Fahamu zaidi kuhusu tatizo la minyoo sugu na tiba yake

Fahamu zaidi kuhusu tatizo la minyoo sugu na tiba yake

The hammer

JF-Expert Member
Joined
May 17, 2011
Posts
2,397
Reaction score
1,786

1608109355795.png

BAADHI YA MASWALI YALIYOULIZWA KUHUSU TATIZO HILI
Wadau ni dawa gani inaweza kutibu minyoo hookworms,tapeworms na wengineo kwa uhakika kwa watoto wadogo na watu wazima. pia ni minyoo aina gani wanaotekenya kwenye anus coz nakumbuka wakati wa udogo wangu niliwahi kukumbwa na tatizo la namna hiyo na je ni dawa gani hasa inayoweza ondoa minyoo ya kwenye anus. Naombeni majibu
---
Wanabodi kwa yule anayefahamu dawa ya kumaliza kabisa minyoo ya aina zote ambayo ni Sugu anijuze hapa naitafuta dawa hii.

Maana hizi Albendazol, Combatrin na Mabendazole naona zimechemsha, nahitaji kwa ajili ya mtu mzima na si mtoto dawa ambayo inauwa minyoo ya aina zote.

Karibuni bandugu na si vibaya ukiipa promo phamacy ambayo naweza kupata dawa hii.

UFAFANUZI WA JUMLA WA TATIZO LA MINYOO
Minyoo ni wadudu hatari ambao huingia tumboni mwa binadamu na kusababisha matatizo kadhaa ya kiafya. Ukubwa wa minyoo tumboni hutofautiana, kuna minyoo yenye urefu wa kuanzia inchi sita hadi inchi 26, ikitegemea imekaa kwa muda gani tumboni.

Kwa kawaida minyoo huingia tumboni kwa njia kuu mbili, ingawa zipo njia nyingine. Minyoo huingia tumboni kwa kula chakula kisicho salama au kwa njia ya ngozi, hasa kwa watu wanaopenda kutembea na kucheza bila viatu miguuni.

Watoto ndiyo wanao ambukizwa zaidi minyoo kwa njia ya ngozi kutokana na tabia yao ya kupenda kucheza bila viatu, tena wakiwa sehemu zisizo safi. Vile vile mtu anaweza kupata minyoo kwa kunywa maji yasiyo salama au kwa kuumwa na mbu, inzi na hata kwa njia ya kujamiana bila kinga.

Dalili za mtu mwenye minyoo ni pamoja na mtu kuwa na utapiamlo, kuonekana dhaifu na ngozi kupauka, kusumbuliwa na tumbo, kula sana na kusikia njaa muda mfupi baada ya kumaliza kula. Pia mtu mwenye minyoo huwa mwenye hasira kila mara.

TIBA YA NYANYA
Pamoja na tiba mbadala nyingine unazoweza kuzijua, nyanya imepewa nafasi ya kwanza katika kutibu tatizo hili kwa mafanikio makubwa na bila kuleta madhara kwa mtumiaji baada ya kumaliza tiba.

JINSI YA KUTUMIA NYANYA KAMA TIBA
Tayarisha nyanya mbili za ukubwa wa kawaida kwa kuziosha vizuri (inashauriwa uzioshe kwa maji ya moto ili kuua vijidudu, ikiwemo minyoo), zikatekate
Kisha changanya na chumvi pamoja na unga kiasi wa pilipili manga.

Kula mchanganyiko huo wa nyanya, chumvi kidogo na pilipili manga asubuhi kabla ya kunywa chai au kitu chochote. Fanya zoezi hilo mara moja kwa siku, kwa muda wa siku 15 au wiki mbili. Kwa kula nyanya hizo, minyoo wote waliyomo mwilini mwako wataondoka na kuacha tumbo lako safi.

Tiba hii inaweza pia kutumiwa na watoto, lakini kwa watoto wenye umri wa KUANZIA MIAKA MITATU TU na kuendelea, haishauriwi kutumiwa na watoto wadogo chini ya umri huo.

Mnyoo ni aina ya nematodi mkubwa ambaye anaishi katika matumbo ya Binadamu na anasababisha ugonjwa wa minyoo. Inakadiriwa kwamba karibu ya robo ya idadi ya watu duniani wameathiriwa na ugonjwa huu, na hasa umeenea sana katika maeneo ya kitropiki na maeneo yenye hali duni ya usafi.

Aina nyingine ya minyoo ya jamii ya Askaris inaweza kusababisha magonjwa katika mifugo. Maambukizi hutokea kwa njia ya kula chakula kilichoathiriwa na kinyesi chenye mayai ya minyoo aina ya Askaris. Buu wa mnyoo hutotolewa, na kujichimbia kupitia utumbo mdogo, hupita mpaka kwenye mapafu na mwishowe kufikia na kuhamia katika mfumo wa hewa.

Kutoka hapo humezwa na mtu na hurudi tena na hukua na kukomaa katika utumbo kwa kuongezeka hadi sentimita 30 (inchi 12) kwa urefu na hujishikiza katika ukuta wa utumbo.

DALILI
  • Kama idadi ya minyoo ni ndogo, unaweza kutoona dalili za ugonjwa huu. Hata hivyo unaweza kuambatana na:-
  • Homa
  • kuharisha
  • kuvimba tumbo
  • kuvimba ini au wengu
  • Kichomi cha mara kwa mara
  • Kichefuchefu na kutapika minyoo ya duara
  • Maumivu ya tumbo
  • Kupungua uzito

Matatizo mazito yanaweza kujitokeza kama minyoo itahamia sehemu nyingine za mwili kama mapafu, ini, na sehemu nyingine za mwili asa msokoto na kuoza kwa sehemu ya utumbo mdogoambayo hupelekea kifo.

MATIBABU
Dawa zinazotumika kuua nematodi huitwa kiuaminyoo ni pamoja na Mebendazole, ivermectin, Albendazole na Pyrantel pamoate ambazo hutolewa hosipitali kwa maelekezo ya daktari kulingana na ukubwa wa tatizo.

Kumbuka matumizi ya vyoo, ulinzi wa chakula kutoka uchafu na udongo na kuosha mkono kabla ya kula ni njia mojawapo za kujiepusha na magonjwa ya minyoo.

BAADHI YA MAONI YALIYOTOLEWA NA WADAU WA JF
Imeandikwa na: Dr.Henry Mayala Jr Mnamo: Mar 29
Mojawapo ya tatizo linaloathiri jamii katika nchi nyingi zinazoendelea ikiwemo Tanzania ni magonjwa yanayohusiana na minyoo. Duniani kwa ujumla, takribani watu billion moja wameripotiwa kuwa na uvamizi wa minyoo aina ya helminthes kwenye miili yao.​
Minyoo huenezwa kwa njia zipi?​
Minyoo huenezwa pale maji au chakula vinapokuwa vimeathiriwa na mayai au mabuu ya minyoo. Hali kadhalika, uwezekano wa kupata minyoo huchangiwa pia na kutonawa mikono kabla ya kula na baada ya kutoka kujisaidia haja kubwa. Aidha watoto wadogo chini ya miaka mitano ambao hupenda kuchezea mchanga au uchafu kwa ujumla na ambao hupendelea pia kunyonya vidole nao pia huambukizwa kwa urahisi. Mambo mengine yanayochangia katika kupata uvamizi wa minyoo ni pamoja na kuishi katika mazingira machafu, kutembea bila viatu (pekupeku) na kula vyakula ambavyo havijaiva au visivyopikwa vizuri (undercooked foods).​
Aina za minyoo na madhara yake kwa binadamu​
Kuna aina kadhaa za minyoo ambazo, ukiachilia mbali kuwashambulia wanyama wengine kama ngombe, nguruwe, mbuzi na kondoo, humshambulia pia binadamu. Aina hizi ni pamoja na​
  • Minyoo jamii ya round worms kwa mfano Ascaris lumbricoides ambao husababisha utumbo kuziba (intestinal obstruction) au uambukizi katika kidole tumbo (appendicitis)
  • Minyoo jamii ya hook worms kwa mfano Ancylostoma duodenale ambao huishi kwa kunyonya damu kwenye utumbo mdogo na hivyo kusababisha upungufu wa damu mwilini.
  • Minyoo jamii ya pin worms au thread worm kwa mfano Enterobius vermicularishusababisha kuwashwa hasa sehemu za haja kubwa kwa sababu ya mcharuko mwili unaotokana na minyoo hii kutoa mayai yao eneo hilo hasa kipindi cha usiku.
  • Minyoo jamii ya whip worms kwa mfano Trichuris trichiura husababisha kinyesi kuchanganyika na damu, kupungua uzito, upungufu wa damu na kutoka nje kwa puru (rectal prolapse).
  • Minyoo jamii ya tegu (tape worms) kama vile Taenia solium husababisha kifafa pindi wanapovamia ubongo hasa katika hatua ya ukuaji iitwayo cystercosis
Dalili za minyoo ni zipi?​
Minyoo-dalili-150x150.jpg
Dalili za kuwepo kwa uvamizi wa minyoo mwilini hutegemea sana aina ya minyoo inayomuathiri mgonjwa. Lakini kwa ujumla, dalili ni pamoja na​
  • Maumivu ya tumbo
  • Kupata choo kigumu sana
  • Kuharisha
  • Kujisikia mchovu na mlegevu kutokana na kupungukiwa damu
  • Kupoteza hamu ya kula
  • Tumbo kuwa na gesi na kuhisi limejaa
  • Kukohoa na kupiga chafya
  • Kwa watoto kusugua meno, kujipinduapindua pamoja na kujikojolea kitandani
  • Kichwa kuuma au kupata kifafa kama minyoo (jamii ya taenia solium) ikitaga mayai yake kwenye ubongo
  • Kuwashwa, na
  • Huathiri ukuaji kwa watoto
Utatambuaje kama umeathiriwa na minyoo?​
Vipimo vinavyoweza kusaidia kugundua uvamizi wa minyoo, aina zake na hata madhara yaliyosababishwa na minyoo ni pamoja na:​
  • Kupima choo kikubwa (Stool examination) kwa ajili ya kuchunguza mayai na mabuu ya minyoo iliyo katika haja kubwa kwa kutumia darubini
  • Kupima damu (Complete blood count) huku mkazo zaidi ukiwa kwenye Eosinophil na kiwango cha damu (Hb). Iwapo kuna uvamizi wa minyoo, kiwango cha Eosinophil huwa juu zaidi kuliko kawaida.
  • X-ray yaweza kusaidia kuchunguza hatua mojawapo ya ukuaji wa minyoo ya Taenia solium iitwayo cystercosis katika ubongo au paja.
  • CT na MRI pia zaweza kurahisisha kugundua na kutambua cyst (vifuko vyenye majimaji) za minyoo aina ya hydatid ambayo huvamia ini, ubongo, figo na sehemu nyingine za mwili.
  • Kipimo cha puru (proctoscopy) husaidia kutambua uvamizi wa minyoo aina ya trichiuris trichiura kwenye puru.
Minyoo inatibika?
Minyoo-matibabu-150x150.jpg
Bila shaka kabisa, minyoo inatibika. Dawa zifuatazo hutumika katika kutibu minyoo kulingana na aina ya minyoo inayomuathiri mgonjwa​
  • Mebendazole hutumika kutibu zaidi uvamizi wa minyoo aina ya round worms
  • Albendazole yaweza kutibu minyoo aina ya tegu (tape worms) pamoja na hydatid
  • Ivermectin hutumika kutibu aina mbalimbali za minyoo
  • Ketrax (levamisole) nayo pia ina uwezo wa kutibu aina kadhaa za minyoo
  • Piperazzine pia ina uwezo wa kutibu aina nyingine nyingi za minyoo.
Hata hivyo, tunashauri sana matumizi ya dawa hizi hasa kwa watoto, yafanyike mara baada ya kupata ushauri wa daktari na si vinginevyo.​
Inawezekana kujinga dhidi ya uvamizi wa minyoo?​
Njia za kujikinga na minyoo ni pamoja na​
  • Kuishi katika mazingira safi.
  • Kunawa mikono na sabuni baada ya kutoka msalani na kabla ya kula
  • Kukata kucha (kucha ndefu huweza kutunza uchafu)
  • Kuwa muangalifu hasa unapokuwa na wanyama kama paka na mbwa
  • Kutumia dawa za kuzuia uvamizi (deworming) kila baada ya miezi mitatu au sita
chanzo Fahamu kuhusu Minyoo (Helminthesis) – TanzMED(old) - Afya Kwa Wote​
---
Minyoo ni wadudu hatari ambao huingia tumboni mwa binadamu na kusababisha matatizo kadhaa ya kiafya. Ukubwa wa minyoo tumboni hutofautiana, kuna minyoo yenye urefu wa kuanzia inchi sita hadi inchi 26, ikitegemea imekaa kwa muda gani tumboni.

Kwa kawaida minyoo huingia tumboni kwa njia kuu mbili, ingawa zipo njia nyingine. Minyoo huingia tumboni kwa kula chakula kisicho salama au kwa njia ya ngozi, hasa kwa watu wanaopenda kutembea na kucheza bila viatu miguuni.

Watoto ndiyo wanao ambukizwa zaidi minyoo kwa njia ya ngozi kutokana na tabia yao ya kupenda kucheza bila viatu, tena wakiwa sehemu zisizo safi. Vile vile mtu anaweza kupata minyoo kwa kunywa maji yasiyo salama au kwa kuumwa na mbu, inzi na hata kwa njia ya kujamiana bila kinga.

Dalili za mtu mwenye minyoo ni pamoja na mtu kuwa na utapiamlo, kuonekana dhaifu na ngozi kupauka, kusumbuliwa na tumbo, kula sana na kusikia njaa muda mfupi baada ya kumaliza kula. Pia mtu mwenye minyoo huwa mwenye hasira kila mara.

TIBA YA NYANYA
Pamoja na tiba mbadala nyingine unazoweza kuzijua, nyanya imepewa nafasi ya kwanza katika kutibu tatizo hili kwa mafanikio makubwa na bila kuleta madhara kwa mtumiaji baada ya kumaliza tiba.

JINSI YA KUTUMIA NYANYA KAMA TIBA
Tayarisha nyanya mbili za ukubwa wa kawaida kwa kuziosha vizuri (inashauriwa uzioshe kwa maji ya moto ili kuua vijidudu, ikiwemo minyoo), zikatekate. Kisha changanya na chumvi pamoja na unga kiasi wa pilipili manga.

Kula mchanganyiko huo wa nyanya, chumvi kidogo na pilipili manga asubuhi kabla ya kunywa chai au kitu chochote. Fanya zoezi hilo mara moja kwa siku, kwa muda wa siku 15 au wiki mbili. Kwa kula nyanya hizo, minyoo wote waliyomo mwilini mwako wataondoka na kuacha tumbo lako safi.

Tiba hii inaweza pia kutumiwa na watoto, lakini kwa watoto wenye umri wa KUANZIA MIAKA MITATU TU na kuendelea, haishauriwi kutumiwa na watoto wadogo chini ya umri huo.@The hammer

Dawa ya kutibu Minyoo kwa wakubwa tu hii hapa chini:

PAMBANA NA FUNGUS SUGU PAMOJA NA MINYOO

Nunua kitunguu swaumu. Menya chote kama vile uandaavyo kwa ajili ya kupikia.Twanga ama saga,vikishasagika

changanya na maji ya uvuguvugu kidogo kipimo cha kijiko cha chai ili vilainike.Chota msagiko wote wa vitunguu

na uvimeze. Tahadhari,jitahidi uwe na mfuko ama sehemu ya maliwatoni maana kama hauna tumbo zuri unaweza

tapika.(Mara chache sana hutokea kutapika) Ukishakaa kama dk 15 hali yako itarudi kawaida.Baada ya SIKU

1,utaona minyoo hakuna tena na fungus wote wamekauka!Kwisha kabisa!!!! Tumia kama Siku 3 Mfululizo ikiwa

bado hujapona ongeza tena Siku 3 zingine haitafika Siku 7 utakuwa umekwisha pona jaribu kisha uje hapa utpe Feedback.
---
Kuna dawa inaitwa Zentel kidonge ni 5000/= unatumia kimoja au zaidi inategemea na ukubwa wa tatizo but kimoja ni dose na ndio komoni.

Zentel inauwezo wakukomaa na minyoo wanaojificha kwenye utumbo mdogo waitwao Ascaris lumbricoids. Hizi dawa hospital nyingi hawatoi nadhani nikutokana na gharama labda hospital kubwa na uwe na bima.

Dawa hizi zinapatikana maduka makubwa ya dawa (pharmacy)

Ukipewa hizo dawa zingatia sana maelekezo ya mtaalamu usije kuathiri dose.
 
Minyoo ni wadudu hatari ambao huingia tumboni mwa binadamu na kusababisha matatizo kadhaa ya kiafya. Ukubwa wa minyoo tumboni hutofautiana, kuna minyoo yenye urefu wa kuanzia inchi sita hadi inchi 26, ikitegemea imekaa kwa muda gani tumboni.

Kwa kawaida minyoo huingia tumboni kwa njia kuu mbili, ingawa zipo njia nyingine. Minyoo huingia tumboni kwa kula chakula kisicho salama au kwa njia ya ngozi, hasa kwa watu wanaopenda kutembea na kucheza bila viatu miguuni.

Watoto ndiyo wanao ambukizwa zaidi minyoo kwa njia ya ngozi kutokana na tabia yao ya kupenda kucheza bila viatu, tena wakiwa sehemu zisizo safi. Vile vile mtu anaweza kupata minyoo kwa kunywa maji yasiyo salama au kwa kuumwa na mbu, inzi na hata kwa njia ya kujamiana bila kinga.

Dalili za mtu mwenye minyoo ni pamoja na mtu kuwa na utapiamlo, kuonekana dhaifu na ngozi kupauka, kusumbuliwa na tumbo, kula sana na kusikia njaa muda mfupi baada ya kumaliza kula. Pia mtu mwenye minyoo huwa mwenye hasira kila mara.

TIBA YA NYANYA
Pamoja na tiba mbadala nyingine unazoweza kuzijua, nyanya imepewa nafasi ya kwanza katika kutibu tatizo hili kwa mafanikio makubwa na bila kuleta madhara kwa mtumiaji baada ya kumaliza tiba.

JINSI YA KUTUMIA NYANYA KAMA TIBA
Tayarisha nyanya mbili za ukubwa wa kawaida kwa kuziosha vizuri (inashauriwa uzioshe kwa maji ya moto ili kuua vijidudu, ikiwemo minyoo), zikatekate. Kisha changanya na chumvi pamoja na unga kiasi wa pilipili manga.

Kula mchanganyiko huo wa nyanya, chumvi kidogo na pilipili manga asubuhi kabla ya kunywa chai au kitu chochote. Fanya zoezi hilo mara moja kwa siku, kwa muda wa siku 15 au wiki mbili. Kwa kula nyanya hizo, minyoo wote waliyomo mwilini mwako wataondoka na kuacha tumbo lako safi.

Tiba hii inaweza pia kutumiwa na watoto, lakini kwa watoto wenye umri wa KUANZIA MIAKA MITATU TU na kuendelea, haishauriwi kutumiwa na watoto wadogo chini ya umri huo.

PAMBANA NA FUNGUS SUGU PAMOJA NA MINYOO
Nunua kitunguu swaumu. Menya chote kama vile uandaavyo kwa ajili ya kupikia.Twanga ama saga,vikishasagika

changanya na maji ya uvuguvugu kidogo kipimo cha kijiko cha chai ili vilainike.Chota msagiko wote wa vitunguu

na uvimeze. Tahadhari,jitahidi uwe na mfuko ama sehemu ya maliwatoni maana kama hauna tumbo zuri unaweza

tapika.(Mara chache sana hutokea kutapika) Ukishakaa kama dk 15 hali yako itarudi kawaida.Baada ya SIKU

1,utaona minyoo hakuna tena na fungus wote wamekauka!Kwisha kabisa!!!! Tumia kama Siku 3 Mfululizo ikiwa

bado hujapona ongeza tena Siku 3 zingine haitafika Siku 7 utakuwa umekwisha pona jaribu kisha uje hapa utupe Feedback.
 
Wanabodi kwa yule anayefahamu dawa ya kumaliza kabisa minyoo ya aina zote ambayo ni Sugu anijuze hapa naitafuta dawa hii.

Maana hizi Albendazol, Combatrin na Mabendazole naona zimechemsha, nahitaji kwa ajili ya mtu mzima na si mtoto dawa ambayo inauwa minyoo ya aina zote.

Karibuni bandugu na si vibaya ukiipa promo phamacy ambayo naweza kupata dawa hii.
 
Wanabodi kwa yule anayefahamu dawa ya kumaliza kabisa minyoo ya aina zote ambayo ni Sugu anijuze hapa naitafuta dawa hii.

Maana hizi Albendazol, Combatrin na Mabendazole naona zimechemsha, nahitaji kwa ajili ya mtu mzima na si mtoto dawa ambayo inauwa minyoo ya aina zote.

Karibuni bandugu na si vibaya ukiipa promo phamacy ambayo naweza kupata dawa hii.

Mkuu kuna hii hapa naona wengi wanaisifia.
 
Wanabodi kwa yule anayefahamu dawa ya kumaliza kabisa minyoo ya aina zote ambayo ni Sugu anijuze hapa naitafuta dawa hii.

Maana hizi Albendazol, Combatrin na Mabendazole naona zimechemsha, nahitaji kwa ajili ya mtu mzima na si mtoto dawa ambayo inauwa minyoo ya aina zote.

Karibuni bandugu na si vibaya ukiipa promo phamacy ambayo naweza kupata dawa hii.

Teh teh teh!

Kwi kwi kwi kwi!

Wacha kula viporo vya kitimoto na yale mapuya pia hayafai!

Utakuja toka nyoka huko nyuma!!

Cc Ritz MUNGU SI MZUNGU
 
Last edited by a moderator:
inaanzia na z jina nimesahau ni kidonge kimoja tu dozi yake kinauzwa 6000 ni from uk inasehemu ya kusearch like vocha afu na maelekezo ya kutuma hizo no ili uambiwe kama hiyo dawa ni yenyewe na haijakwisha mda wake
 
thiabendazole jarbu hyo mku ibatibi aina zote za worms iwe hook worms,entarobius,trichius trichiuras,or strongloidy..ikishndkana muone dr.
 
Wanabodi kwa yule anayefahamu dawa ya kumaliza kabisa minyoo ya aina zote ambayo ni Sugu anijuze hapa naitafuta dawa hii.

Maana hizi Albendazol, Combatrin na Mabendazole naona zimechemsha, nahitaji kwa ajili ya mtu mzima na si mtoto dawa ambayo inauwa minyoo ya aina zote.

Karibuni bandugu na si vibaya ukiipa promo phamacy ambayo naweza kupata dawa hii.

Mkuu Una minyoo bado?
 
Comments za wengui hazijakaa sawa hata kama humkubali mtu kuna vitu sio vyakuwekea maskhara hasa linapokuja swala la afya
 
Today nimecheka sana kwa comment za watu against tatizo lake, huyu jamaa inabidi aji-refresh.....something is wrong somewhere!
 
Ascaris ni minyoo sugu sana kufa kwa kutumia dawa za hospitali na hata dawa za asili ambayo ni hafifu, hivyo kama kuna mtu yeyote anaijua dawa ya kutibu hii minyoo mibishi tafadhali tuelimishane.
 
Ubmm inspatikana dar free maketinkwny korido kwa binti muuza meza
 
Back
Top Bottom