiwa Akili Na Kanjanja mmoja!!
Hizi vikundi vya ONLINE vimekua vingi na watu wanapigwa!! Ukiwaambia et acha #Uwoga!!
Ni vizuri hizo Idea watu wazirejeshe kwenye familia,Ukoo Kama Ni kilimo mashamba ya kwenu yapo, Kama Biashara ya mazao,bidhaa mbalimbali angalie vipato vyenu kwenye familia,Ukoo wekeni hizo hisa changishaneni Mukiwa na lengo moja
Najua hata kwenye familia,au ukoo unaweza pata changamoto lakini Ni vizuri zaidi kuliko haya yanayoendelea ONLINE
 
UPATU maana yake rahisi ni kuwa mr kuku hakuwa anatoa GAWIO kupitia faida za kuendesha mradi bali ni makusanyo ya wawekezaji wapya yanatumika kulipa wawekezaji wa zamani.

Yaani muda wote anakusanya mtaji hakuna deadline, no target....

Hata kwenye bond mwaka jana tumeona NMB walikusanya mtaji kwa njia ya bond kutoka kwa wawekezaji...time frame miaka 3 faida baada ya kutoa kodi kwa milioni 50 wanatoa milioni 13.2 kwa miaka 3.

Nmb waliruhusiwa kuuza bond wakilenga kukusanya bilioni 300 I think....Ndio ni muhimu ijulikane unalenga kukusanya kiasi gani na BOT waliwapa Nmb time frame ya lini mwisho wa kununua bond na target ya amount.

Kwahiyo kwa 50m kwa mr kuku ndani ya miezi 3 anakupa 35m huu ni utapeli usiohitaji degree wala elimu hata ya cheti tu kujua unaibiwa.

Wawekezaji mliambiwa bei gani ilikuwa inahitajika au mkiambiwa kuna kuku 280,000 mnapagwa mnaweka hela[emoji23]Poleni.Amekuasanya bilioni 17 ana kuku broiler 280,000 na mnasema alikuwa anauza broiler 1 sh 4500 maana yake kuku wote 280,000 ni bilioni 1.2 na yeye amekusanya bilioni 17 hao wawekezaji wengine ATAWALIPAJE?

Kwa mfumo wa serikali hapo mmeumia hela zimeenda hizo zilizotumika na hata zilizopo benki no gawio[emoji91]
Kuna jamaa yangu alichukua ka"nssf" kake akaamua kuweka huko km laki4 iv...skumbuki fresh... ingawa sina utaalam na izo makitu ila nlimwambia aachane nazo bora atafte biznez rahisi anayoweza kuisimamia mwenyewe... akasema ye hawezi bora awekeze....
Saiv anasema bora angeniskiza...

Saiv kanssf kameisha.... huko nako wamempuga.... dah.... kitonga noma.
 
Muwe mnafuatilia mambo kabla ya kutuhumu watu. Je, mnaamini watu wote walio Segerea kwa Money Laundering ni kweli wametakatisha pesa?

Nendeni Kigamboni Kisarawe 2 karibu na kiwanda cha Maji (Afya) muone mabanda makubwa sana ya kufugia Kuku tena yapo 14 na mlima wa Mbolea ya kuku. Walikua wanafuga Kuku mpaka laki 2 kwa mpigo kutokana na pesa za wawekezaji. Nenda kaulize hata majirani kama hakukua na mradi wa ufugaji uliokua ukiendelea. UPATU unatokea wapi hapo?

Huyo Wankyo Simon ndio kiboko ya kesi za Money laundering. Wanatafuta tu sababu ya kutaifisha hizo Bilioni17 za wananchi.

Kama kweli huu ni Upatu, mbona kuna miradi mingine kama hio mitatu nayoifahamu bado inaendelea na watu wanawekeza huko?

CHEMA - Unawekeza hela kisha baada ya miezi mitano unarudishiwa 60% ya pesa ulowekeza

WEKU - Picha inajieleza

JATU - Hawa wana wanachama zaidi ya 2000 na viongozi wa Serikali hadi Waziri Manyanya kashahudhuria mikutano yao. Unawekeza 1/3, wanakukopesha 2/3 na kukulimia Mahindi, Maharage, Mpunga n.k na baada ya mavuno wanakurudishia 1/3 yako plus faida yote ya mauzo ya mavuno yatokanayo na 3/3 ya mtaji.

Acheni ushamba, kilimo kina faida kikifanywa kitaalamu. Huyo Tariq wa Mr Kuku amesoma SUA na aliajiri maafisa Kilimo waliokua full time pale Shambani. Anachukua pesa yako na kuizungusha kwa faida mara NNE kabla ya kukurudishia 70% ya faida. Broiler anakuzwa kwa mwezi MMOJA tu na kuuzwa, maajabu yako wapi hapo?

Hii ni dhulma tu, hamna maelezo tofauti.

Hio Bilioni 17 imewatoa watu fulani mate.View attachment 1533329View attachment 1533332
Bado kuna wanaotetea duh
 
Sema idea ya jamaa ilikua poa sana maana hela inaingia kwenye mzunguko. Ila labda kwakua serikali inataka watu wafanye kazi sio kuweka hela wakisubiri faida, basi ana makosa
 
Vimoradi miradi hivi vya sungura mara sijui samaki mara kuku mara nyanya huwa siviamini, ni bora ifanye mwenyewe at your own pace na kujijengea uwezo taratibu, asije mtu akaja kukupa plan ya kuingiza hela haraka haraka, ni utapeli tu
 
Muwe mnafuatilia mambo kabla ya kutuhumu watu. Je, mnaamini watu wote walio Segerea kwa Money Laundering ni kweli wametakatisha pesa?

Nendeni Kigamboni Kisarawe 2 karibu na kiwanda cha Maji (Afya) muone mabanda makubwa sana ya kufugia Kuku tena yapo 14 na mlima wa Mbolea ya kuku. Walikua wanafuga Kuku mpaka laki 2 kwa mpigo kutokana na pesa za wawekezaji. Nenda kaulize hata majirani kama hakukua na mradi wa ufugaji uliokua ukiendelea. UPATU unatokea wapi hapo?

Huyo Wankyo Simon ndio kiboko ya kesi za Money laundering. Wanatafuta tu sababu ya kutaifisha hizo Bilioni17 za wananchi.

Kama kweli huu ni Upatu, mbona kuna miradi mingine kama hio mitatu nayoifahamu bado inaendelea na watu wanawekeza huko?

CHEMA - Unawekeza hela kisha baada ya miezi mitano unarudishiwa 60% ya pesa ulowekeza

WEKU - Picha inajieleza

JATU - Hawa wana wanachama zaidi ya 2000 na viongozi wa Serikali hadi Waziri Manyanya kashahudhuria mikutano yao. Unawekeza 1/3, wanakukopesha 2/3 na kukulimia Mahindi, Maharage, Mpunga n.k na baada ya mavuno wanakurudishia 1/3 yako plus faida yote ya mauzo ya mavuno yatokanayo na 3/3 ya mtaji.

Acheni ushamba, kilimo kina faida kikifanywa kitaalamu. Huyo Tariq wa Mr Kuku amesoma SUA na aliajiri maafisa Kilimo waliokua full time pale Shambani. Anachukua pesa yako na kuizungusha kwa faida mara NNE kabla ya kukurudishia 70% ya faida. Broiler anakuzwa kwa mwezi MMOJA tu na kuuzwa, maajabu yako wapi hapo?

Hii ni dhulma tu, hamna maelezo tofauti.

Hio Bilioni 17 imewatoa watu fulani mate.View attachment 1533329View attachment 1533332
Mmoja wa wapiga debe alikuwa huyu.
 
In
1.Uwepo wa wafanyabiashara wengine wanaofanya UPATU sio justification ya anachofanya mr kuku

2.Kukusanya mtaji kwa umma lazima uwe na kibali cha benki kuu na mamlaka ya mitaji na masoko na IJULIKANE UNAKUSANYA KIASI GANI KWA LENGO GANI KIASI HICHO KIKITIMIA KAMA ULIVYOAINISHA KWENYE PROPOSAL BASI ZOEZI LINASITISHWA....Hapa ndipo tatizo linapoanzia

3.Huyu Mr Kuku alikuwa ndo anaanza kuwekeza... kununua eneo,kujenga mabanda,....kama sehemu ya mtaji unawekwa huko maane yake RETURN yake sio ya miezi 3

4.Kuna vigezo vinahitajika kufikiwa kwa kampuni ili iweze kuruhusiwa kukusanya mtaji kwa umma sio start up

5.Mimi nafuga NAWAMBIA UKWELI HUWEZI KUPATA FAIDA YA 70% KWA MIEZI 3 HAPA NDIPO UPATU ULIPO....AJABU MR KUKU ALIKUWA ANATOA GAWIO LA 70% NA KUBAKIA NA FAIDA YAKE KWAHIYO LABDA ALIKUWA ANAPATA 100% ANATOA 70% KWA MWEKEZAJI ANABAKI NA 30%

Dada yangu alitaka kuwekeza aliponitafuta nilimzuia kwa kumpa FACT leo amenishukuru.
Inamaana wawekezaji walikuwa wanapata pesa zao ??
 
UPATU maana yake rahisi ni kuwa mr kuku hakuwa anatoa GAWIO kupitia faida za kuendesha mradi bali ni makusanyo ya wawekezaji wapya yanatumika kulipa wawekezaji wa zamani.

Yaani muda wote anakusanya mtaji hakuna deadline, no target....

Hata kwenye bond mwaka jana tumeona NMB walikusanya mtaji kwa njia ya bond kutoka kwa wawekezaji...time frame miaka 3 faida baada ya kutoa kodi kwa milioni 50 wanatoa milioni 13.2 kwa miaka 3.

Nmb waliruhusiwa kuuza bond wakilenga kukusanya bilioni 300 I think....Ndio ni muhimu ijulikane unalenga kukusanya kiasi gani na BOT waliwapa Nmb time frame ya lini mwisho wa kununua bond na target ya amount.

Kwahiyo kwa 50m kwa mr kuku ndani ya miezi 3 anakupa 35m huu ni utapeli usiohitaji degree wala elimu hata ya cheti tu kujua unaibiwa.

Wawekezaji mliambiwa bei gani ilikuwa inahitajika au mkiambiwa kuna kuku 280,000 mnapagwa mnaweka hela[emoji23]Poleni.Amekuasanya bilioni 17 ana kuku broiler 280,000 na mnasema alikuwa anauza broiler 1 sh 4500 maana yake kuku wote 280,000 ni bilioni 1.2 na yeye amekusanya bilioni 17 hao wawekezaji wengine ATAWALIPAJE?

Kwa mfumo wa serikali hapo mmeumia hela zimeenda hizo zilizotumika na hata zilizopo benki no gawio[emoji91]
Unajua hesabu

Chukua 18 Billion gawanya miaka mitatu aliyo oparate Mrkuku ambzo ni siku 360×3 then uoate Figure kwasiku alikuwa anakusanya kihasi gani then uwangalie kuana uharisia...there is extra thing than upatu.
 
L
Huyu ni tapeli,si ndio huyuhuyu aliwapiga hela watu katika mradi wake wa kukopesha kupitia mtandao wa L-PESA?
L-pesa alipigaje elezea japo ??

Nimeshindwa kuumiza akiri mkopeshaji ampige mkopeshwa hemu eleza hii.
 
Huyu jamaa ni tapeli per se! Ole wenu mnaokubali kutapeliwa mchana kweupe tena kwa jambo lililo dhahiri. Nina uhakika fedha zenu zitapotea na hamtakuwa na namna ya kumshtaki kwani anafanya utapeli wa kisayansi! Anafuata sheria zote na mwisho wake jibu litakuja kuwa ''kampuni ilifikilisika kama biashara yoyote inavyoweza kufilisika''. Na sheria itakuwa upande wake kwani ninyi wawekezaji mmejiunga kwa hiyari baada ya kuafiki katiba na kanuni za kampuni ikiwemo kufilisika.
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
 
We mbona ulikuwaga unamtetea Sana inaonekana mko kundi moja so unajifanya kutokea nyuma ya keyboard ili kuwaaminisha watu. Pumba..... Sana.
Mimi mpaka leo naweza tetea hoja ya jamaa kuna client wake aliye taperiwa...sipo upande wowote ila jambo lina angle tofauti na tunavyoliumba.
 
Kwahio tunatakiwa wote tumkosoe?

Usiwe kama Nyumbu, tumia akili yako uelewe na sio kufata tu mkumbo.
Unajua kuna hali ya ukondoo inatengenezeka automatically JF member kufata upepo ukienda agaist au kuhoji wanakugeukia ili wakupige vichwa.
 
Habari wana chamvi, nimesoma uzi kuhusu mada tajwa hapo juu nami nataka kushirikishana uzoefu wangu kuhusu huyo 'mwekezaji".

Huyo bwana anaitwa Tariq, mwaka juzi 2018 nilisoma bandiko lake fb kuhusu mradi wa kilimo cha nyanya cha umwagiliaji, ahadi ilikuwa nzuri kuhusu faidi ambapo kiwango cha chini cha hisa ilikuwa 36 na kila hisa 5000/= hivyo unapata 180,000 /=

Baada ya miezi mitatu unapata 360,000/= nilitamani kuwekeza japo nilikuwa na shaka, niliongea nae akanielewesha kwamba uwekezaji ni kupitia vikundi vya watu 15, hivyo akaniunganisha na wadau tukawa na kikundi cha What App tulikuwa mikoa tofauti ila mm niliiona na advantage kwa kuwa mradi ungefanyika jirani.

Tukaanza taratibu za katiba usajili wa kikundi, kabla ya kusajili kikundi akasema tutume fedha ili mradi uanze kuendana na wakati ili kuwahi soko la nyanya.

Baada ya kutoa fedha tulipitia ubabaishaji mwingi sana, mara mradi wa arusha hauwezekani kuna shamba moro, wadau wakataka kwenda moro baada ya muda akasema kule eneo linapitiwa na reli mradi utakuwa Tanga akatutumia vi picha vya eneo na ka tank. Wadau wakalazimisha wakaenda Tanga kufika hakuna kinachendelea.

Tukaanza harakati za kukamilisha katiba na mkataba ili tujipange kwa hatua zaidi. Baada ya muda sana akasema amepata hasara hivyo fedha iliyobaki atawekeza mradi wa kuku uliopa kigamboni. Tukaendelea kupambana na kufuatilia.

Baada ya mwaka baada ya kuwa na maamuzi ya kwenda vgombo vya sheria ndo akaturudishia mitaji yetu na kuahidi faida baada ya muda. Baada tu ya kurudisha mitaji hakuwa anapokea simu wala kujibu hoja za group la What App ambalo tulianzisha. Baada ya kuanza tena harakati za kutaka kufuatilia faida akatoka katika kundi kwa jazba na kusema tufanye tunavyotaka hayupo tayari kuendelea na sisi.

Kama ambavyo mmeona tangazo lake ndivyo alivyo huwa hajibu wala kutoa ufafanuzi wa kina kuhusu hoja.

Pamoja na kwamba uoga wako ndo umaskini wako ila kwa wawekezaji wa kibongo bora kuwa mwoga. "invest on your own risk"

Nawatakia wakati mwema.
Kumbe Jamaa ni Tapeli tu kama kina Ontario ilikuwaje akaaminika na wakulungwa? Au alitumia Ndumba na Ngaye?
 
Dah mimi sijui tunakwama wapi.

Huyu mtu anajinadi kuwa ana biashara ya kuku na anawaalika watu waende kwenye mashamba yake kuona uwekezaji, wanaenda na wanashawishika na wanawekeza, mtu mmoja ninayefahamiana naye amewekeza huko 5,000,000. Sasa maswali ya kujiuliza ni haya:

1. Ikiwa Mr Kuku Farms ana biashara ambayo inakua kwa kasi na kuweza kurejesha mtaji na faida kubwa ndani ya muda mfupi, NI IPI RAHISI KWA MWEKEZAJI HUYU KATI YA KUCHUKUA 700,000 KWA RIBA YA 100% KWA MUDA WA MIEZI 6 KUTOKA KWA INDIVIDUALS au KUCHUKUA MKOPO BENKI KWA RIBA TUNAZOZIJUA

2. Iikiwa investment ya Mr Kuku Farms ina return kubwa kiasi hiki, kwa nini anaendelea kuchukua fedha kwa watu wengine?

Mimi umaskini wangu huwa unaletwa na roho ya kusita sita, ndio maana hata utajiri wa Namaingo Business Agency ulinikosa. Niliuliza maswali nikafukuzwa kwenye semina na wamama wenye ushungi walinizodoa. Naamini sasa watakuwa matajiri wakubwa kwa ufugaji wa sungura kuku na samaki huko kijiji cha Mbawa ikiwa hakikuota mbawa
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
 
Back
Top Bottom