Minyoo ni wadudu hatari ambao huingia tumboni mwa binadamu na kusababisha matatizo kadhaa ya kiafya. Ukubwa wa minyoo tumboni hutofautiana, kuna minyoo yenye urefu wa kuanzia inchi sita hadi inchi 26, ikitegemea imekaa kwa muda gani tumboni.
Kwa kawaida minyoo huingia tumboni kwa njia kuu mbili, ingawa zipo njia nyingine. Minyoo huingia tumboni kwa kula chakula kisicho salama au kwa njia ya ngozi, hasa kwa watu wanaopenda kutembea na kucheza bila viatu miguuni.
Watoto ndiyo wanao ambukizwa zaidi minyoo kwa njia ya ngozi kutokana na tabia yao ya kupenda kucheza bila viatu, tena wakiwa sehemu zisizo safi. Vile vile mtu anaweza kupata minyoo kwa kunywa maji yasiyo salama au kwa kuumwa na mbu, inzi na hata kwa njia ya kujamiana bila kinga.
Dalili za mtu mwenye minyoo ni pamoja na mtu kuwa na utapiamlo, kuonekana dhaifu na ngozi kupauka, kusumbuliwa na tumbo, kula sana na kusikia njaa muda mfupi baada ya kumaliza kula. Pia mtu mwenye minyoo huwa mwenye hasira kila mara.
TIBA YA NYANYA
Pamoja na tiba mbadala nyingine unazoweza kuzijua, nyanya imepewa nafasi ya kwanza katika kutibu tatizo hili kwa mafanikio makubwa na bila kuleta madhara kwa mtumiaji baada ya kumaliza tiba.
JINSI YA KUTUMIA NYANYA KAMA TIBA
Tayarisha nyanya mbili za ukubwa wa kawaida kwa kuziosha vizuri (inashauriwa uzioshe kwa maji ya moto ili kuua vijidudu, ikiwemo minyoo), zikatekate. Kisha changanya na chumvi pamoja na unga kiasi wa pilipili manga.
Kula mchanganyiko huo wa nyanya, chumvi kidogo na pilipili manga asubuhi kabla ya kunywa chai au kitu chochote. Fanya zoezi hilo mara moja kwa siku, kwa muda wa siku 15 au wiki mbili. Kwa kula nyanya hizo, minyoo wote waliyomo mwilini mwako wataondoka na kuacha tumbo lako safi.
Tiba hii inaweza pia kutumiwa na watoto, lakini kwa watoto wenye umri wa KUANZIA MIAKA MITATU TU na kuendelea, haishauriwi kutumiwa na watoto wadogo chini ya umri huo.
PAMBANA NA FUNGUS SUGU PAMOJA NA MINYOO
Nunua kitunguu swaumu. Menya chote kama vile uandaavyo kwa ajili ya kupikia.Twanga ama saga,vikishasagika
changanya na maji ya uvuguvugu kidogo kipimo cha kijiko cha chai ili vilainike.Chota msagiko wote wa vitunguu
na uvimeze. Tahadhari,jitahidi uwe na mfuko ama sehemu ya maliwatoni maana kama hauna tumbo zuri unaweza
tapika.(Mara chache sana hutokea kutapika) Ukishakaa kama dk 15 hali yako itarudi kawaida.Baada ya SIKU
1,utaona minyoo hakuna tena na fungus wote wamekauka!Kwisha kabisa!!!! Tumia kama Siku 3 Mfululizo ikiwa
bado hujapona ongeza tena Siku 3 zingine haitafika Siku 7 utakuwa umekwisha pona jaribu kisha uje hapa utpe Feedback.