Fahamu zaidi kuhusu tatizo la minyoo sugu na tiba yake

The hammer

JF-Expert Member
Joined
May 17, 2011
Posts
2,397
Reaction score
1,786

BAADHI YA MASWALI YALIYOULIZWA KUHUSU TATIZO HILI
Wadau ni dawa gani inaweza kutibu minyoo hookworms,tapeworms na wengineo kwa uhakika kwa watoto wadogo na watu wazima. pia ni minyoo aina gani wanaotekenya kwenye anus coz nakumbuka wakati wa udogo wangu niliwahi kukumbwa na tatizo la namna hiyo na je ni dawa gani hasa inayoweza ondoa minyoo ya kwenye anus. Naombeni majibu
---

UFAFANUZI WA JUMLA WA TATIZO LA MINYOO
Minyoo ni wadudu hatari ambao huingia tumboni mwa binadamu na kusababisha matatizo kadhaa ya kiafya. Ukubwa wa minyoo tumboni hutofautiana, kuna minyoo yenye urefu wa kuanzia inchi sita hadi inchi 26, ikitegemea imekaa kwa muda gani tumboni.

Kwa kawaida minyoo huingia tumboni kwa njia kuu mbili, ingawa zipo njia nyingine. Minyoo huingia tumboni kwa kula chakula kisicho salama au kwa njia ya ngozi, hasa kwa watu wanaopenda kutembea na kucheza bila viatu miguuni.

Watoto ndiyo wanao ambukizwa zaidi minyoo kwa njia ya ngozi kutokana na tabia yao ya kupenda kucheza bila viatu, tena wakiwa sehemu zisizo safi. Vile vile mtu anaweza kupata minyoo kwa kunywa maji yasiyo salama au kwa kuumwa na mbu, inzi na hata kwa njia ya kujamiana bila kinga.

Dalili za mtu mwenye minyoo ni pamoja na mtu kuwa na utapiamlo, kuonekana dhaifu na ngozi kupauka, kusumbuliwa na tumbo, kula sana na kusikia njaa muda mfupi baada ya kumaliza kula. Pia mtu mwenye minyoo huwa mwenye hasira kila mara.

TIBA YA NYANYA
Pamoja na tiba mbadala nyingine unazoweza kuzijua, nyanya imepewa nafasi ya kwanza katika kutibu tatizo hili kwa mafanikio makubwa na bila kuleta madhara kwa mtumiaji baada ya kumaliza tiba.

JINSI YA KUTUMIA NYANYA KAMA TIBA
Tayarisha nyanya mbili za ukubwa wa kawaida kwa kuziosha vizuri (inashauriwa uzioshe kwa maji ya moto ili kuua vijidudu, ikiwemo minyoo), zikatekate
Kisha changanya na chumvi pamoja na unga kiasi wa pilipili manga.

Kula mchanganyiko huo wa nyanya, chumvi kidogo na pilipili manga asubuhi kabla ya kunywa chai au kitu chochote. Fanya zoezi hilo mara moja kwa siku, kwa muda wa siku 15 au wiki mbili. Kwa kula nyanya hizo, minyoo wote waliyomo mwilini mwako wataondoka na kuacha tumbo lako safi.

Tiba hii inaweza pia kutumiwa na watoto, lakini kwa watoto wenye umri wa KUANZIA MIAKA MITATU TU na kuendelea, haishauriwi kutumiwa na watoto wadogo chini ya umri huo.

Mnyoo ni aina ya nematodi mkubwa ambaye anaishi katika matumbo ya Binadamu na anasababisha ugonjwa wa minyoo. Inakadiriwa kwamba karibu ya robo ya idadi ya watu duniani wameathiriwa na ugonjwa huu, na hasa umeenea sana katika maeneo ya kitropiki na maeneo yenye hali duni ya usafi.

Aina nyingine ya minyoo ya jamii ya Askaris inaweza kusababisha magonjwa katika mifugo. Maambukizi hutokea kwa njia ya kula chakula kilichoathiriwa na kinyesi chenye mayai ya minyoo aina ya Askaris. Buu wa mnyoo hutotolewa, na kujichimbia kupitia utumbo mdogo, hupita mpaka kwenye mapafu na mwishowe kufikia na kuhamia katika mfumo wa hewa.

Kutoka hapo humezwa na mtu na hurudi tena na hukua na kukomaa katika utumbo kwa kuongezeka hadi sentimita 30 (inchi 12) kwa urefu na hujishikiza katika ukuta wa utumbo.

DALILI
  • Kama idadi ya minyoo ni ndogo, unaweza kutoona dalili za ugonjwa huu. Hata hivyo unaweza kuambatana na:-
  • Homa
  • kuharisha
  • kuvimba tumbo
  • kuvimba ini au wengu
  • Kichomi cha mara kwa mara
  • Kichefuchefu na kutapika minyoo ya duara
  • Maumivu ya tumbo
  • Kupungua uzito

Matatizo mazito yanaweza kujitokeza kama minyoo itahamia sehemu nyingine za mwili kama mapafu, ini, na sehemu nyingine za mwili asa msokoto na kuoza kwa sehemu ya utumbo mdogoambayo hupelekea kifo.

MATIBABU
Dawa zinazotumika kuua nematodi huitwa kiuaminyoo ni pamoja na Mebendazole, ivermectin, Albendazole na Pyrantel pamoate ambazo hutolewa hosipitali kwa maelekezo ya daktari kulingana na ukubwa wa tatizo.

Kumbuka matumizi ya vyoo, ulinzi wa chakula kutoka uchafu na udongo na kuosha mkono kabla ya kula ni njia mojawapo za kujiepusha na magonjwa ya minyoo.

BAADHI YA MAONI YALIYOTOLEWA NA WADAU WA JF
---
---
 
Minyoo ni wadudu hatari ambao huingia tumboni mwa binadamu na kusababisha matatizo kadhaa ya kiafya. Ukubwa wa minyoo tumboni hutofautiana, kuna minyoo yenye urefu wa kuanzia inchi sita hadi inchi 26, ikitegemea imekaa kwa muda gani tumboni.

Kwa kawaida minyoo huingia tumboni kwa njia kuu mbili, ingawa zipo njia nyingine. Minyoo huingia tumboni kwa kula chakula kisicho salama au kwa njia ya ngozi, hasa kwa watu wanaopenda kutembea na kucheza bila viatu miguuni.

Watoto ndiyo wanao ambukizwa zaidi minyoo kwa njia ya ngozi kutokana na tabia yao ya kupenda kucheza bila viatu, tena wakiwa sehemu zisizo safi. Vile vile mtu anaweza kupata minyoo kwa kunywa maji yasiyo salama au kwa kuumwa na mbu, inzi na hata kwa njia ya kujamiana bila kinga.

Dalili za mtu mwenye minyoo ni pamoja na mtu kuwa na utapiamlo, kuonekana dhaifu na ngozi kupauka, kusumbuliwa na tumbo, kula sana na kusikia njaa muda mfupi baada ya kumaliza kula. Pia mtu mwenye minyoo huwa mwenye hasira kila mara.

TIBA YA NYANYA
Pamoja na tiba mbadala nyingine unazoweza kuzijua, nyanya imepewa nafasi ya kwanza katika kutibu tatizo hili kwa mafanikio makubwa na bila kuleta madhara kwa mtumiaji baada ya kumaliza tiba.

JINSI YA KUTUMIA NYANYA KAMA TIBA
Tayarisha nyanya mbili za ukubwa wa kawaida kwa kuziosha vizuri (inashauriwa uzioshe kwa maji ya moto ili kuua vijidudu, ikiwemo minyoo), zikatekate. Kisha changanya na chumvi pamoja na unga kiasi wa pilipili manga.

Kula mchanganyiko huo wa nyanya, chumvi kidogo na pilipili manga asubuhi kabla ya kunywa chai au kitu chochote. Fanya zoezi hilo mara moja kwa siku, kwa muda wa siku 15 au wiki mbili. Kwa kula nyanya hizo, minyoo wote waliyomo mwilini mwako wataondoka na kuacha tumbo lako safi.

Tiba hii inaweza pia kutumiwa na watoto, lakini kwa watoto wenye umri wa KUANZIA MIAKA MITATU TU na kuendelea, haishauriwi kutumiwa na watoto wadogo chini ya umri huo.

PAMBANA NA FUNGUS SUGU PAMOJA NA MINYOO
Nunua kitunguu swaumu. Menya chote kama vile uandaavyo kwa ajili ya kupikia.Twanga ama saga,vikishasagika

changanya na maji ya uvuguvugu kidogo kipimo cha kijiko cha chai ili vilainike.Chota msagiko wote wa vitunguu

na uvimeze. Tahadhari,jitahidi uwe na mfuko ama sehemu ya maliwatoni maana kama hauna tumbo zuri unaweza

tapika.(Mara chache sana hutokea kutapika) Ukishakaa kama dk 15 hali yako itarudi kawaida.Baada ya SIKU

1,utaona minyoo hakuna tena na fungus wote wamekauka!Kwisha kabisa!!!! Tumia kama Siku 3 Mfululizo ikiwa

bado hujapona ongeza tena Siku 3 zingine haitafika Siku 7 utakuwa umekwisha pona jaribu kisha uje hapa utupe Feedback.
 
Wanabodi kwa yule anayefahamu dawa ya kumaliza kabisa minyoo ya aina zote ambayo ni Sugu anijuze hapa naitafuta dawa hii.

Maana hizi Albendazol, Combatrin na Mabendazole naona zimechemsha, nahitaji kwa ajili ya mtu mzima na si mtoto dawa ambayo inauwa minyoo ya aina zote.

Karibuni bandugu na si vibaya ukiipa promo phamacy ambayo naweza kupata dawa hii.
 
Mkuu kuna hii hapa naona wengi wanaisifia.
 
Teh teh teh!

Kwi kwi kwi kwi!

Wacha kula viporo vya kitimoto na yale mapuya pia hayafai!

Utakuja toka nyoka huko nyuma!!

Cc Ritz MUNGU SI MZUNGU
 
Last edited by a moderator:
inaanzia na z jina nimesahau ni kidonge kimoja tu dozi yake kinauzwa 6000 ni from uk inasehemu ya kusearch like vocha afu na maelekezo ya kutuma hizo no ili uambiwe kama hiyo dawa ni yenyewe na haijakwisha mda wake
 
Mi ningeshauri hawa watu wanaoandika uduwansi wafutwege mazima,wanarusha asee
 
thiabendazole jarbu hyo mku ibatibi aina zote za worms iwe hook worms,entarobius,trichius trichiuras,or strongloidy..ikishndkana muone dr.
 
Mkuu Una minyoo bado?
 
Comments za wengui hazijakaa sawa hata kama humkubali mtu kuna vitu sio vyakuwekea maskhara hasa linapokuja swala la afya
 
Today nimecheka sana kwa comment za watu against tatizo lake, huyu jamaa inabidi aji-refresh.....something is wrong somewhere!
 
Ascaris ni minyoo sugu sana kufa kwa kutumia dawa za hospitali na hata dawa za asili ambayo ni hafifu, hivyo kama kuna mtu yeyote anaijua dawa ya kutibu hii minyoo mibishi tafadhali tuelimishane.
 
Ubmm inspatikana dar free maketinkwny korido kwa binti muuza meza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…