min -me
JF-Expert Member
- Jul 20, 2022
- 23,322
- 64,738
Kiroho ni kitu gani elezea hapa .Hivi kukesha mkesha wa mwaka mpya kuna umuhimu GANI KIROHO?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kiroho ni kitu gani elezea hapa .Hivi kukesha mkesha wa mwaka mpya kuna umuhimu GANI KIROHO?
Mungu muweza wa yote hayupo , hayo ni maneno ya kujifariji ambayo hayana uthibitisho wowote , ni maneno ya kiimani tu , ambapo dini mbalimbali wanayo na Mungu wao pia wapo tofauti kifikra.Ni mahubiri yanayothibitisha uwepo wa Mungu.
Mungu yupi unahisi anatakiwa ashukuriwe kwa sababu wapo zaidi ya 1000 wote wanajinadi ni waumba kila kitu?N
Wakati wa mkesha wa mwaka mpya, watu wanatumia muda mwingi kumshukuru Mungu. Faida za kushukuru tayari zimedadavuliwa.
Uzi mzuri sana mkuuTarehe 31 Desemba ni siku ambayo watu wengi hukusanyika makanisani kumshukuru Mungu. Zifuatazo ni faida 10 za kumshukuru Mungu:
1. Huimarisha Imani: Kumshukuru Mungu hutufundisha kutambua uaminifu Wake na kuimarisha imani yetu, tukijua kwamba anafanya kazi kwa manufaa yetu.
2. Hutupa Amani ya Moyoni: Shukrani huondoa mawazo ya wasiwasi na huzuni, na kutuachia amani ya kiroho inayotokana na kumtegemea Mungu.
3. Huongeza Furaha: Watu wanaoshukuru wana furaha zaidi kwa sababu wanathamini hata mambo madogo ambayo Mungu amewatendea.
4. Hutuleta Karibu na Mungu: Shukrani huimarisha uhusiano wetu na Mungu kwa kutufanya tutambue ukuu na upendo Wake maishani mwetu.
5. Huinua Nafsi Zetu: Kumshukuru Mungu hutusaidia kuona maisha katika mtazamo chanya, hata katika changamoto, na hutufanya tujihisi wenye thamani.
6. Hulinda Moyo Usipotoshwe: Moyo wa shukrani hutusaidia kuepuka kiburi na kujiona kuwa sisi ndio chanzo cha mafanikio yetu, badala ya kumtambua Mungu.
7. Hufungua Milango ya Baraka: Shukrani ni kitendo cha imani kinachomfanya Mungu kufungua milango ya baraka zaidi maishani mwetu.
8. Hutuongezea Uvumilivu: Tunaposhukuru kwa yale tuliyonayo, tunapata nguvu za kustahimili majaribu huku tukisubiri Mungu kutimiza ahadi Zake.
9. Hutufundisha Roho ya Unyenyekevu: Shukrani hutufundisha kuwa wanyenyekevu kwa kutambua kwamba kila kitu tunachopata kinatoka kwa Mungu.
10. Ni Njia ya Kutoa Ushuhuda kwa Wengine: Tunapomshukuru Mungu hadharani, tunawashawishi wengine kumwamini na kumtumikia Mungu kwa kuona jinsi alivyotutendea mema.
"Shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu." (1 Wathesalonike 5:18).
Baada ya kuzijua faida hizo, naamini kesho utajiunga na Wakristo wengine kumshukuru Mungu kwa mambo mengi aliyotutendea mwaka huu. Sio kesho tu, siku zote kumbuka kumshukuru Mungu, ujionee faida hizo.
Imani ni bayana ya mambo yasiyoonekana.
Sijui hata kama unaelewa unachokiandika🤔 siku ukithibitisha uwepo Mungu unitag nisije nikabaka uelewa wako bure.Mungu ni mmoja tu. Wengine ni miungu
Kwenda bhana, wewe unanipotezea tu mda hapa.Mambo yanayothibitisha uwepo wa Mungu ni mengi sana. Nimekutajia hilo moja tu, kwamba aliyesema wanadamu tutakufa ni Mungu. Na tangu aseme hakuna aliyeweza kupinga
IMANI ni kuwa na uhakika bayana juu wa uwepo wa mambo yatarajiwayo pasipo uthibitisho.Thibitisha uwepo wake , hili ni jukwaa huru na hapa sio kanisani sawa mkuu?
Kwenda wewe hauna uwezo hata wa kuelezea unachokiamini sio tu kuthibitisha , kwa hiyo naomba hata usinijibu kama hautojali.Pole. Mungu akusaidie umjue na uone waziwazi uwepo wake.
Nataka nimjue huyo Mungu ndio naomba uthibitisho , sijue kama unanielewa lakini🤔IMANI ni kuwa na uhakika bayana juu wa uwepo wa mambo yatarajiwayo pasipo uthibitisho.
Mfano kupanga mipango ya kesho kwa imani kuwa utaiona kesho ukiwa hai mzima ,lakini kabla ya kuiona hiyo kesho unaweza ukafa na usiione hiyo kesho.
Huu uzi ni wa Kumshukuru Mungu kwa watu kwa watu wanaoamini katika uwepo wa Mungu.
kama endapo mimi ningekuwa siamini katika Mungu nisingechangia huu uzi mana ungekuwa haunihusu.Ni sawa na budha au siku wakiamua kumtembeza sanamu la mungu wao wale wahindi wameomba na kibali wanamtembeza mungu wao kwa maandamano ya amani wakimshukuru mungu wao wa kuchonga ambaye ni sanamu..halafu mimi navamia nawaambia huyo siyo mungu na kuwataka wanithibitishie kuwa huyo ni mungu..ndicho unachokufanya hapa .
Hivi "kuthibitisha" ni kufanyaje?Kwenda wewe hauna uwezo hata wa kuelezea unachokiamini sio tu kuthibitisha , kwa hiyo naomba hata usinijibu kama hautojali.
Kutoa uhakika / kujua jambo na sio imani , kujua kitu kunakomesha kuamini.Hivi "kuthibitisha" ni kufanyaje?
Hayupo kwa macho ya nyama, lakini kiroho Mungu alikwepo,yupo na atakwepo milele.(kwa wenye imani)Tumshukuru nani? Mungu muweza wa yote hayupo wala dalili ya uwepo wake tu haipo , hayo ni maneno ya kujifariji tu ya kiimani .